MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,232
- 22,312
Leo nimeona nitoa maoni yangu kuhusu hali ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu 2025. Ingawa upinzani (CHADEMA) kunachechemea lakini bado kuna wanasiasa wa upinzani wana nguvu kisiasa na wanaweza kuwa tishio kwenye uchaguzi dhidi ya Chama Tawala CCM. Binafsi naona wafuatao kutoka CHADEMA bado wanakubalika kisiasa hasa majimboni kwao kama watagombea ubunge;
1. Freeman Mbowe
Pamoja na mashambulizi mengi ya kisiasa dhidi yake ila ukweli ni kwamba bado kisiasa Mbowe yuko imara hasa jimboni Hai. Mbowe anakubalika sana na watu wa kwao hasa Machame alipozaliwa. Hii hali imechangiwa pia na misingi aliyoweka baba yake hayati Aikaeli Mbowe. Nakumbuka kwenye msiba wa baba yake Mbowe nilikuwa soda 7 siku ya mazishi. Ule msiba ulikuwa kama sherehe. Mzee alikubalika. Hata Mbowe pia ni mtu wa watu sana. Akigombea ubunge anaweza shinda.
2. Dr Wilbroad Slaa
Huyu ni kipenzi cha wanakaratu. Muda wowote hata saa 8 usiku zikipigwa kura anashinda. Tangu akiwa CCM kabla ya 1995 alikubalika. Hata alipoacha ubunge na kugombea urais bado alikubalika nchi nzima. Kimsingi Dr Slaa akigombea jimbo lolote Tanzania anashinda.
3. Halima Mdee
Huyu mama wa shoka aliibeba BAWACHA mabegani mwake. Bila Halima kungekuwa na BAWACHA mbovu sana. Wanasiasa wachache sana wa jinsia ya kike wanaomzidi kisiasa Halima Mdee. Pale Kawe anashinda saa 2 asubuhi hata akisema ajiondoe CHADEMA na kugombea kupitia CHAUSTA.
4. Esther Bulaya
Huyu swahiba wa Mdee hana wa kufananishwa nae huko Bunda. Anaweza shinda kirahisi. CHADEMA wana jembe hapa.
Hao wanne ni tishio mno kisiasa hadi wakati huu. Kuna wabunge walikuwa vizuri kisiasa ila kwa sasa wamechokwa mno na hakuna namna wananchi wanaweza badili msimamo wa kutowaadhibu kupitia sanduku la kura, hao ni Sugu, Lema, Heche, Mnyika, Msigwa, John Pumbulu na Catherine Ruge.