Wanaume wazuri ni wale waliopata malezi ya karibu ya mama zao, kweli?

Tausi Mzalendo

JF-Expert Member
May 23, 2010
1,471
722
Nilibahatika kusikiliza mazungumzo ya wadada fulani wakisema ati wanaume wazuri ni wale waliopata malezi ya karibu ya mama zao.
Wakatoa mifano ya ni vipi waliliona hilo:
Wanaume hao wanajua kupika, kulea watoto, wana huruma zaidi, wanaheshimu wanawake, wana upendo, wanajali, etc.

Hili likanifanya nifikirie na kwa kiasi nikaona lina ukweli.Nimeliona hilo kwa ndugu zangu wa kiume waliolelewa na mama zao bila kuwepo baba, au wale waliokuwa na baba lakini wakatii sana mafundisho ya mama zao.Wako independent zaidi, hawanaga makeke sana kwa wake zao, nk...
Hebu tupate mawazo zaidi kwa wale wenye uzoefu.
 
Kuna ukweli ndani yake ingawa sio wote halafu sio tu waliolelewa na mama zao tu bila kuwepo baba bali hata wale waliolelewa na wazazi wote wawili lakini unakuta mama alikuwa anajitahidi sana kuwa karibu nao na kuwapa malezi na wakatii mafundisho ya mama zao kwahiyo kwenye suala hili kiasi fulani kama asilimia 70 hivi nakubaliana na wewe.
 
Nilibahatika kusikiliza mazungumzo ya wadada fulani wakisema ati wanaume wazuri ni wale waliopata malezi ya karibu ya mama zao.
Wakatoa mifano ya ni vipi waliliona hilo:
Wanaume hao wanajua kupika, kulea watoto, wana huruma zaidi, wanaheshimu wanawake, wana upendo, wanajali, etc.

Hao wamedekezwa sana hawajui kujishughulisha mtaani tunawaita watoto wa mama wao ni kudeka deka na kuona wanaonewa kwa kila kitu
 
Naamini kuna ukweli lakini wengine wanasema ni watu waliodekezwa sana na kuharibiwa! Ndio huwa wanaitwa "watoto wa mama" a.k.a 'mama's boy'
Mwanakijiji lazima kuna watu watasema hivyo...
Hao wamedekezwa sana hawajui kujishughulisha mtaani tunawaita watoto wa mama wao ni kudeka deka na kuona wanaonewa kwa kila kitu
Hahahaha!!! Mwanakijiji umeona nilijua tu lazima watasema hivyo...
 
Nilibahatika kusikiliza mazungumzo ya wadada fulani wakisema ati wanaume wazuri ni wale waliopata malezi ya karibu ya mama zao.
Wakatoa mifano ya ni vipi waliliona hilo:
Wanaume hao wanajua kupika, kulea watoto, wana huruma zaidi, wanaheshimu wanawake, wana upendo, wanajali, etc.

Hili likanifanya nifikirie na kwa kiasi nikaona lina ukweli.Nimeliona hilo kwa ndugu zangu wa kiume waliolelewa na mama zao bila kuwepo baba, au wale waliokuwa na baba lakini wakatii sana mafundisho ya mama zao.Wako independent zaidi, hawanaga makeke sana kwa wake zao, nk...
Hebu tupate mawazo zaidi kwa wale wenye uzoefu.

Tausi,

Hapo kwenye blue...hivyo navyo ni vigezo vya mwanamume mzuri???

Na hapo kwenye red, hiyo list in exhaustive??
 
Mwanamme kujua kupika ni quality ya kusema ni mwanamme mzuri?
Hata mimi sijui, ila nadhani kama mwanaume anajua kupika hawezi kuwa fussy kama wale wasiojua.Mwenye kujua kupika most probably hatazinguka sana na "mapishi" ya nje maana hata yeye ajua kupika!Ngoja tusikie watakaojibu wanasemaje.
 
That was my biggest issue,

Huku uswahilini hiyo ni disqualification!!

Sidhani hata kuwa hicho kigezo kinakubalika kwa wanawake wengi...at least wale wengi nnao wajua sijawahi kuwasikia kutaja hicho kuwa ni moja ya vigezo vya mwanamme mzuri.

Na kwa vile kimetajwa awali zaidi ya vyote, jee inamaanisha kuwa kinabeba uzito mkubwa zaidi a vyengine?
 
Mwanamme asiyejua kupika mbona ni hatari sana; ndio mwanzo wa unyanyasaji.. nadhani hata kwa mwanamke ni to her own interests to have a man who can cook. Matokeo yake mama akiugua au kusafiri utaletewa msaidizi wa kupika.. (vyote viwili)..
 
Tausi,

Hapo kwenye blue...hivyo navyo ni vigezo vya mwanamume mzuri???

Na hapo kwenye red, hiyo list in exhaustive??

MSINIULIZE MIYE JAMANI... mimi nimewanukuu tu hao waliosema.Hii sredi inataka kudadavua kujua "uzuri wa wanaume waliolelewa na mama kwa karibu ukilinganisha na wale waliojikita zaidi kwa baba zao" .
 
Hata mimi sijui, ila nadhani kama mwanaume anajua kupika hawezi kuwa fussy kama wale wasiojua.Mwenye kujua kupika most probably hatazinguka sana na "mapishi" ya nje maana hata yeye ajua kupika!Ngoja tusikie watakaojibu wanasemaje.

Hapo umekusudiaje?

Ikiwa tunazungumzia haya haya mapishi ya kawaida, basi kama mwanamme anajua kupika nadhani atapata tabu sana kula vyakula vya mwanamke asiyejua kupika, atakuwa fussy zaidi, unless niambiwe kuwa ataamua kupika yeye mwenyewe hivyo nafuu kwa mwanamke.
 
Sidhani hata kuwa hicho kigezo kinakubalika kwa wanawake wengi...at least wale wengi nnao wajua sijawahi kuwasikia kutaja hicho kuwa ni moja ya vigezo vya mwanamme mzuri.

Na kwa vile kimetajwa awali zaidi ya vyote, jee inamaanisha kuwa kinabeba uzito mkubwa zaidi a vyengine?

nadhani mtoa mada ametoa with a light touch bila kujali sana uzito wanini kilichotajwa, vipi kimetajwa au nini kimeachwa. The point is simple kwamba wanaume waliolelewa na mama zao na kupewa yale mapenzi ya mama wanakuwa very sensitive, loving na kwa ujumla "wazuri" yaani "good". Ninavyoelewa ni kulinganisha na wanaume ambao hawakupewa mapenzi ya karibu ya mama zao.
 
Mwanamme asiyejua kupika mbona ni hatari sana; ndio mwanzo wa unyanyasaji.. nadhani hata kwa mwanamke ni to her own interests to have a man who can cook. Matokeo yake mama akiugua au kusafiri utaletewa msaidizi wa kupika.. (vyote viwili)..

Hakuna hoja ya kuwa mwanamme asipojua kupika atachochea unyanyasaji. Correlation hapo inakaribia zero.
 
Binafsi nadhani mwanaume kujua kupika katika zama hizi is a PLUS!!
Mwanaume kama hujui kupika mbona unaweza kujikuta katika hali mbaya pale huyo mkeo hayupo.
 
nadhani mtoa mada ametoa with a light touch bila kujali sana uzito wanini kilichotajwa, vipi kimetajwa au nini kimeachwa. The point is simple kwamba wanaume waliolelewa na mama zao na kupewa yale mapenzi ya mama wanakuwa very sensitive, loving na kwa ujumla "wazuri" yaani "good". Ninavyoelewa ni kulinganisha na wanaume ambao hawakupewa mapenzi ya karibu ya mama zao.

Mifano imetajwa ili kubeba hoja. Kama mifano haikubaliki, inamaanisha hakuna hoja. Kwa sababu suala la kwanza litakuwa "mwanamme mzuri ndo yupi?" ambalo litaturejesha tena kwenye mifano.
 
MSINIULIZE MIYE JAMANI... mimi nimewanukuu tu hao waliosema.Hii sredi inataka kudadavua kujua "uzuri wa wanaume waliolelewa na mama kwa karibu ukilinganisha na wale waliojikita zaidi kwa baba zao" .

Kweli???

Halafu tukimbilie kwa nani tena???
 
  • Thanks
Reactions: bht
Back
Top Bottom