Wanaume msiache kusoma hapa

vincentmwakisyala

New Member
Jan 30, 2023
3
36
Kuna Jambo ambalo natamani tukumbushane leo, na Jambo lenyewe linaitwa MWANAMUME. Ikiwa ni mwanaume ama ni mzazi wa mtoto wa kiume si vema kupita bila kusoma huenda ukapata kitu, Karibu.

Nianze kwa kusema mwanaume ameumbwa tofauti sana na mwanamke, mwanaume ndiyo asili ya mwanamke na uzao wake. Mwanaume ni mfano wa utukufu wa Mungu na Kristo kwa kanisa. Mungu anaitwa Baba ila aina maana ana jinsia kwa namna ya kibanaadamu ila anaonyesha mfano kwa namna ya kibinaadamu ili tuelewe anapojiita Baba ana maana gani.

Tukirudi katika historia ya Kwanza Mwanzo 2 hadi 3, utagundua kuwa Mungu alimpa Enzi Adamu. Alimfanya Adamu kuwa mfalme wa Kwanza kabisa. Alimuumba na asili ya utawala na uongozi kitu ambacho akijaondoka kwa mwanaume mpaka leo.

Leo hii kwa kadri muda unavyosogea ndivyo mambo ambavyo yanabadilika. Wanaume wengi wametoka katika nafasi zao nyeti na zinashikwa na wanawake. Nataka nikuonyeshe mambo matatu muhimu ambayo mwanaume anatakiwa arudi upesi katika nafasi yake kama Baba au mwanaume, tutaharibu kila kitu.

1.KIROHO

Kiasili mwanaume anatakiwa kuwa kiongozi wa mambo ya kiroho yanayohusu familia yake. Kwa bahati mbaya sanaa tumewaachia wakina Mama. Tunaona kuwa majukumu yetu ni kutafuta hela familia ipate mahitaji yote ya mwilini. Nataka niseme leo mwanamume anawajibika kwa familia kuipatia mahitaji ya mwilini na Rohoni pia.

Tunapata mfano mzuri kwa Ayubu yeye alikuwa kihani wa familia yake. Alikuwa akiibeba katika mambo ya kiroho na kuitolea sadaka za kutekelezwa. AYUBU 1:5, Yoshua anatoa msimamo wake na familia yake kuwa mimi na Nyumba yangu tutamtumikia Bwana, anaongea kama Baba wa familia kuonyesha msimamo wa imani. Mara nyingi akinamama ndiyo wanaongoza kuhama makanisa na kutoka imani moja hadi nyingine, pengine wanaume wangesimamia nafasi zao wakinamama wasingeyumba, wakiyumba wao wanayumbisha na watoto.

Mwanaume unayo haki kumuuliza Mungu kama Baba na kiongozi wa familia kuhusu Jambo fulani. Isaka alipoona mke waje hapati mtoto alimuuliza Mungu kama Mume na Baba inakuwaje nikose mtoto MWANZO 25:21 leo ndoa inapokosa mtoto lawama uenda moja kwa moja kwa mwanamke, ila kama kiongozi unaweza kufanya kama Isaka muulize Bwana, Mlilie Mungu.

Tunapowaachia akinamama kuisemea familia katika mambo muhimu ya kiroho ni kujiondolea nafasi zetu kama Baba. Baba ndiye anapaswa kuulizwa na kujibu katika Jambo lolote linalohusu familia yake, liwe la rohoni au la mwilini. Siku hizi akina Mama wamechukia nafasi kubwa sana mpaka kwa watoto wao sabu ya wanaume kutekeleza nafasi zao.

Zamani ilikuwa kijana akitaka barikiwa basi anayetoa baraka na laana ni Baba. Pamoja na Rebeka kujua hatma za watoto wake ila ilimlazimu ampeleke Yakobo kwa Isaka Baba yake ili abarikiwe. Yeye asingeweza kutoa baraka wakati Yakobo yupo hai, hata katika jamii zetu kipindi cha nyuma Baba ndiyo anabariki n kulaani. Ila sasa sivyo mtoto hubarikiwa na Mama na Mungu anaeshimu sabu ndiye kachukua nafasi ya kichwa katika baadhi ya Mambo hasa ya kiroho.

Nilikuwa najiuliza sanaa kwa nini makanisani wengi ni wanawake kuliko wanaume? Vita ni kubwa sanaa kwa mwanaume kukaa katika mstari wa kiroho. Adui anajua wanaume wana msimamo, wanamaanisha, ni majasiri, wana nguvu, wana hekima, wanajiweka kiuchumi, basi akiwaacha wajae makanisani hana chake.

Wanaume wakiokoka familia inaokoka, jamii inaokoka, kanisa linakuwa. Ilo ni Jambo la Kwanza sasa la pili.....

2. KIMWILI NA KIAKILI

Mungu alipomuumba mwanaume alimuumba tofauti na mwanamke katika mambo mengi kuanzia maumbile yani misuli na ukakamavu wa mwili, maamuzi, uvumilivu, upambanaji n.k

Wazazi wa kiafrika wametulea vizuri sanaa mfano ukianguka ukalia utasikia "nyamaza bana unalia kama mwanamke!" utagundua kuwa sipaswi kulia kama mwanamke mimi ni mwanaume. Basi ilitujenga kuwa kwa namna yeyote hutakiwi kuwa kama mwanamke. Ndio maana tukiadhibiwa shuleni tulijifunza kugandisha viboko kuwa mwanaume anapaswa kuhendo maumivu. ukilia sanaa watu wana kushangaa.

Kuna wakati katika kucheza watoto wa kiume tunacheza michezo yetu ya kiume ume, ya kikakamavu, na ya hatari zaidi(ingawaje watoto wa sikuhizi wanacheza kwenye magemu) sisi tulicheza analogi kabisa. Na tuliambiana usilete mambo ya kike hapa, inakukumbusha wewe ni nani.

Hivyo basi tukirudi Bustanini Hawa anapokula Tunda hakuna kilichotokea, zaidi ilisubiliwa maamuzi ya mwanaume yataangukia wapi. Yamkini labda mwanamke angeponywa na maamuzi ya mkewe, na Mungu anamuambia Adamu kwa sababu umeisikiliza sauti ya mkeo.... Mwanzo 3:7-18 Ilitarajiwa maamuzi ya mwanaume yaweze kushinda ilesituation lakini yakamezwa.

Ona Mungu anachofanya anaamua kuwalaani wanyama wote ambao Mfalme wao alikuwa ni mwanaume, akaamua kuilaani Dunia kwa maana ya Ardhi ambayo mmiliki wake alipewa mwanaume. Nataka kusema kuna wakati mwanaume anabeba hatma ya vitu na watu wengi, asiposimama vyema anawafelisha.

Mwanaume ni mtu anaye pitia vita kubwa na changamoto nyingi kuliko mwanamke. Kichwa chake kimejaa vitu vingi vizito. Ndiyo maana linapotokea swala gumu nyumbani atasubiliwa Baba arudi ili atoe mwongozo, au yupo mbali sanaa atapigiwa simu. Uwezo wa kutatua changamoto wa mwanaume ni mkubwa kuliko mwanamke, tumeumbwa hivyo na kulelewa hivyo. Ndiyo maana ni nadra sanaa kukuta wanaume wanapigana kisa ugomvi wa watoto, au wamekaa kumsema mtu ni nadra sanaa.

Hivyo basi ukiwa kama mwanaume ukae ukijua shetani anafanya namna yeyote kukufelisha. Katika takwimu Duniani wanaume ni wachache kulinganisha na wanawake, lakini hao hao wachache ndiyo utakuta wanaongoza kwa matukio ya hovyo. Ukienda gerezani utakuta idadi ya wafungwa wanaume ni wengi kuliko wanawake, ukienda baa utakuwa idadi ya walevi wanaume ni wengi kuliko wanawake, ukienda mitaani idadi ya mateja, wezi, wauaji, wanaume ni wengi kuliko wanawake, lakini pia idadi ya mashoga wa kiume ni wengi kuliko wa kike. Na hao waliobaki watahakikishwa wanabanwa kiroho, kiuchumi, kielemu wabaki kwenye ushabiki wa mechi na kuishia kubeti. Na wengi wao kutoka katika nafasi zao katika familia na wengine kukimbia majukumu kama mwanaume. Uwajibikaji kuanzia ndani ya nyumba (kwenye ndoa) mpaka nje (kijamii) usionekane na kuondoka hadhi ya kiume.

Si ajabu kusikia mwanamke akisema humu ndani mimi ndiye Baba. Me nilimsikia mwanamama mmoja akisema mbele ya kanisa kuwa kimaumbile mimi ni mwanamke ila kiakili mimi ni mwanamume. Niliielewa vizuri kauli yake japo wengi waliishia kushangilia kutokana kujiamini kwake.

Nilimsikia Paster Kapola hivi karibuni anasema kuwa kuwa mwanaume ni kazi ngumu ambayo si kila mtu anaweza, ndiyo maana wengi wajibadili jinsia. Kuwa mwanaume ni deni, na kupambana, ni kipimo.

3. KIUCHUMI

Ni bahati mbaya sanaa sikuhizi watu wanachugua kazi, wavivu, jeuri, si waaminifu, na wanajua kila kitu. Ila kuhusu uchumi sihitaji hata kuongea chochote sabu linaeleweka. Tunatakiwa tuwe juu.

Mwl. Vincent Mwakisyala
Whatsapp no 0753114222
 
Imeandikwa wapi kwamba mwanaume hatakiwi kulia kipindi anakumbwa na Hali ngumu?

Mambo Kama hayo ya kutolia ndiyo huwafanya wanaume wengi wafe vifo vya kustaajabisha Kama kujinyonga na kunywa sumu eti kwa sababu waliambiwa wakomae kiume wasilie hovyo hovyo.

Crying is the natural way of responding to pain and each & everyone is entitled to it depending on the degree of the pain he/she feeling in his heart.
Crying relieves one from pain and makes him/ her feel somehow comfortable.Stop misleading others.
 
Back
Top Bottom