Wanaofanya kazi ya kupoteza watu ndani ya "Kitengo" wanapataje kazi hii?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,085
144,518
Kwa mwenye kujua, hivi watu wanaofanya hii kazi ya kikatili wanakuwa na sifa gani za kupewa hii kazi ndani ya Kitengo?

Kama ni vibarua, Je, hununuliwa vitu kama bangi waweze kuifanya hiyo kazi pasipo kujali wanachokiofanya?

Au watu wakishapata ajira, baadhi yao hupangiwa hii kazi wapende wasipende?

Na je, hii kazi ina mafunzo maalumu na ambayo yanapatikana nje ya nchi?

Au wanaofanya hii kazi ni watu wenye historia ya uhalifu na ambao ndio hupewa hii ajira?

Yaani unaweza kuwa unatoka nyumbani umetinga kaunda suti halafu kazi yako ikawa ni ya kupoteza watu au kusimamia operration/tukio la mtu kupotezwa na kisha siku ya ibada unaenda kuabudu?

Yataka moyo na ni bora kufanya kazi mochwari kuliko kuwa ndani ya hiki kitengo.
 
Ungejiuliza kwanza wale wanaopiga Wanyama kama Paka au Mbwa mpaka anakata roho hupewa mafunzo gani? Kwa nini Tanzania wanapiga paka mpaka anakata roho?

Wanambana mahali na kumpiga mpaka anakata roho unafikiri ni kwa nini? Au kwa nini Tanzania Mwanaume akimuua Mke wake kwa ukatili Wanaume (siyo wote) wa Tanzania wanamtetea Mwanaume kwa ukatili aliomfanyia Mwanamke na hawaonyeshi huruma na Mwanamke aliyeuliwa kikatili?

Ukipata majibu ya hayo maswali ndiyo utaelewa kwamba unaweza kuuwa mtu kirahisi sana klk unavyodhania, unahitaji kumchukia tu, kila kitu kimeisha.

Hao watu ni psychopath sifa ya psychopathy ni kukosa huruma na wataalamu wanasema wanaotesa Wanyama ni psychopaths na siyo watekelezaji tu kuna wanaotoa oda pia unawaweka kundi gani?
 
Ungejiuliza kwanza wale wanaopiga Wanyama kama Paka au Mbwa mpaka anakata roho hupewa mafunzo gani?

Hao watu ni psychopath sifa ya psychopath ni kukosa huruma na wataalamu wanasema wanaotesa Wanyama ni psychopath, na siyo watejelezaji tu kuna wanaotoa oda pi unawaweka kundi gani?
Kuna kitu nakigiundua hapa, ila stasema kwa sasa.
 
Hizo kazi huwa wanapewa watu wasio na akili. Watu wanaoweza kuendeshwa kama Robot.

Mtazame Bashite. Kila aliposoma aliondoka na daraja sifuri. Halafu akafanywa kuwa mkuu wa kitengo cha kupoteza watu.
 
Criminology trait
1.Narcist ni wale Mbwa wanaojijali wao na wako aggressive ukiwapinga kwa chochote.

2.Marchiaveli hawa maadili sifuri na hawana Hisia kabisaa....Faida mbele utu hakuna.

3.Psycopath Hawa hawana huruma Wala uelewa wako Kama mafta ya taa wanalipuka TU wakiona target Yao.

Kiujumla Ni wajomba ambao ndani yao Kuna huzuni ili wawe na Raha lazima watafute wa kumpa huzuni au kumuumiza.
Wachunguze wakishatenda uovu utaona Wana Furaha flani hivi.
#Unaweza ukaeditiwa TU ikawa ndio stable position yako mupya.
 
Hawa watu huitwa "hitmen". Hutumiwa na magenge ya waharifu, serikali (government conspiracies) ama walipa visasi (vendetta).

Nije kwenye hoja yako ya mafunzo. Hitmen wa serikali hupewa mafunzo ya kupoteza watu.

Hitmen wa Tanzania (enzi za ujamaa) walikuwa wanapelekwa Moscow ambako kuna chuo ambacho hutoa mafunzo ya kuuwa kwa kutumia sumu, bunduki na kumnyonga mtu kwa mikono.
 
Kwahiyo BTP yao ni watu gani?
Hawa watu huitwa "hitmen". Hutumiwa na magenge ya waharifu, serikali (government conspiracies) ama walipa visasi (vendetta).

Nije kwenye hoja yako ya mafunzo. Hitmen wa serikali hupewa mafunzo ya kupoteza watu.

Hitmen wa Tanzania (enzi za ujamaa) walikuwa wanapelekwa Moscow ambako kuna chuo ambacho hutoa mafunzo ya kuuwa kwa kutumia sumu, bunduki na kumnyonga mtu kwa mikono.
 
Back
Top Bottom