Wananchi wanaoishi katika mazingira magumu kupatiwa Bima ya Afya iliyoboreshwa CHIF Kyela

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Zaidi ya Wananchi 100 Wilayani Kyela Mkoani Mbeya, wanaoishi katika mazingira magumu wanatarajiwa kupatiwa Bima ya Afya iliyoboreshwa CHIF na Umoja wa Wanakyela waishio ndani na nje ya Nchi katika Kyela Ibasa Festival itakayofanyika Desemba 27, 2023 Wilayani humo.

Huo utakuwa ni msimu wa tano wa kufanyika kwa Tamasha la Ibasa Festival likiwaunganisha Wazawa wa Wilaya ya Kyela waishio ndani na nje ya nchi wakitoa michango yao ya hali na mali kwa ajili ya kuisaidia jamii ya Kyela kila unapofika mwisho mwa mwaka.

0d11e99f-11ce-4c00-89ad-3cffc1e96b49.jpeg

Akizungumzia maandalizi ya Tamasha hilo, Katibu wa Ibasa Festival, Nicholaus Mwangomo, amesema maandalizi yamekamilika kwa Asilimia 100 na kwamba wamejipanga kuisaidia jamii yao katika nyanja ya Afya, Elimu, utalii na utamaduni.

“Ibasa litaanza Desemba 27 hadi tarehe mosi 2024 Wilayani Kyela likiwa na matukio mbalimbali ya kijamii kama vile utoaji wa Kadi za Bima ya Afya, usafi katika Kituo cha Afya, mpira wa miguu na wa pete, ngoma za asili na burudani nyingine ambazo zinawakutanisha pamoja wanakyela,” amesema Mwangomo.

f5569c9a-e1a4-4285-bcf7-67991dc56aef.jpeg

Mtunza Hazina wa Ibasa Festival, Lufingo Mwakilasa, amesema katika michango waliyoitoa wanachama asilimia 40 itaenda kwa jamii ili kusaidia uboreshaji wa huduma za afya na elimu.

Naye Mratibu wa Tamasha hilo, Pablo Kais, amesema furaha yao ni kuwa sehemu ya kuisaidia jamii na kwamba wataendelea kufanya hivyo kama sehemu ya kurudisha fadhila.

Kyela Ibasa Festival liliasisiwa mwaka 2019 likiwa na maono ya kuisaidia jamii ya Kyela katika nyanja ya elimu, afya, uchumi na utamaduni.
 
Back
Top Bottom