Wanaume wazuri ni wale waliopata malezi ya karibu ya mama zao, kweli?

Hata mimi sijui, ila nadhani kama mwanaume anajua kupika hawezi kuwa fussy kama wale wasiojua.Mwenye kujua kupika most probably hatazinguka sana na "mapishi" ya nje maana hata yeye ajua kupika!Ngoja tusikie watakaojibu wanasemaje.
Tatizo la sie tunaojua kupika tunatend kuweka expectation kubwa zaidi kutoka kwa mwanamke! So mwanamke (mke) 'akikosea' kidogo tu kwenye mapishi, keshakuboa!
 
Sidhani hata kuwa hicho kigezo kinakubalika kwa wanawake wengi...at least wale wengi nnao wajua sijawahi kuwasikia kutaja hicho kuwa ni moja ya vigezo vya mwanamme mzuri.

Na kwa vile kimetajwa awali zaidi ya vyote, jee inamaanisha kuwa kinabeba uzito mkubwa zaidi a vyengine?

hehehheeh Gaijin, maadam wewe ni mwalimu nimekupata kwanini umeona hivyo...kumbuka hii ni mada nyepesi tu siyo academic kiviiile.Kutaja mwanzo au mwisho haimaanishi uzito. Kumbukeni uzito/wepesi ni utashi wa mtu binafsi na anavyoona yeye.

Tausi,

Hapo kwenye blue...hivyo navyo ni vigezo vya mwanamume mzuri???

Na hapo kwenye red, hiyo list in exhaustive??

Ndio tutajua kama ni vigezo au la.Kwamba ni exhaustive, nisome tena hapo chini....umeona kuna "etc, na N.K"?...BADO TU HAIJAELEWEKA?

Nilibahatika kusikiliza mazungumzo ya wadada fulani wakisema ati wanaume wazuri ni wale waliopata malezi ya karibu ya mama zao.
Wakatoa mifano ya ni vipi waliliona hilo:
Wanaume hao wanajua kupika, kulea watoto, wana huruma zaidi, wanaheshimu wanawake, wana upendo, wanajali,
etc.

Hili likanifanya nifikirie na kwa kiasi nikaona lina ukweli.Nimeliona hilo kwa ndugu zangu wa kiume waliolelewa na mama zao bila kuwepo baba, au wale waliokuwa na baba lakini wakatii sana mafundisho ya mama zao.Wako independent zaidi, hawanaga makeke sana kwa wake zao,
nk...
Hebu tupate mawazo zaidi kwa wale wenye uzoefu.
 
Mwanamme asiyejua kupika mbona ni hatari sana; ndio mwanzo wa unyanyasaji.. nadhani hata kwa mwanamke ni to her own interests to have a man who can cook. Matokeo yake mama akiugua au kusafiri utaletewa msaidizi wa kupika.. (vyote viwili)..

Si kweli hata kidogo,

Hata wanaojua kupika katika mazingira yetu hawana nafasi au muda wa kwenda jikoni.. Utaendaje kupika wakati nyumba imejaa watu...Mke, mabinti 2-3 na vijana wengine
 
Mwanamme kujua kupika ni quality ya kusema ni mwanamme mzuri?
Kwa mtizamo wa wadada kadhaa ambao nawafahamu, yes ni wanaona kama mmojawapo ya "added advantages" (nachelea kutumia neno 'quality':lol::lol:)!
 
Kweli???

Halafu tukimbilie kwa nani tena???

DC,dont complicate issues.... its so simple.Kama unaona siyo vigezo, potezea...
Self- reflection ikikupa kuwa huna hivyo vigezo usijiskie mnyonge lol.Jipe moyo..utakuwa na vigezo vingine......
Mbona mnapowananga kuwa ni mama's boys kwa vile wako karibu na mama zao hamjali kuwaangalia kwenye maeneo mengine?
Je kuna added value gani kwa mwanaume "kutokujua kupika" kwa mfano?
 
Kuna ukweli mkubwa sana kwa hili ingawa kama mama hajaweza kubalance, mtoto wa kiume anaweza kuharibika na kuwa mtu anayedeka kupita kiasi. Na kitu kingine pia kama mwanaume yuko so close na mama yake, halafu mama yake akawa ndo waleeee, huyo dada atakayeolewa mbona atakoma kuringa. maana the guy would never be independent....kila kitu lazima mama atoe mwelekeo.
 
Yaaawiii
kuna baadhi wanatoka super kweli
Ila kuna wengine balaaa bora u date mwanamke
mwanzako kuliko huyo.
 
Mwanamme asiyejua kupika mbona ni hatari sana; ndio mwanzo wa unyanyasaji.. nadhani hata kwa mwanamke ni to her own interests to have a man who can cook. Matokeo yake mama akiugua au kusafiri utaletewa msaidizi wa kupika.. (vyote viwili)..
mmmmmmhhhh Mkuu,haya bana!
 
Kuna ukweli mkubwa sana kwa hili ingawa kama mama hajaweza kubalance, mtoto wa kiume anaweza kuharibika na kuwa mtu anayedeka kupita kiasi. Na kitu kingine pia kama mwanaume yuko so close na mama yake, halafu mama yake akawa ndo waleeee, huyo dada atakayeolewa mbona atakoma kuringa. maana the guy would never be independent....kila kitu lazima mama atoe mwelekeo.
Hili nalo neno! Mama anatakiwa asidekeze bali alee kijana wake kwa kuzingatia kuwa anachopaswa kufanya ni kumsaidia kijana kujitegemea. Vinginevyo mkaka atakuwa anaamini hawezi kufanya kitu bila kumuuliza mama.Kaazi kwelikweli!

Yaaawiii
kuna baadhi wanatoka super kweli
Ila kuna wengine balaaa bora u date mwanamke
mwanzako kuliko huyo
.

KWELI...
bold ya pili..............nimeona mfano wa mtu wa hivyo!
 
Binafsi nadhani mwanaume kujua kupika katika zama hizi is a PLUS!!
Mwanaume kama hujui kupika mbona unaweza kujikuta katika hali mbaya pale huyo mkeo hayupo.
jamani mbona migahawa chungu tele? kwanza hao waliooa mbona kutwa kucha tunakula nao magengeni? nenda rose garden,breakpoint,hugo,jackies,bulyaga,rosanna etc uone mianaume iliyooa inavyofakamia michemsho na mi shwein ya kuchoma wakati wake zao wamejaa tele majumbani mwao,akifika anafunua hotpot na kuvunga vunga kama anakula kisha huyooo kwenye blanketi.
 
Kwa mtizamo wa wadada kadhaa ambao nawafahamu, yes ni wanaona kama mmojawapo ya "added advantages" (nachelea kutumia neno 'quality':lol::lol:)!

Haya hawajui kuwa inabidi wawe wazuri sana kupika au watarudishwa nacho jikoni kila jioni.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Inategemea na malezi mama yake aliyompa.
Anaweza akawa very dependent kwa mama yake, mpaka kimawazo, ndo pale unakuta mwanaume hata kununua kitanda/sofa mpya anakwambia "subiri mpaka nizungumze na mama".Anaweza akawa too sensitive, akawa lege lege na mdekaji sana, akawa hawezi kazi yoyote (shauri ya kudekezwa) n.k.

Kwahiyo ukikutana na mwanaume anaesema "nampenda sana mama yangu jiandae either kuwa dissapointed au kuwa impressed na namna atakavyokutreat wewe kama mwanamke.
Pia hao wasiolelewa na mama zao wanaweza wakawa na hizo quality ulizoanisha kwamba ni nzuri ,kutegemea na malezi waliyopata toka kwa baba zao. Ikiwa baba yake atamlea kwa misingi inayoheshimu wanawake then atakua kijana/mwanaume anaehishimu wanawake, kama sio basi hatokua nayo hiyo heshima labda kama atajijenga mwenyewe tofauti na malezi aliyopata.

Kwahiyo sidhani kama ni sahihi tukianza kupiga chapa kwamba hawa watakua hivi na wale watakua vile. . . mtu yeyote katika mazingira sahihi kwa malezi ya mama au baba pekee/zaidi anaweza akawa mzuri tu.Kwahiyo malezi bila kujalisha ya nani ndio yanayoweza kumfanya huyo mwanaume akawa "mzuri".
 
Hapo umekusudiaje?

Ikiwa tunazungumzia haya haya mapishi ya kawaida, basi kama mwanamme anajua kupika nadhani atapata tabu sana kula vyakula vya mwanamke asiyejua kupika, atakuwa fussy zaidi, unless niambiwe kuwa ataamua kupika yeye mwenyewe hivyo nafuu kwa mwanamke.
Nadhani kuna wakati inabdi tukubaliane kuwa tuna ltifestyles za aina mbalimbali. Wnaume wanachange diapers,wanalisha watoto......
Wengine, wanapika etc.... kuna watu wapo na mashost wa kizungu, wengine wameolewa na hao wazungu. Pia kuna couples nyingi zipo just westernized. So, cooking might be a plus, depending on lifestyles
 
Hivi kila nikiingia jikoni kupika how do you feel?

Inapendeza zaidi unapowalisha watoto wakati mi na umwa
na nilipo kuwa safarini.
Lakini sasa sipendi kabisa, napenda zaidi tukiwa wote jikoni.

au nikikununia kalale huko huko jikoni..
 
Kupika is one thing...na kuosha masufuria je? Bora niende kula kwenye mikahawa. Chips mayai, nyama za mshikaki, mbuzi katoliki, ugali nyama choma...so many varieties I can't get tired!!
 
Back
Top Bottom