Safina
JF-Expert Member
- Jun 18, 2009
- 497
- 64
Habari za mchana wana jamvi.
Hebu sikilizeni kisa hiki, huwa nina ki-grocery changu, sasa hapa huwa nina mashoga zangu kibao, kila mtu anakuja na la kwakwe kuhusu kutendwa, mengine naona ya kawaida lakini hili jamani!!!!! Limenichosha nimeona niwashirikishe.
Huyu shoga yangu kaja hapa mchana huu analia. Kuna jamaa alijifanya anampenda kwa dhati ya moyo wake, katika kukaa, kaa kwenye hilo penzi lao kwa takribani miezi mitatu kwa jamaa kuonyesha mapenzi mazito haswa mpaka wenzake wakawa wanaona mamsapu kapata bwana wa ukweli. Kumbe jamaa alikuwa na yake kichwani, kamdanganya dada wa watu, eti kuna biashara huwa anafanya lakini amekwama, hivyo anamwomba mdada amkopeshe shilingi 6m. Mdada hakuwa nazo, jamaa akamwambia kwa sababu umeajiriwa naomba unikopee ofisini kwako nitakuwa nikirudisha kidogo, kidogo, mdada wa watu kakopa kampa jamaa. Jamaa baada ya kushika kitita mkononi, kidogo kidogo mapenzi yakaanza kupungua na mwisho yakaisha kabisa, kwani hivi sasa dada akimpigia simu hapokei, akipokea akiulizwa mbona siku hizi hauonekani anasema yuko bize. Mdada si akaamua kujitoa fahamu kumfuata huko nyumbani kwake, akakuta jamaa full shangwe na mwanamke mwingine na deni yeye anaendelea kukatwa kwenye mshahara wake kila mwisho wa mwezi. Mwanaume hajajali kuwa kafumaniwa wala nini? Sana sana alimuuliza unashida gani, binti akamwambia inakuwaje leo hii unaniuliza nimefuata nini wakati mimi ni mpenzi wako jamaa akamwambia una kichaa na maneno mengine mengi ambayo siwezi hata kuendelea kuyaandika. Wanaume jamani, jamani mbona mnatutenda vibaya, vibaya hivi why? Kwanini?