Kiboko ya Jiwe
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 12,702
- 36,143
Nchi ya Tanzania watu wanachapa kazi sana na watu wavivu au wenyewe wanajiita wasio na kazi wako pia.
Turudi kwenye mada.
Serikali inawaza nini juu ya kazi ambazo hazina tija kwa taifa, hazichangii pato la taifa?
Kazi ambazo zinampa ugali mfanyaji na familia yake basi.
Taifa litasonga vipi mbele ikiwa wananchi wako busy kufanya kazi zisizo na mchango kwenye pato la taifa?
• Kazi ya udalali
Hapa nchini haina mchango kwenye kukuza pato la taifa. Madalali hawalipi Kodi. Hakuna wanachozalisha.
Ni muda sasa madalali wasajiliwe na kulipishwa kodi. Ni aibu nchi kubwa kama hii kusaidiwa na kinchi kidogo kama Uswizi. Dawa ni kupanua wigo wa mlipa Kodi.
• Kazi za umachinga
Licha ya kazi hii kuwa ndiye mwajiri mkubwa hapa nchini lakini haina faida kwa Taifa. Machinga wengi au wote hawalipi Kodi licha ya kuwa wapo machinga mauzo yao kwa siku moja kufikia mpaka milioni 5. Pili machinga wengi huuza bidhaa za kichina hivyo machinga ni watumishi wa nchi ya uchina wanaofanya kazi nje ya China. Wanakuza uchumi wa nchi za watu .
• Kazi ya bodaboda
Serikali imeshindwa hata kugawa leseni za kuendeshea bodaboda angalau kwa sh. 50000. Kazi ya bodaboda haina manufaa kabisa kwa hii serikali. Bodaboda ni kama kitengo cha ukusanyaji mapato binafsi ya polisi na mgambo. Wapo watu watasema bodaboda ananunua mafuta serikali inapata kodi, lakini wanashindwa kufikiri zaidi ya hapo. Kwanza bodaboda zinajenga uchumi wa India na China maana wao ndio wanaozizalisha na kuzi export maelfu kwa maelfu kila siku kuja kuvunja migongo ya vijana wa Dunia ya 3.