Wanaume wanatuchosha lakini hatusikii na wala hatuoni.

Matatizo ya kuamini mtu haraka....jamani miezi mitatu ya mapenzi unamkubalia ombi kubwa kiasi hicho? Na umefunguka mapema sana yaelekea binti alitoa siri \zake zote kuwa ana uwezo wa kupata huo mtaji au mkaka alikuwa anamlia timing..................................duh kweli kuna haja ya kumshirikisha MUNGU katika kuchagua wenzi wetu!!

Tamu ya Peremende aijuaye anayeimumunya.
 
Nigeshauri tukumbuke maana halisi ya haki sawa kijinsia. Hapo zamani wanawake walikuwa wanayafanya haya kwa wanaume kwa wale waliokuwa wakiudhulia dansini au sehemu za manunuzi ya vitu mbali mbali watakumbuka kuwa wanaume walikuwa wanaghalamika sana kwa wanawake na hakukuwa na guarantee ya mapenzi kwani mwisho wa siku walikuwa wanakimbiwa na kuanza kusakwa na kwakuwa aliyetapeliwa ni mwanaume basi akimtia mkononi atampa kipondo havy!

Sasa twende kwenye mfumo wa kisasa ambapo wanawake wanashindana na wanaume kushikilia nguzo za uchumi meanwhile wapo wanaume ambapo deals zote zina bounce wanaamua kuwa tegemezi hapo tambua kwamba si kila atakayekufuata amekuja kimapenzi bali kikazi zaidi, si ajabu anakuwa ameagana na mpenzi wake kwamba subiri kuna demu namchuna mambo yako yatakuwa fit yaani anampelekea mshiko lakini pia na huyo anayepelekewa kwa maana ya demu naye anaye mwanaume mwingine ambaye akipewa naye anampelekea!

Hii ndiyo tunaita ngoma draw anayetoa cheni ya bandia naye anapewa hela bandia!!
 
Amu curse atarudi mwenyewe kuomba msamaha na kurudisha

Mie naamini cursing a person works as long as wewe huna makosa

Mpe pole
 
Sio kila kitu mnatulaumu tu,huyo rafiki yako ni mjinga.miezi 3 unmkopesha hela??mi hata ndururu sikupi.mnabaki kusema sisi ni waongo ila na nyie mmezidi kudanganyika kama watoto
 
kwanini wadada mnashangaa 3 months ?? hata iwe miaka mitano hata 20 kama hakuna ndoa msitupe hata mia 100. mbona hivyo bana???
 
Ni kweli huyo mwanaume ni tapeli hasa. Lakini inashangaza wadada hapa wanapoimba wanaume wanaume! Au kwa sababu huyo kachukua nyingi kwa mara moja? Wasichana wengi wanakula na kufuja hela za wanaume huku wakijua mioyoni mwao hawana mpango na wanaume hao, ukiwauliza utasikia 'si kanipa mwenyewe? Kwani nimemlazimisha?' si zinamuwasha, nk. Hapa kila mdada ni malaika hajawahi kutumia hela ya mwanaume huku akijua hana feelings zozote za mapenzi naye! Wote tunaujua ukweli, wadada wengi ni matapeli sawa na huyo jamaa, labda tofauti tu ni amount. Wangapi wanagarimiwa masomo, nyumba/vyumba, gari, mavazi, misosi, vinywaji na vitu kibao lakini mwisho wa siku wanawatema wanaume tena kwa kejeli kibao?! Huyo jamaa ni mwizi kamili, lkn hiyo isitumike kutuita wanaume wote majina ya kila namna. Wasichana wanatumia hela za wanaume kwa udanganyifu zaidi ya wanaume wanavyotumia za wanawake! Vumilieni hadi usawa utimie!!
 
Back
Top Bottom