Wanatuibia:Tuache kununua sinema za KIBONGO

tatizo niliokuwa nalo mimi ni kuwa nyingi hazina uhalisia na mtiririko wake haueleweki, mfano kuna sinema moja nilikuwa naangalia wanaonesha mtu amekamatwa na kupelekwa kituo cha polisi, lkn ukiangalia sio kituo cha polisi ila ni nyumba tu ya kawaida, sasa hapa uhalisia uko wapi ? kwa kweli nyingi hazina mvuto,
 
Sijaona watu waliotoa maoni kuhusu "subtittles" za kiingereza kwa zile filamu ambazo zinaonyeshwa kwenye "channels" za DSTV. Kwa kweli zinachefua sana hasa kama unazitazama na watu ambao si Watanzania. Unatamani ardhi ipasuke upotelee huko. Kiingereza kinachoandikwa huko ni Kiswangilishi kitupu. Sielewi kwa nini hawataki kutumia pesa kidogo kupata watu ambao wanajua kiingereza ili wawaandikie hizo "subtitles". Nawaomba sana sana waache Uswahili kwani wanajiadhirisha wao na nchi yetu Tanzania.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Kuanzia mapozi...story zenyewe...muda wanaotumia kufikiria au kwenda kazini...expression wakiwa wamekasirika au wanashangaa...lugha wanavyochanganya viinglish wakati hawajui...subtitle za kuchapia mi wananichosha!!!Binafsi siwezi kutoa hata mia mbili yangu...labda siku watakapoanza kupokea na kukubali mapungufu yao wakayafanyia kazi!!!
 
tutaendela kujionea vitu vya ovyo ovyo mpaka watu kwenye hii industry watakapo kuwa serious, kwa watengenezaji wa filamu, hii ni taaluma kama zilivyo taaluma nyingine tusiweke ile dhana eti kila mtu anaweza, hapana .... watu wanasomea kuanzia waongoza filamu mpaka waigizaji wenyewe ,tukitaka kufanya vitu kiujanja ujanja matokeo yake ndo haya tunayo yaona
 
Mmegusa penyewe, mimi mwenyewe naona kinyaa kabisa kutizama haya maigizo ya tz a.k.a filamu za kibongo.
Naona kama wameelemea zaidi kwenye mapenzi halafu hata uhusika wanashindwa kabisa kuuvaa, yaani hakuna uhalisia kabisa.

Mie ndio kabisa nimeshindwa kuziangalia
 
kuna mmoja anajiita THE GREATEST bila ya woga wala aibu, ananichefua huyo. hivi ulishawahi kumsikia Brad pitt au Matt Damon anajiita the greatest au sijui ushuzi gani?
 
jamani kwani mnalazimishwa kuzinunua au mnanunua kwa matakwa yenu?

Acheni ujinga huo
 
Nyie pigeni kelele hapo mwenzenu ze great na ze greatest wako busssy kuandaa maigizo mengine kule,muvi zinatoka kila wiki.
 
Sijaona watu waliotoa maoni kuhusu "subtittles" za kiingereza kwa zile filamu ambazo zinaonyeshwa kwenye "channels" za DSTV. Kwa kweli zinachefua sana hasa kama unazitazama na watu ambao si Watanzania. Unatamani ardhi ipasuke upotelee huko. Kiingereza kinachoandikwa huko ni Kiswangilishi kitupu. Sielewi kwa nini hawataki kutumia pesa kidogo kupata watu ambao wanajua kiingereza ili wawaandikie hizo "subtitles". Nawaomba sana sana waache Uswahili kwani wanajiadhirisha wao na nchi yetu Tanzania.
Subtitles ni tatizo kubwa ukiachilia mbali haya maigizo ya kulipua lipua eti mtu anatengeneza picha akiwa mkulima lakini uso amescrub na nywele amekalikiti...hahaaa ..CRAP!!
 
Hivi bado kuna watu wanaangalia filamu za kibongo. Mimi nilijaribu kuwapa sapoti hawa vijana lakini nilishindwa kwa kweli. Kwa zile filamu nilizobahatika kuziona, ni kama vile waigizaji hasa wa kike wangependa kukaa uchi kabisa ila kwa namna moja au nyingine wanashindwa. Maadili ni hakuna yaani taabu tupu.
 
mimi ninashangaa ... filamu au cinema a.k.a movies originally inatakiwa iwe kwenye large format na irushwe na kuonyeshwa kutoka kwenye projector katika cinema theater na kuonekana na kuonyeshwa publicly..... halafu baada ya muda ndiyo copy zinapelekwa kwenye DVD's na CD'S ... sasa huku kwetu hawa jamaa wanatoa DVD's halafu siyo original wanaita movie
 
Back
Top Bottom