Wanaume wa Dar na mbwembwe za kupiga mazoezi barabarani

Youngblood

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
18,967
55,067
Basi bwana juzi baada ya kipindi kirefu kupita nikiwa nimejichimbia huko kijijini kwetu Ushongo pangani, nikaona isiwe tabu niende mjini kati Daslam kwaajili ya kununua mahitaji mbalimbali kwa ajili ya sikukuu ya Christmas na mwaka mpya pamoja na mambo ya shule Januari.

Basi bwana nipo zangu ndani ya Tashreef chombo imeivaa full AC, tumefika Tegeta Nyuki kuna abiria alikuwa anashuka pale, jambo la kwanza baada ya kufunguliwa mlango ni harufu kali ya uozo na vinyesi baada ya watu kuzibua mitaro, unajua tena Dar kipindi cha mvua ndo wakati wake. Mji unanuka... basi nikaona isiwe tabu maadamu wenyewe wamezoea na supu ya pweza wanapiga bila kutapika sio mbaya.

Gari ikatembea mpaka stendi ya Magufuli pale wakashuka baadhi ya abiria wengine tukaanza safari kuelekea Magomeni mapipa, kufika pale sijui ni kimara au mbezi kwenye lile daraja la kuvuka kwa miguu naona wanaume kibao na vibukta vyao eti wanapanda ngazi na kushuka wanafanya mazoezi

Nikajisemea moyoni hawa kweli wanafanya mazoezi au show off tu. Nikavunga zangu nikamwambia konda usisahau kunishusha shekilango mana nimebeba bata wangu wawili na mahindi mabichi nampelekea mjomba kama zawadi,mana nitapata nao shida kama nikipitishwa kituo.

Basi ile njia nzima kuanzia stendi ya magufuli ni wanaume tu na viboksa wanakimbia pembezoni mwa barabara na mbwembwe kibao za kupiga push up na kuruka ruka kamba huku wakipishana na magari na pikipiki.

Cha ajabu wengi wana vitambi vikubwa sana, ila viatu walivyovaa vimechakaa ikimaanisha hayo mazoezi wameanza siku nyingi lakini workdone inaonyesha kuwa ni zero bin sufuri, mana hawafanyi mazoezi bali wanaturingishia vibukta na vi Nike na Adidas uchwara vya mlimani city.

Nikakumbuka kule kwetu pangani wanaume kijiji kizima hakuna ambaye hana six pack, wakati huko mjini Daslam nasikia kuna watu wanawekewa mapulizo tumboni ili wapungue uzito na vitambi,nikacheka sana.

Kule kwetu ushongo watu tunachana mbao za Minazi kwa kututumia ile misumeno ya juu- chini na kupalilia mkonge asubuhi,na mchana wa jua kali bila shida.

Nikapata wazo moja kichwani kwamba kinachowasumbua wanaume wa dar ni tamaa, majivuno na kupenda mteremko katika mambo yanayohitaji mabadiliko na juhudi, mwanaume wa kweli huwezi kutoka nyumbani ukaenda Mloganzila kuweka puto tumboni ili upungue uzito, inamaana umeshindwa kujizuia kula supu ya pweza na chips mayai rojorojo.

Nikajiuliza moyoni hivi hawa jamaa wanaoruka humu mitaroni wakijifanya wanafanya mazoezi wangekuwa na nia kweli si wangetafuta mashamba huko chanika ndani ndani au bagamoyo wakalime kila weekend waone kama vitambi vitabaki

Nikakumbuka wanaume wengi wa jiji la Daslam maneno mengi lakini uvumilivu na juhudi hawana, mana nimewahi kusikia panya road watatu walifunga mtaa mzima huko buza huku wanaume kwa wanawake wote wamejifungia ndani siku nzima, wakati nakumbuka kipindi hicho nina umri wa miaka kumi tu niliuwa chatu kule kijijini kwetu bila hata kuwa na kiwembe.

Kwaherini mpaka kipindi kingine tena nikija mjini tena, wapeni hai wale majamaa wavaa vibukta wakiwa na vi mackbook/laptop wanafanya kazi wakiwa night club, bado mpaka leo najiuliza huwa wanafanya kazi zipi nashindwa kupata majibu.
 
Mkuu umebebelea bata alafu unasema dar Kunanuka

Huyo bata wako ulimvisha nepi kutoka ushongo kipumbwi au ulimuacha anaharisha mchana kutwa
Sina tabia ya kusafiri na bata au kuku kwenye gari, ila mjomba ameniomba zawadi nifanyeje sasa, lakini pia Bata walifungwa vizuri kwenye box so hakuna abiria alilalamika kero yoyote ya harufu.
 
Sina tabia ya kusafiri na bata au kuku kwenye gari,ila mjomba ameniomba zawadi nifanyeje sasa,lakini pia Bata walifungwa vizuri kwenye box so hakuna abiria alilalamika kero yoyote ya h
Sina tabia ya kusafiri na bata au kuku kwenye gari,ila mjomba ameniomba zawadi nifanyeje sasa,lakini pia Bata walifungwa vizuri kwenye box so hakuna abiria alilalamika kero yoyote ya harufu.
Mkuu jiongeze hizo bata unasema hujasikia harufu na wakati Kila baada ya dk 5 anaharisha hili nalo mlichunguze watu wa shamba mnanini mmekosa Cha kubeba mpaka mubebe bata kwenye usafiri wa umma
 
mkuu mbona km unasimanga watu aiseé alafu km una hasira sana na vijana wa dar ambao Kwa mujibu wako vibukta wanavyovaa ndio nguo za mtoko ,ingali uko kwenu mnavalia ndan ya suruali km boksa

Embu waache vijana wa dar wanaendaa na wakati c wote lazima wakalimee..
 
Sasa hivi jioni Wanamalizia kunyoa mkuu watakuja uparuane nao...

20231025_063637.jpg
 
Back
Top Bottom