Wanatuibia:Tuache kununua sinema za KIBONGO

Tom Hanks,Jolie,Denzel,Damon,etc wanatoa atmost film moja per year,lakin the great na wenzake,mpaka sasa wanatoa movie kila wiki..znapendwa sana na wanawake na housegirls..Crap
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Nikweli ila lawama nyingi tuwatupie madairecta ambao wao wana produce vidio isi kidhi viwango na ubora wa filamu. Naishutu idara inayo husika na mambo haya kuto lichukulia jambo kamahili uzito.
 
alafu % kubwa wamekosa chakuigiza unakuta dume zima limeigiza eti ni shoga haya si ndiyo yale yanayoitwa mambo ya ajabu halafu
lingine hauwezi kukaa nyumbani na kuangalia na familia kwa mf muigizaji akipata gape la denda atang'angania mpaka basi na hawa waigizaji wa kike akikunja 4 unatazama mpaka nywele za ndani yani ni utumbo mtupu pamoja na aibu
 
Sijaona watu waliotoa maoni kuhusu "subtittles" za kiingereza kwa zile filamu ambazo zinaonyeshwa kwenye "channels" za DSTV. Kwa kweli zinachefua sana hasa kama unazitazama na watu ambao si Watanzania. Unatamani ardhi ipasuke upotelee huko. Kiingereza kinachoandikwa huko ni Kiswangilishi kitupu. Sielewi kwa nini hawataki kutumia pesa kidogo kupata watu ambao wanajua kiingereza ili wawaandikie hizo "subtitles". Nawaomba sana sana waache Uswahili kwani wanajiadhirisha wao na nchi yetu Tanzania.

mbombo ngafu
 
Sasa ndiyo ulitaka kusema nini hapa? DVD Original kwa film za Kibongo ziko wapi? Naona na wewe umejichanganya hadi unashindwa kueleweka kabisa. Labda wengine wamekuelewa.......
mimi ninashangaa ... filamu au cinema a.k.a movies originally inatakiwa iwe kwenye large format na irushwe na kuonyeshwa kutoka kwenye projector katika cinema theater na kuonekana na kuonyeshwa publicly..... halafu baada ya muda ndiyo copy zinapelekwa kwenye DVD's na CD'S ... sasa huku kwetu hawa jamaa wanatoa DVD's halafu siyo original wanaita movie

Mie niliangalia JOHARI na nikai-forward vipande vingi tu ili iishe haraka. Mwisho nikaja kuangalia film nyingine na sikuimaliza na nikaitupa kwa hasira baada ya kuona kipande cha jamaa aki-PARK gari kikirudiwa kutoka kona tofauti na mara kibao kama nusu saa nzima...... Mwisho wa siku nilifurahi tu na kucheka sana huku nikishushia Wanzuki moja bariiidi hapa kwangu Sikonge.
 
Yaani mimi sizipendi!bahati mbaya ukiwa kwenye bus la mkoani movie inayoonyeshwa ni hiyo ya kibongo,safari nzima unasikia kichefuchefu!
 
utakuta mwenye muvi yeye cameraman yeye producer yeye stering nashindwa kuelewa hapo kwakweli inatakiwa wajifunze kutoka kwa wenzao
 
utakuta mwenye muvi yeye cameraman yeye producer yeye stering nashindwa kuelewa hapo kwakweli inatakiwa wajifunze kutoka kwa wenzao

No division of labour no profession.
Wabongo tunaigiza kwenye movie industry, hatuko serious hata kidogo
 
majina ya kizungu stori ya kiswahili, hili nalo ni tatizo.

Yani nionapo movie jina la kizungu na waqt najua stori itakuwa ya kiswahili tayari nshaachana nayo. si movie tu, hata stori za yule mdau kwenye magazeti yake heading kuubwa ya kingereza 'The President Loves my Wife...' halafu tafsiri ya kiswahili ndogoooo na hadithi yenyewe ya kiswahili hapo unajua pumba tupu ndani ya hadithi husika. sijui tuna matatizo gani waswahili. kiswahili chetu wenywe, tunakijua tangu utoto. hadithi yetu wenyewe, kingereza cha nini? Dah, kero kero kero
 
Walikosea kupuuza vipindi vya maigizo mashuleni. kuigizwa kulifundishwa shuleni mashuleni, na ndipo haswa panatakiwa kutoa waigizaji wa ukweli. si kuigiza kwa kuwa umekuwa maarufu. hili ni tatizo kubwa sana, kwani ndiko kunapelekea wasanii kushindwa kufaidika na kazi zao. hawako makini kabisa, ni kuuza sura tuu. wamechukua maudhui yote ya afrika magharibi. hakuna ubunifu hata wa jina la filamu/igizo, majina hayana mvuto bali vioja. hovyo kabisa.
 
Hata mimi nashauli hivyo kwani ili hawa jamaa wabadilike basi sisi tusinunue kazi zao kwani bora iwe na part one na two hakuna tatizo, lakini ikiwa copy and paste then edit from english to swahili, then inakuwa ni bora zama za akina mkandala rufufu, kwani utakuta hawa wakina kanumba wanakopy cd nzima kutoka nigeria, just wanabadili wahusika na english to swahili, example worst mariage, imeigwa na akina Ray, monalisa.....
 
tena wanawaza muda wote, mtu anawaza nusu saa nzima.
Tujifunze kutoka Hollywood sio kutoka Nollywood

Teh teh hii nayo imeniacha hoi, kwamba mtu anawaza nusu saa nzima. Mi wananibore wanaongea kwa kupayuka.
 
Nilishaacha muda mrefu kuangalia huu utumbo,, yaani muv ikianza tu ushajua itaishaje, hivi wanashndwa kuwaiga hata Wafilipino? Hawa watu wako siriaz na kaz
 
kuna this day nimeboard bus,, nacheki muv ya kibongo naona kuna this girl anakojoa kwa kitanda 1st season anakojoa tuu hadi to be continued, 2nd season bado akojoa,,,lol
 
Kumbe kuna watu bado mnaziangalia, Binafsi nilishaacha miaka 3 na nusu iliyopita kwa bongo huwa nazicheki comedy tu hizo nyingine ujinga mtupu picha gani ikishaanza unajua itaishaje. Mimi ninaiomba wizara iweze kuwasaidie watu wakuweza kuhariri filamu zao otherwise watakuwa wanaziona wenyewe
 
Zinaniboa, yaani Watanzania wamekosa vitu vya kufanya sasa wanafikiria wizi tu.
Sinema moja kuwa na Part 1 na Part 2 ni wizi, tusikubali kuibiwa, tuache kununua kazi zao hadi hapo watakapo jirekebisha.


BjBj nimewahi toa jibu hili katika thread moja naona na hapa inafaa badala ya kujirudia...


Ni watu wengi saana ambao huponda sana hizi Bongo Movies kwa kuzilinganisha na za nchi nyingine. Personally napenda saana kuangalia movies lakini nimewahi angalia za kibongo kama tano, nakumbuka tu moja jina I think it goes something like 14 days or 14 weeks (mtanisamehe sikumbuki vizuri).

En ways kitu ambacho nilitaka kugusia ni ukweli ulio wazi kua watanzania weengi lugha ya kigeni yani kiingereza kinatusumbua saana. Hivyo basi hio ilipelekea kua Wananchi wachache sana wa Tanzania walikua wakiketi chini na kukaa kama familia kuangalia filamu, hasa hasa wakijitahidi saana ilikua zinachuliwa picha za ngumi ambazo haziihitaji uelewe lugha bali kujua tu sterling kashinda na hajauwawa... (Enzi za Van Damme, Jacky chain, Arnold...)

Bado naona kiwango cha filamu Tanzania ni kidogo but kweli kwa moyo wa dhati kabisa napongeza wale woote Tanzania walio katika filamu industry kwa kazi wanayofanya kwani ni Wananchi wengi sasa wanoweza kuketi na kuangalia filamu akaelewa lugha na akafurahia. Weakness zao katika hizi picha ni kubwa na nyingi to the extent mtu anae angalia movies toka zamani na kuzoea kuangalia za nje ina kua kazai kweli kuvumili sababu kubwa kwamba movies zetu hazina suspense. I wish ifike a time ambayo hata mimi naenda dukani kutaka movie fulani ya Kitanzania huku nikijua nita enjoy....

Big up watu wa film industry, someni historia za Movie entertainment Bollywood na most importantly Hollywood then tuta observe nao walianza kwa kuchechemea....
 
Katika idadi ya sinema zangu hupati ya tz coz of those errors staki kabisa kuziangalia wangeweza kunishawishi kwa ubora wa filam mi ni mteja mzuri tuu wa filamu lakini sina cha kuangalia katika hizo bongo movie!
 
Back
Top Bottom