Wanafunzi wawili wafariki kwa kukosa hewa wakitoa maharage kwenye pipa

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,116
Wanafunzi wawili wa Shule ya Sekondari Kisomachi, iliyopo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wamefariki dunia baada ya kudaiwa kukosa hewa, wakati walipoingia kwenye tenki la kuhifadhia maharage.

Akizungumza Mwenyekiti wa Kijiji cha Kileuwo wilayani hapa, Godfrey Mrema amesema tukio hilo limetokea Mei 12, 2023, wakati wanafunzi hao walipoingia kwenye tenki hilo kwa ajili ya kutoa maharage ya chakula shuleni.

“Wanafunzi hao wote wana umri wa miaka 17, na uongozi wa shule umesema wote walifariki baada ya kuingia kwenye tenki kwa ajili ya kutoa maharage ya kupeleka stoo kwa ajili ya kupika,” amesema.

Ameongeza kuwa “Kwa taarifa tuliyoipata shuleni ni kwamba wanafunzi hao walipanda kwenye pipa hilo kwa kutumia ngazi na kisha kutumbukia ndani kutoa maharage na alianza kuingia mmoja, halafu akaanza kupiga kelele ndipo mwenzake akaingia kwa ajili ya kumuokoa lakini walikosa hewa na hadi kugeuza pipa kutolewa walishafariki,” amesema.

“Hapa inaonekana kuna uzembe, maana kama shule ina mpishi, kwa nini wanafunzi waingie kwenye pipa kwa ajili ya kutoa maharage kupeleka stoo? Alihoji mwenyekiti huyo na kueleza kuwa, tayari vyombo vya usalama pamoja na Mkuu wa Wilaya walifikaa eneo la tukio

Alipotafutwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kisare Makori kuzungumzia tukio hilo, amesema atalizungumzia baadaye.

Chanzo: Mwanachi
 
Hilo tank lilitengenezwaje? Mbn Kuna matank siku hizi ukitaka kutoa nafaka Kuna kitu unafungua Kwa chini tu. Yani huzuni sana.

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
 
Picha ya pipa ni muhimu kuiona vinginevyo wote Kila mmoja atajenga kivuli Cha pipa ka la kuwekea maji - simtank/kiboko/et
 
Back
Top Bottom