Wanaume tuwapende na kuwajali wake zetu; Pitia hapa ujifunze kitu

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,490
WANAUME TUWAPENDE SANA WAKE ZETU ZAIDI

Baba alinisisitizia kuchukua likizo, kazini nilikua na mambo mengi sana lakini aliniambia kuwa mwezi mmoja wa kuwa kazini naweza ujutia maisha yangu yote kwani yeye hatavuka mwezi atakufa. Kwa namna alivyokua anaongea mpaka niliogopa, Baba yangu hakua mtu wa kudekadeka mara nyingii alijifanya mgumu hata alipokua anaumia sana, nilipomsikia anaongea vile nilijua kuwa kuna kitu na nahitajika kwenda kumuona.

Nilichukua likizo na kwenda nyumbani, kweli alikua anaumwa, alikua kaisha, alikua kakonda afya imedhoofu na alikua hawezi hata kunyanyuka. Alikua mpole anaongea taratibu mnyonge sana, kwa mtu aliyekuwa anamfahamu Baba yangu angemuonea huruma na hata kutoa machozi kwa kumuona vile. Nilimuangalia kwa huruma lakini alilazimisha tabasamu, hakutaka kuonekana mnyonge.

Aliniambia kuwa wewe ndiyo mtoto wangu wa kwanza, una wadogo zako sita, wa kike wawili na wanaume wanne, kuna kitu nataka nikufundishe kabla sijafa ili uje kuwa Bora na si kuwa kama mimi. Nilimuitikia nikidhani kuwa kuna kitu ataniambia, lakini mpaka likizo inaisha hakuniambia kitu chochote, nilishangaa na kumuuliza mbona kaniahidi kuniambia kitu lakini hajaniambia na likizo inaisha natakiwa kurudi kazini.

Alitabasamu na kuniambia kuwa ameshaniambia. Nilifikiria sana nikijaribu kukumbuka kama kuna kitu labda aliniambia nikakisahau lakini sikukumbuka, nilifikiri sana na sana sikukumbuka chochote, nilishindwa nikamuambia Baba mbona sikumbuki chochote. Alitabasamu tena, huku akiongea kwa shida aliniuliza nimekaa pale kwa siku ngapi, nilimuambia siku 23, akaniuliza wewe una Shangazi wa ngapi nikamuambia wawili na Baba wadogo nikamuambia watatu.

Akaniuliza tangu nikae hapo walishakuja mara ngapi, nilimuambia Shangazi mmoja alikuja mara tatu, kuna mwingine kila baada ya siku mbili anakuja, Baba wadogo aliyekuja ni mmoja mara moja kwani wote wapo mjini na familia zao. Alitabasamu tena na kuniuliza vipi Mama yako tangu uje hapa yeye kaja mara ngapi? Nikashangaa na nikidhani labda Baba kachanganyikiwa nilimuambia.

“Baba, Mama mbona kila siku yuko hapa, ndiyo anakupikia, anakusafisha, anakufanyia kila kitu? Ina maana umesahau?” Nilidhani Baba akili zimeanza kupotea lakini alitabasamu na kuniambia “Hapana mwanangu, sikusahau leo kuwa Mama yako hayupo, nilisahau kipindi namuoa kuwa hayupo. Niliendekeza ndugu na kuwajali, niliwapa kila kitu huku Mama yako nikimfungia ndani, nilikuwa nikimpiga kwa maneno tu ya ndugu zangu.

Alivumilia kila kitu kwakuwa hakuwa na pakwenda lakini leo yeye ndiyo yuko na mimi na ananihudumia kwa kila kitu wakati mimi sina pa kwenda. Ndugu zangu wana maisha mazuri lakini wapo na familia zao wanakuja kunisalimia wakati Mama yako ananiogesha na kunilisha. Nyie wanangu mpo huko mna maisha yenu, siwalaumu lakini ukweli ni kuwa mimi si jukumu lenu hata kuja kunisalimia mnapangiana zamu.

Lakini Mama yako hana cha zamu, akilala akiamka yuko na mimi, akigeuka ni mimi, akila ni mimi, akipumua ni mimi, nikijisaidia ni yeye, nikitapika ni yeye, nikidondoka ni yeye. Wakati zamani nilikua namuambia kama umenichoka basi ondoka, lakini leo siwezi hata kujisaidia bila yeye. Mwanangu wapende ndugu zako lakini kama hutaki kufa kwa unyonge kama mimi basi Mpende mke wako zaidi, huyo ndiyo Mungu akipanga utazeeka naye.

Ndugu watakuja kukusalimia tu na kukupa pole lakini wakubeba kinyesi chako ni mkeo. Mfanye abebe huku akikumbuka mema uliyomfanyia na si mateso uliyompa, mwanangu ukimnyanyasa mwanamke lazima utateseka tu, akitangulia kufa yeye utabaki na watoto wanaokuchukia kwakuwa ulimtesa Mama yao, hata kama hawakuona lakini utakua unaumia kila siku ukiwaona na ukitangulia wewe basi yeye ndiyo atakua karibu kukuhudumia, mheshimu sana mke wako.”

Baba alimaliza kuongea, akaniambia nimuache apumzike. Siku iliyofuata niliondoka kurudi mjini lakini sikufika, nilipigiwa simu kuwa Baba yangu kafariki dunia. Nilirudi kwenye msiba, ndugu zake walikuja na kulia tena sana. Lakini baada ya siku mbili wote walirudi kwao na familia zao, alibaki Mama tu, nilijikuta badala ya kulia natabasamu kwani Baba alinifundisha kuwa watakuja watalia na mwisho wa siku atabaki mkeo na wanao.
 
Kila mmoja (ndugu, jamaa na marafiki) ana nafasi yake. Muhimu kujua mipaka na nafasi yao.
 
Unazungumzia wake wa karne gani mkuu?,ni hawa hawa tuma na yakutolea ama unaandika tamthilia mkuu?
 
Ndio umpate Mwanamke aliyefundwa Na Bibi Yake Jinsi ya Kuishi na Mwanaume. Si hawa wanaofundishwa Jinsi ya Kushindana na Mwanaume. Huyo Mama yako Alifundwa hakufanyiwa Kitchen Party ila Alifundwa
 
katika UISLAM mwanaume jukumu lako ni mke wako na watoto kuwalea na kuwatimia mahitaji yao mpaka kufa kwako

UISLAM ukaenda mbali zaidi ukishamuozesha MTOTO wa kike huyo si wako tena ni wa mkwewako
na hana maamuzi naye yote huyo mkwewe na wewe MUME unapaswa umlee mkeo kama yai kama alivyolelewa na wazazi wake kwa kumpa huduma zote stahiki na nzuri

Ama hakika kusudio LA MWENYEZIMUNGU katika hiloni kuwa mkeo ndie atakayekufaa UZEENI
ni Kama hapo mamaaki alivyomfaa MZEE WAKO UZEENI

NA MIMI NAKAZIA TUWAPENDE WAKE ZETU NA TUWAESHIMU ukitakujua ukweli wa hiki kisa Nenda wodi ya WANAUME hosptri za UMA za SERIKALI hutapata ukweli wa KISA HIKI
 
Baba yako alikuwa na mke mzuri, anayasema hayo kwa Msingi wa mke aliyekuwa naye, wewe oa tatizo halafu fuata principles za Baba, utakuja kulia.
 
naunga mkono asilimia 201% jamani wenza tupendane na kujalianaaa, madhaifu kila mtu anayooo, tusipende kuchunguza/kutafuta madhaifu kwa wenza wetu tuuu.... mahusiano imara hujengwa na namna unavyopokea madhaifu ya mwenziooo...

wanaume wanachofuwata kwa wanawake ni motooo sema aaa motoooo .......hahaa so hot insideee ooor
 
Mkuu kila Mtu mpenafasi yake katika Maisha awe Ndugu, Mke, Jamaa na Marafiki.

Huwezi jua nani atakufaa hapo baadae
 
Dah unawzungumza hawa wake zetu amabao wana wanaume kadhaa wanatugongea?
Unawzungumza wake amabao wakishakua kwenye vifua vya wanaume zao vitandani wanatoa aibu zote za waume zao?
 
katika UISLAM mwanaume jukumu lako ni mke wako na watoto kuwalea na kuwatimia mahitaji yao mpaka kufa kwako

UISLAM ukaenda mbali zaidi ukishamuozesha MTOTO wa kike huyo si wako tena ni wa mkwewako
na hana maamuzi naye yote huyo mkwewe na wewe MUME unapaswa umlee mkeo kama yai kama alivyolelewa na wazazi wake kwa kumpa huduma zote stahiki na nzuri

Ama hakika kusudio LA MWENYEZIMUNGU katika hiloni kuwa mkeo ndie atakayekufaa UZEENI
ni Kama hapo mamaaki alivyomfaa MZEE WAKO UZEENI

NA MIMI NAKAZIA TUWAPENDE WAKE ZETU NA TUWAESHIMU ukitakujua ukweli wa hiki kisa Nenda wodi ya WANAUME hosptri za UMA za SERIKALI hutapata ukweli wa KISA HIKI
Umenena vizuri Sana mkuu,kweli wanaume tunatakiwa tuwapende wake zetu kwa dhati
 
Back
Top Bottom