Wanaopajua dodoma mniambie.

kwa msaada zaidi tuwasiliane nikutembeze maeneo mengi mengi, hasa tutakapokutana nitajua hoby zako so itakua rahisi kujua wapi nikupeleke.

ahsante tufikiri, kuhusu hoby naweza kukwambia kabla.
 
Heshima kwako Husninyo,

Sehemu nnzuri ya kulala nenda Gold Coins ipo area D inatazamana na makao mapya tarajiwa ya Waziri mkuu,
Bei ya chumba tsh 30,000/= plus breakfast.full kiyoyozi joto la Dodoma utakuwa umelipiga chenga.Ni sehemu tulivu hakuna machangudoa labda ukatafute sehemu nyingine.

Unaweza kubadili sehemu ya kula kutegemea na aina ya vyakula unavyopenda.DodomaHotel ni sehemu ambayo unaweza kupata vyakula vya aina mbali mbali kuanzia vyakula vya kihindi,kichina na nk.Kama una usafiri binafsi gari likileta shida nenda Action Garage authorised dealer wa Toyota pia wanatengeneza magari ya aina tofauti na Toyota.

Natumaini nitakuwa nimekusauidia kidogo.

umenisaidia sana si kidogo. Nashukuru.
 
and where the H is Kaizer..................?

Husninyo..................wasiliana na Mkiti wa JF Dodoma wing Kaizer......then tutapanga makaribisho rasmi, bahati mbaya niko safarini Singida

Karibuu makao makuu!

ahsante maskini jeuri. Huyo kaizer nae yupo dodoma au?
 
Wapenzi naombeni kujua maeneo ya kujidai/mtoko katika mkoa wa dodoma. Napenda sehemu tulivu ambazo hazina makelele. Nataka niwe najipa mtoko angalau weekend katika kipindi chote nitakachokuwa huku. Thanx.

Mji una wenyewe bana tumejaa huku baki huko huko ujidai vizuri. teh teh .... . .
 
Wapenzi naombeni kujua maeneo ya kujidai/mtoko katika mkoa wa dodoma. Napenda sehemu tulivu ambazo hazina makelele. Nataka niwe najipa mtoko angalau weekend katika kipindi chote nitakachokuwa huku. Thanx.

dah upo dodoma? wabunge wa chadema wakitoka tena bungeni tunaomba utupatie picha zao laivu.
 
Unaweza ukaenda pia royal village inapatikana area D ni sehemu nzuri, tulivu, upepo mzuri hakuna msongamano nyama nzuri za kuku, mbuzi, ng'ombe zinapatikana ila sina hakika kama "mbuzi mkatoliki" anapatikana pale. But all the same ni sehemu tulivu.
 
Mkuu mbona baada ya maelekezo ya wadau, hujaeleza kama umetembelea maeneo waliokuelekeza na umeyaonaje.

nitakupa feedback ila kuna maeneo niliyoelezwa nasikia yana makelele eg chako chako.
 
Ukipata muda nenda mtera katembelee lile bwawa letu,
Nenda Chilonwa huko utamkumbuka Chonya wa Shida
Pandambili wapajuwa wewe? ni muhimu kupajua pana kahistoria fulani muhimu
Siku nyingine nenda mvumi nyumbani kwa .. huko utajua definition ya maendeleo
Kwa starehe zako za utulivu pitapita maeneo haya:
St. Gaspar
Royal Village Area D
Desert Palm Area D
Kitoli
Savanah- Iringa Road
Twiga hotel
Gold coin
Police jamii
Fujo fujo nazo zina raha yake, hebu pita CnC (chako ni chako), Rose garden area C, Mpepo area C, Ipo ****** baa maeneo ya stend, Four ways Singida road,Club la azizi Makole hapo huwa kuna live band na Club 84. Hizo ni kwa kuanzia tu.


Hahahah , Hiyo inaitwa M@T@KO BAR!
 
Ukitaka kwenda kanisani uende kanisa la Mtakatifu paulo Maeneo ya iringa road!
 
Back
Top Bottom