Enny
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 962
- 130
Kuna kaka mmoja alipendana na mdada. wakati urafiki umekolea akaanza kuhamia kwa mdada huyu kwa kuleta nguo moja, mbili mara kahamisha nguo zote. Mwisho chumba chake kimechukuliwa. Siku moja alimwambia huyu mdada kuwa anataka awalete watoto wake hapo, lakini bibie alikataa na kumwambia kwanza atafute nyumba yake wahamie kwake badala ya yeye kuishi kwa mwanamke. Lakini sasa , huyu mdada jana ananiambia mwanaume kaamua kuagiza watoto waje tu pale hivyo sasa wapo njiani. sasa ameniomba ushauri afanyeje nae hapendezwi na huyu mkaka kuhamia kwake na familia yake? naomba mchango wenu kwa hili.