Wanaume wakibongo kwenda nje ya ndoa.

Darwin

JF-Expert Member
May 14, 2008
908
56
Kiukweli kuna hili jambo linanikera sana.
Mama yangu ni mswahili baba Irish/dutch nakuna haya machache yanayonikera kwenye blog ya mdada mmoja wa TZ kaolewa na Caucasian .

Huwa kwa asilimia kubwa anachoongelea nikwamba wanaume wakibongo huwa niwadanganyifu sana kwenye ndoa [kutembea nje za ndoa na wanawake wengine].

Mimi nimeishi Africa na Europe nanimeona ndoa nyingi za watu wa Europe ambazo zilivunjika kwa wanaume wakizungu kwenda nje ya ndoa.

Mpaka sasa siamini kwamba ni wanaume wakiafrica tu ndio wanaoenda nje ya ndoa.

Hivi kwenda nje ya ndoa nikutokana na rangi au ni tabia ya mtu?

Kama ni rangi ya uafrica mbona Europe kuna madanguro mengi tu? na wengi wa wateja sio kwamba wako single?.
 
sio blog ya mange hio??? ndio inatukuza wazungu!...waache malimbukeni tu hao...:A S 13::A S 13::wink2:
 
Yeye ndo anavyoona,mi kwa kuwa nawafahamu wanaume wa kiafrica na hasa wa kitanzania zaidi nakubaliana nae kuwa wengi wao wanakwenda nje ya ndoa zao,imefika hatua sasa si kitu cha ajabu tena......wanaume wa mabara mengine wapo wanakwenda nje ya ndoa lakini hawajafikia wa kiafrika.....hapa hata kwa risasi sikanushi....l.o.l
 
Mange kiboko,yaani anafanya watu waone kuwa ukiwa na mzungu maisha yananyooka,unaenda paradiso,haonyeshagi the other side of wazungu,watu wanaolewa na mijizee ya kizungu wakitamani kuwa kama Mange wasijue bahati ya mtu si yao!!!!
 
Yeye ndo anavyoona,mi kwa kuwa nawafahamu wanaume wa kiafrica na hasa wa kitanzania zaidi nakubaliana nae kuwa wengi wao wanakwenda nje ya ndoa zao,imefika hatua sasa si kitu cha ajabu tena......wanaume wa mabara mengine wapo wanakwenda nje ya ndoa lakini hawajafikia wa kiafrika.....hapa hata kwa risasi sikanushi....l.o.l

Africa hakuna legal madanguro, Europe yapo tena mengi tu. Unataka kusema wateja wote ni single?

Kwenda nje ya ndoa mimi ninavyoona ni tabia ya mtu na hulka zake tu lakini huwezi ukasema Afrika wanaongoza, kwa utafiti upi uliofanya?
 
Tatizo la Wanawake mmekuwa "hypotinized" na tamaduni ambazo hamzijui...

Siyo Tanzania tu - bali DUNIA nzima - Kila mwanaume aliye katika ndoa ni LAZIMA atoke nje ya ndoa yake - That is natural!

Lazima mwanaume awe na wanawake zaidi ya mmoja wanaoweza kutimiza haja zake za mwili at any given time "t"!
 
ni kweli ni sawa na kuona wanawake zaidi ya 20 ml watanzania, kisha ukaona wanawake wazungu wasiofika kumi wabaguzi wa rangi kwelikweli, hivyo hawataki hata kuchangamana na watanzania wakaja na kejeli zao za kuwakejeli wananawake wenzao wa kitanzania kuwa ni wachafu. na kwa ukaibuka na kusema wanawake wote wazungu ni wabaguzi wa rangi.

huyo mange siku akikabidhiwa divorce mume atakapo amua kuoa mzungu mwenzake au siku akirudishwa kwao naye akaonekana kama house girl wa familia ya mumewe ndipo atawajua wazungu.
 
Yeye ndo anavyoona,mi kwa kuwa nawafahamu wanaume wa kiafrica na hasa wa kitanzania zaidi nakubaliana nae kuwa wengi wao wanakwenda nje ya ndoa zao,imefika hatua sasa si kitu cha ajabu tena......wanaume wa mabara mengine wapo wanakwenda nje ya ndoa lakini hawajafikia wa kiafrika.....hapa hata kwa risasi sikanushi....l.o.l

U've spoken with lots of confidence, nadhani haitakuwa sawa kukubishia!
 
Uko sahihi sana mkuu, tukumbuke scandal za akina john terry, wyne rooney, bill clinton hawa ni wachache ukifanya utafit utakutana nao wengi tu.
 
Tatizo la Wanawake mmekuwa "hypotinized" na tamaduni ambazo hamzijui...

Siyo Tanzania tu - bali DUNIA nzima - Kila mwanaume aliye katika ndoa ni LAZIMA atoke nje ya ndoa yake - That is natural!

Lazima mwanaume awe na wanawake zaidi ya mmoja wanaoweza kutimiza haja zake za mwili at any given time "t"!
Kyabushaija hiyo nakataa kabisa kwamba si kweli, eti kila mwanaume lazima atoke nje ya ndoa yake!!!!Kwanza kutoka nje ya ndoa ni kuwa irresponsible, kuna mambo mengi ya kufikiri, HIV, creation of extended families etc etc.Kwa hiyo wapo baadhi ya watu ni careless na future zao, wanapenda kujikoroga baadae watakuja kujutia matendo yao. Tukirudi kwenye mada, kwenye kutenda hiyo dhambi hakuna ubaguzi si wabongo au wazungu wala kabila gani au rangi gani wote wanaweza kutenda dhambi ya uzinzi. Lakini nakuhakikishia bado kuna watu waaminifu kwenye ndoa zao na wanamuogopa Mungu kutenda dhambi. Mbarikiwe.
 
Africa hakuna legal madanguro, Europe yapo tena mengi tu. Unataka kusema wateja wote ni single?

Kwenda nje ya ndoa mimi ninavyoona ni tabia ya mtu na hulka zake tu lakini huwezi ukasema Afrika wanaongoza, kwa utafiti upi uliofanya?

wewe kwa utafiti upi uliofanya hadi ukaweka hii thread hapa??kuna utofauti wa wewe unavyoona na wengine wanavyoona,na mi sizungumzii navyoona bali hali halisi...........katika maelezo yangu sikumaanisha huko Europe hawatoki ila levels za kutoka nje ya ndoa zinatofautiana kati ya Europe na Africa na utafiti nimeufanya......najua nachosema!!!
 
Tatizo la Wanawake mmekuwa "hypotinized" na tamaduni ambazo hamzijui...

Siyo Tanzania tu - bali DUNIA nzima - Kila mwanaume aliye katika ndoa ni LAZIMA atoke nje ya ndoa yake - That is natural!

Lazima mwanaume awe na wanawake zaidi ya mmoja wanaoweza kutimiza haja zake za mwili at any given time "t"!

Nakubaliana na wewe kwamba tatizo la kutoka nje ya ndoa sio la waafrika peke yao, ni tabia ya mtu! ILA, sikubaliani na wewe kwenye hapo juu kwa red....sio kila mwanaume, hii si kweli, unaweza ukasema wengi, lakini kila mwanaume sikubaliani na wewe!
 
Kyabushaija hiyo nakataa kabisa kwamba si kweli, eti kila mwanaume lazima atoke nje ya ndoa yake!!!!Kwanza kutoka nje ya ndoa ni kuwa irresponsible, kuna mambo mengi ya kufikiri, HIV, creation of extended families etc etc.Kwa hiyo wapo baadhi ya watu ni careless na future zao, wanapenda kujikoroga baadae watakuja kujutia matendo yao. Tukirudi kwenye mada, kwenye kutenda hiyo dhambi hakuna ubaguzi si wabongo au wazungu wala kabila gani au rangi gani wote wanaweza kutenda dhambi ya uzinzi. Lakini nakuhakikishia bado kuna watu waaminifu kwenye ndoa zao na wanamuogopa Mungu kutenda dhambi. Mbarikiwe.

Mtumishi nakubaliana na wewe...100%. Barikiwe na wewe pia!
 
Hiyo research kaifanyia wapi na amepublish journal gani? Aache ushamba wake. yeye aseme alikuwa anatafuta mzungu tu basi na siku akigundua huyo kitimoto wake anatoka nje ya ndoa atakufa kwa BP. wanaume wa kitanzania wapo wengi tu ambao hawatoki nje ya ndoa. kutoka nje ya ndoa ni hulka ya mtu husika. Je wanawake wanaotoka nje ya ndio ni wote?
 
angalia kipindi kimoja kinaitwa cheaters ndio utajua wazungu nao wamo sana
 
Nakubaliana na wewe kwamba tatizo la kutoka nje ya ndoa sio la waafrika peke yao, ni tabia ya mtu! ILA, sikubaliani na wewe kwenye hapo juu kwa red....sio kila mwanaume, hii si kweli, unaweza ukasema wengi, lakini kila mwanaume sikubaliani na wewe!
kerrenH,mea culpa (unagonga kifua) mea culpa (unagonga tena) tafsiri yake 'nimekosa mimi,nimekosa mimi, kwa mawazo,maneno na matendo,ndo maana nakuungamia Mwenyezi Mungu..... Hii maana yake nini? maana yake ni kwamba kuzini(adultery) si lazima mlalane nje ya ndoa, kuwaza tu ni zinaa tosha .Sasa Kerren nionyeshe mwanandoa mmoja tu humu duniani ambaye hajawahi kutamani mwanamke mwingine,mmoja tu unionyeshe!
 
Yeye ndo anavyoona,mi kwa kuwa nawafahamu wanaume wa kiafrica na hasa wa kitanzania zaidi nakubaliana nae kuwa wengi wao wanakwenda nje ya ndoa zao,imefika hatua sasa si kitu cha ajabu tena......wanaume wa mabara mengine wapo wanakwenda nje ya ndoa lakini hawajafikia wa kiafrika.....hapa hata kwa risasi sikanushi....l.o.l

Nadhani itakuwa sahihi zaidi ukisema kwamba hata wanawake wa kiafrika na hasa wa kitanzania (sio wote) wanakwenda sana nje ya ndoa zao. Hili lina -apply kote kote
 
Back
Top Bottom