Wanaume wazuri ni wale waliopata malezi ya karibu ya mama zao, kweli?

bana eeh mimi sijui kupika,sitaki kupika,and i am not interested na kitu inaitwa jiko,period.
ps: mbona nasikia sikia eti wavulana wanaokuwa close saaaaaaaana na mama zao eti baadae kuna hatari wakawa sio riziki?ya kweli haya?
 
jamani mbona migahawa chungu tele? kwanza hao waliooa mbona kutwa kucha tunakula nao magengeni? nenda rose garden,breakpoint,hugo,jackies,bulyaga,rosanna etc uone mianaume iliyooa inavyofakamia michemsho na mi shwein ya kuchoma wakati wake zao wamejaa tele majumbani mwao,akifika anafunua hotpot na kuvunga vunga kama anakula kisha huyooo kwenye blanketi.
Mkuu nafikiri inategemea na hulka za watu wakiamua kufanya wanafanya tu so nafikiri ni utashi wa mtu mwenyewe
 
duhh Ivi kumbe ..
em nipe story zaid Bishanga..
kibaya zaidi duka zinakouzwa condoms hajui liko wapi,ye anapuyanga tu,hafai kabisa,Kloro kamuonya imeshindikana na kuoa hataki anajiita eti yeye helikopta popote anatua,yaani we acha tu!
 
bana eeh mimi sijui kupika,sitaki kupika,and i am not interested na kitu inaitwa jiko,period.
ps: mbona nasikia sikia eti wavulana wanaokuwa close saaaaaaaana na mama zao eti baadae kuna hatari wakawa sio riziki?ya kweli haya?
Tobaaaaaa!!
 
Si kweli hata kidogo,

Hata wanaojua kupika katika mazingira yetu hawana nafasi au muda wa kwenda jikoni.. Utaendaje kupika wakati nyumba imejaa watu...Mke, mabinti 2-3 na vijana wengine

aisee miye ilibidi nijifunze kupika baada ya mtu kuweka mgomo wa kupika!! "Nenda kapike mwenyewe!" macho yakanitoka kama sungura aliyekoswakoswa na gari!
 
Hata mimi sijui, ila nadhani kama mwanaume anajua kupika hawezi kuwa fussy kama wale wasiojua.Mwenye kujua kupika most probably hatazinguka sana na "mapishi" ya nje maana hata yeye ajua kupika!Ngoja tusikie watakaojibu wanasemaje.

Sina hakika ila nina imani kuwa hakuna mwanamume hata mmoja anayekwenda nje kutafuta mapishi...Shida yao ni moja tu, "sex" !! Ndiyo maana wakishapata wanakimbia na nguo mkononi kuwahi kwa wake zao.

Huo anayetafuta mapishi lazima awe ameamua kuuwa na mke wa 2!
 
tausi,

hapo kwenye blue...hivyo navyo ni vigezo vya mwanamume mzuri???

Na hapo kwenye red, hiyo list in exhaustive??

so unataka kupinga ndo mana miafrika hatuendelei sasa unataka kupinga nini?

Ndomana ndoa nyingi hazidumu mtu unaona kumsaidia mkewako kupika kazi au dhambi ni ujinga tena upumbafu

ushanikera wewe mimi asubuhi yangu na nahisi siku nzima itakuwa mbaya
 
Inategemea na malezi mama yake aliyompa.
...... . mtu yeyote katika mazingira sahihi kwa malezi ya mama au baba pekee/zaidi anaweza akawa mzuri tu.Kwahiyo malezi bila kujalisha ya nani ndio yanayoweza kumfanya huyo mwanaume akawa "mzuri".
Perfetto!
 
Mwanamme asiyejua kupika mbona ni hatari sana; ndio mwanzo wa unyanyasaji.. nadhani hata kwa mwanamke ni to her own interests to have a man who can cook. Matokeo yake mama akiugua au kusafiri utaletewa msaidizi wa kupika.. (vyote viwili)..

Sijajua mnaongelea mapishi yepi....:A S-coffee:
 
kibaya zaidi duka zinakouzwa condoms hajui liko wapi,ye anapuyanga tu,hafai kabisa,Kloro kamuonya imeshindikana na kuoa hataki anajiita eti yeye helikopta popote anatua,yaani we acha tu!

Mwehhhhh
Hivi kumbe na kuoa amekataa..

yawiiii Bishanga mambo ya plastic bag nayo hayajui
nlidhani kijana wenu huyo mmesha mfunza huko counter ya juu.

hahahaha hiyo helicopter tunaondoa tu blades haiendi mahali..
 

DC,dont complicate issues.... its so simple.Kama unaona siyo vigezo, potezea...
Self- reflection ikikupa kuwa huna hivyo vigezo usijiskie mnyonge lol.Jipe moyo..utakuwa na vigezo vingine......
Mbona mnapowananga kuwa ni mama's boys kwa vile wako karibu na mama zao hamjali kuwaangalia kwenye maeneo mengine?
Je kuna added value gani kwa mwanaume "kutokujua kupika" kwa mfano?

Tausi,

Hapa tunajadili hoja ambayo umeileta wewe na siyo kwamba tunasubmit confessions!

Sijajiongelea kama nina vigezo au la. Na kusema kweli, anayejua kama mimi ni mume mzuri au mbaya ni Mama DC...Na bahati mbaya, it's most likely too late for her to reverse the clock!!

Maadamu wewe ndiye mleta thread, jitahidi kujibu hoja bila ku-attack...Ila kama nimeku-offend nisamehe mdogo wangu. Lengo ni kujadiliana na kupeana mawazo.

I hope umenielewa!!
 
Mimi research yangu inaniambia wengi wao wamekuwa mabwabwa na wamefurahishwa sana na kauli ya kameruni.
Kinamama wanaharibu sana watoto wa kiume, tena naongelea kinamama wote mpaka wa hapa JF (ole wenu mbishe)

Klorokwin naona umenywesha mapema leo.. NABISHA mpaka YESU atakaporudi..

Nimekupa like ili uje usome .. Halafu naiondoa ukisha soma au kunijibu.. teh teh teh
 
Nadhani watu tunaweza kukosa mitihani hivi hivi; hili siyo suala la kupika (it is just one element). Haya tuondoe huko kupika, na kukaa jikoni. Nadhani hoja inahusu uhusiano wa malezi na mapenzi ya mama kwa mtoto wa kiume. Hoja ambayo imedokezwa ni kuwa mtoto wa kiume aliyepewa mapenzi mazuri na malezi mazuri (hatuzungumzii kudekezwa kuliko n.k - kwani si sawa na malezi mazuri) anaweza kujenga mahusiano mazuri sana anapokuwa mtu mzima hususan mahusiano yake na wanawake.

Ni sawasawa na uhusiano uliopo kati ya malezi na mapenzi ya baba kwa mtoto wa kiume na wa kike na jinsi gani inaathiri malezi na maisha ya baadaye ya watoto. Kwa mfano, mtoto wa kike ambaye hakupewa malezi mazuri na kujengwa mahusiano mazuri na baba yake anaweza vipi kuhusiana na wanaume isipokuwa in a sexual way? Baba anayemjenga binti yake kuwa confident, independent, n.k n.k anaweza kujikuta anamlea mtoto wa kike kuwa mama mzuri kwa watoto wake na mke mzuri kwa mumewe.

Sasa watu wameng'ang'ania jiko na kupika na kusahau the bigger picture: MALEZI NA MAPENZI YA MAMA KWA MTOTO WA KIUME NA JINSI INAVYOMJENGA MTOTO WA KIUME KUWA NA MAHUSIANO MAZURI NA UWEZO MZURI WA KULEA.
 
Back
Top Bottom