Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,382
- 33,237
Mimi Ninahisi yata tokea kama yailyo tokea kwa aliyekuwa Mpendwa wa Watu na Mtetezi wa Wanyonge RIP Magufuli tungojee hiyo sinema ya kutisha mwisho wake itakwishaje? Hii ni Sirikali siyo Serikali.Tulimpoteza Magufuli kwa sababu kuumwa hadi kuzidiwa kulifanywa National Bigly Secret ambapo wananchi hatukujulishwa iwapo anaumwa ama amezidiwa zaidi ya kustuliwa na taarifa ya kifo chake mnamo 17 March 2021.
Rais ni wa Jamhuri ijulikane kuwa anamilikiwa na wananchi wote bila kujali itikadi, imani wala kabila. Nasema anamilikiwa ni kwa sababu shughuli zake zote zinamhusu kila raia awe mdogo au mkubwa kwa jinsia zote.
Rais anamilikiwa na wananchi ndo maana analindwa na wananchi na kutunzwa na kodi za wananchi. Ingawa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wanadhani wao pekee ndo wenye dhamana ya kumtunza na kumlinda Rais. Wananchi watasali kwa miungu yao, watatambika kwa mahoka wao na kadhalika ilimradi Rais aweze kufikia matarajio na matamanio yao. Wenye Mungu nao watamuombea ili awe salama na aweze kutekeleza majukumu yake vyema.
Inaelekea tukio la marehemu JPM halijatupa funzo lolote. Zimeanza tetesi kupitia wale wale walioeneza uvumi kuhusu hatma ya JPM na sasa wanamtaja Makamu wa Rais. Tetesi hizi zimeendelea kupata mwangwi mkubwa kupitia mitandao ya kijamii kuhusu afya na uhai wa Makamu wa Rais.
Serikali, imeendelea kupuuza uvumi huo kama ilivyopuuza uvumi (uliokuwa siyo uvumi) enzi Mwendazake wakati anapigania uhai wake vyumba vya afya. Tuliona viongozi wakubwa akiwemo Waziri Mkuu wakitoa matamko ya kubeza tetesi hizo kwa kuuaminisha Umma kwamba Rais wao anachapakazi yupo gado kabisa.
Jana, serikali ilisambaza bango mitandaoni kumuonesha Makamu wa Rais atakuwa mgeni rasmi kwenye Mkutano wa TAWIRI unaoanza tarehe 06 Desemba 2023..... sisi tunaochoshwa na tetesi za vifo vya wakubwa tukanyenya mikono juu kumshukuru Mungu kuwa tetesi kuhusu hali ya Mhe. Mpango ni uzushi na upotofu. Lakini aliyefika mkutanoni ni mwakilishi (Mhe. Kairuki) na siyo mgeni mlengwa.
Tumepatwa na msiba wa kitaifa kule Hanang kwa kuondokewa na ndugu zetu kutokana na mafuriko makubwa. Tumeona mfariji wa Taifa ambaye ni Rais ameshajitokeza na kusimama na wananchi wote na hata Waziri Mkuu na viongozi wengine wa Serikali wanafanya kila linalowezekana ili kuwanasua waliokwama chini ya tope zito la mlima Hanang. Lakini hatujamsikia popote Makamu wetu wa Rais akitoa pole kama ilivyo kawaida yake kwa matukio aina hii.
Kwa niaba ya Watanzania, naleta ombi kwa serikali ituondoe kizani kuhusu alipo makamu wa Rais. Hizi tetesi zinazoendelea hazina afya kwa Taifa.
Endapo kweli hatunaye na hatukutangaziwa kuumwa kwake ni wazi hatutazuiwa kuwaza kwamba serikalini kuna hila nyingi dhidi ya viongozi wa Kitaifa na hakika tutaamini kwamba vyombo vyetu vya ulinzi na usalama pamoja na mamlaka zingine zina muunganiko usio na afya kwa Taifa letu.
Naomba tujulishwe