Mpanda: Wananchi waondokana na adhaa ya maji ya visima

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Wananchi wa Mtaa wa Tulieni iliyoko Kata ya Nsemulwa, Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamesogezewa huduma ya maji safi mara baada ya mradi wa kutanua mtandao wa maji safi kukamilika katika mtaa huo.

Hadija Kunja na Saidi Ramadhani ni wananchi wa mtaa huo wamesema kwa muda mrefu Wananchi wa Mtaa wa Tulieni walikuwa wanatumia maji ya visima ambayo yalikuwa yawapa wasiwasi ya kiafya ambapo kwa sasa wameondokana na adhaa hiyo mara baada ya mamlaka ya maji safi Mpanda kukamilisha mradi wa kutanua mtandao wa maji kwa wananchi.

Rehema Nelson ni Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Maji Safi Manispaa ya Mpanda amesema kuongeza mtandao wa maji kwa Wananchi ni kutekeleza usogezwaji wa huduma ya maji safi kwa wananchi ili kuwaondolea changamoto ya kufuata maji mbali lakini pia kutumia maji ya kisima.
 
Walete na huku milala bwawa mpanda girls lipo karibu Ila maji kufika huku imekuwa changamoto
 
Back
Top Bottom