Wanaume tunapenda hatari

bahati93

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
1,141
2,017
Kuishi kwa hatari ndio jadi yetu Wanaume. Tokea utotoni michezo yetu mingi ilihusu mapambano, kuuwana, na kuchinjana. Nakumbuka tulikuwa tukipiga kelele kali sanaa kutokana na hashishi iliyoletwa na michezo yetu ya maigizo.

Sasa tumekuwa wakubwa mambo ya kuigiza hamna tena, ila kuna vitu viwili vya Hatari Mwenyezi Mungu katujalia. Vitu vyenyewe ni Vita na Mwanamke.

Sina haja ya kumwelezea sanaa Mwanamke na hatari kubwa aliyobeba. Nachoweza kusema ni kwamba Tumeshuhudia baadhi ya makamanda wenzentu wakijitoa uhai kisa mwanamke, wengine wakifilisika, hakika hiki chomboo ukiwa nachoo ni mwisho wa kiu ya hatari kwani mda wowote waweza pigwa tukio. Lakini, jadi yetu ni vitu vya hatari, hivyo hivi vyombo Wanaume wa kweli tutavichukua na kuviweka ndani.

Vita ni mchezo wa kiume wenyee hatari kubwaa sana, kwani matokeo ya kushindwa hupelekea mchezaji kulipia Uhai wake na matokeo kwa washindi ni kula mbususuu Mpaka mishale kuwa butu. Utofauti kati ya hizi hatari mbili, vita na mwanamke ni Kwamba ndani ya vita kuna mwanamke asiye na hatari. Tokea mwaka 1945 Wanaume dunia nzima wana Kiu kubwaa sana ya kucheza huu mchezo, ndio maana mwaona karibia kila kona Ya Dunia hivi sasa kuna Wanaume wapo kucheza.

Nawaza miaka thelasini mbele, nadhani wanaume wa Kenya na Tanzania tutauchezaa huu mchezo, na kombe litakuwa mlima Kilimanjaro na rasilimali zake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom