Watanzania wanaoishi Nje ya Nchi watoa msaada wa vitabu 100 kwa Wanafunzi Kyela

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Zaidi ya Vitabu 100 vya masomo mbalimbali vimetolewa na Umoja wa Wazawa wa Kyela Mkoani Mbeya waishio ndani na Nje na Nchi, Kyela Ibasa Festival kwa ajili ya kuwawezesha Wanafunzi kuanzia Kidato cha kwanza hadi cha nne kusoma kwa utulivu na kumaliza mada zote kwa wakati ili kujiandaa na mitihani.

Mwenyekiti wa Kamati Jamii katika kundi hilo, Vanessa Nyesyenge amekabidhi kwa Diwani wa Kata ya Ikimba, Omary Rashid Mwinyijuma.
ede7a36d-a90e-4127-84d2-92827f693a62.jpeg

0eae8cba-eef9-4833-9536-167a5010621b.jpeg
Vanessa amesema vitabu hivyo vitakabidhiwa kwenye Shule ya Sekondari Njisi kwa ajili ya kuwasaidia Wanafunzi kumaliza mada kwa wakati ili kupata muda wa kujisomea.

“Miongoni mwa maono ya Ibasa ni kuisaidia Jamii ya Kyela katika nyanja ya elimu wakati tunaadhimisha miaka mitano tangu kuanzishwa kwa Ibasa tumetoa misaada ya madawati na sasa vitabu ambavyo tunaamini vitaongeza chachu ya wanafunzi kusoma kwa bidii maana vitabu vipo,” amesema Vanessa.

Ameongeza kuwa vitabu 150 vya masomo ya Hisabati, Kingereza, Fizikia, Kemia, Kiswahili, Bailojia, Jiografia na Uraia.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya Serikali, Diwani wa Kata ya Njisi, Omary Mwinyijuma amesema vitabu hivyo vitasaidia kuongeza ufaulu kwa Wanafunzi hao kwa sababu watajifunza vizuri kwa nadharia kwa sababu tayari watakuwa na muongozo.

Amewataka Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Njisi kuvitumia vitabu hivyo kuongeza maarifa ili waweze kufanya vizuri kwenye mitihani yao.

Akizungumza kwa niaba Wanachama wa Kyela Ibasa, Sady Mwang’onda amesema umekuwa ni utaratibu kila unapifika mwisho wa mwaka wazawa wote wa Kyela wanahamasishana kurudi nyumbani kuisaidia jamii yao kwenye nyanja ya afya, elimu, kuenzi utamaduni na kutembelea vivutio vya utalii.

Naye Sara Mwangasa, amesema wataendelea kutoa misaada ya hali na mali kwa jamii yao na kwamba wanatamani kuona wilaya ya Kyela inapiga hatua ya Maendeleo.

Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo, Farida Mwakalyelye amesema katika kuisaidia jamii Mwaka 2024 wametoa Sh Milioni 4.9 kusaidia masuala mbalimbali.
 
Siku nyingine waambie watoe msaada wa hela. Watu wanataka maokoto ndio mpango mzima
 
Back
Top Bottom