Wananchi wavamia ofisi za CCM, wavunja uzio

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Vurugu kubwa zimeubuka eneo la Mbagala Kiburugwa, jijini Dar es Salaam, baada ya wananchi wenye hasira kuvamia jengo la ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kubomoa ukuta wa uzio.
Vurugu hizo zimeibuka kufuatia kuwepo kwa mvutano kati ya wananchi na CCM kuhusu nani mmiliki na msimamizi halali wa kisima cha maji.
Tukio hilo lilitokea juzi saa 11: 30 na kushuhudiwa na Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile, ambaye alikwenda hapo kwa ajili ya kukirudisha kisima mikononi mwa wananchi baada kikundi cha wanaCCM kukimiliki kwa miaka saba.
Katika vurugu hizo, umati wa wananchi walivamia jengo hilo la CCM na kuanza kubomoa uzio uliojengwa kwa mabati kuzuia watu kuchota maji kwenye kisima hicho, huku wakimshangilia Dk. Ndugulile kutokana na uongozi wake usiojali itikadi ya vyama.
Mvutano huo uliibuka baada ya wananchi hao kuunda kamati ya maji ya muda na kuiondoa kamati ya zamani kwa madai ya ubadhirifu, lakini uongozi wa CCM ulipinga hatua hiyo na kudai kisima hicho kilichopo ndani ya eneo lao hawatakubali kuona wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) wakienda eneo hilo kwa mgongo wa kisima.
Dalili za kutokea vurugu zilianza wakati Mbunge huyo akiwahutubia wananchi wa eneo hilo mita 500 kutoka ofisi hiyo ya CCM, ambapo wengi wa wananchi waliojitokeza kutoa kero zao walisema mgogoro wa kisima hicho uliopo kati ya vyama viwili vya CCM na CUF, umewafanya kukosa maji kwa kipindi kirefu.
Akiwa mkazi wa kwanza kutoa kero yake, Abdallah Kiumbaumba, alimwambia mbunge huyo kuna umuhimu wa kwenda eneo la kisima hicho kutatua mgogoro huo kutokana na wananchi kuchoshwa na hatua ya baadhi ya viongozi wa CCM kung'ang'ania kuhodhi mradi wa kisima kinyume na utaratibu.
"Tunajua mradi wa kisima ni mali ya wananchi wote, lakini CCM imekihodhi na kufanya mali yake, ninavyokueleza kuna hali mbaya wananchi wamechoshwa na kuna hatari damu itamwagika," alisema Kiumbaumba na kushangiliwa na umati wa watu.
Kutokana na malalamiko hayo, Mbunge huyo aliamua kwenda eneo hilo kuangalia hali halisi, lakini alipofika, kundi la wananchi walivamia uzio uliojengwa kuzunguka ofisi hizo na kuanza kubomoa huku baadhi yao wakibeba mabati na mbao na kukimbia nazo.
Kitendo cha wananchi kunyimwa huduma hiyo ya maji kilionekana kumkera Dk. Ndugulile na kuamuru mambomba yaliyopo kisimani hapo yaondolewe kufuli zilizofungwa ili wananchi wachote maji.
Akizungumza mbele ya wananchi hao, Dk. Ndugulile alisema licha ya yeye kuwa mwanachama wa CCM, lakini ameumizwa na tukio hilo la wananchi kunyimwa huduma ya maji na kuanzia jana aliagiza wananchi wapo huru kuchota maji eneo hilo huku akilitaka Jeshi la Polisi kuweka ulinzi ili kuzuia vurugu kutokea.
"Mimi kama Mbunge wa Kigamboni, siwezi kukubaliana na jambo hili na nasema kama mbunge wa wananchi wote, mabomba yote yaliyofungwa yafunguliwe ili wananchi wapate maji huku utaratibu mwingine tukiendelea kuufanya kuondoa utata wa jambo hili," alisema Dk. Ndugulile na kushangiliwa na wananchi hao.
Hata hivyo, jana kiliitishwa kikao maalum cha kuzungumzia sakata hilo kwa kushirikisha uongozi wa Manispaa ya Temeke, wananchi na uongozi wa CCM kutafuta njia ya kuutatua mgogoro huo unaonekana kuleta vurugu kwa wakazi wa eneo hilo.
CHANZO: NIPASHE
 
Ccm wanashindwa kusorve vitu vidogo sana kisima nacho tatizo. Pesa za mabango makubwa wakati wauchaguzi walikuwa nazo nyambafuuuu zao.
 
Ipo siku wananchi watachoka na watamvamia JK akiwa ikulu au Lumbumba au Bagamoyo!
 
Back
Top Bottom