Wanafunzi wa St. Joseph wafungua kesi ya kudai Sh6 bilioni kutoka kwa TCU

Dennis002

Senior Member
Aug 18, 2014
149
52
Wanafunzi 316 waliokuwa wakisoma katika Chuo Kikuu cha St. Joseph ambao walirudishwa nyumbani kwa kuwa hawana sifa, wamefungua kesi ya madai ya Sh 6 bilioni katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam dhidi ya Chuo hicho na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).

Katika kesi hiyo iliyopangwa kuanza kusikilizwa Septemba 13,2016 mbele ya Jaji Winfrida Koroso, wanafunzi wanne Ramadhan Kipenya, Inocent Peter , Faith Kyando na Mohammed Mtunguja waliruhusiwa kuwawakilisha wenzao mahakamani hapo.

Wanafunzi hao ambao wanatetewa na Wakili, Emmanuel Muga wanaiomba mahakama hiyo iamuru walipwe zaidi ya Sh 1 bilioni kama gharama ikiwamo za ada walizokilipa chuo hicho. Pia wanaomba kulipwa Sh 5 bilioni kama fidia ya jumla ya gharama za hasara walizozipata.

Kwa upande wa Wakili Muga ambaye anawawakilisha wanafunzi hao aliiomba mahakama kuendesha kesi hiyo kwa haraka kwa sababu wanafunzi hao wapo mtaani na hawajui hatma yao na fedha zao zimeliwa.

Chuo Kikuu cha St. Joseph katika kesi hiyo kinawakilishwa na Wakili Jerome Msemwa huku Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ikiwakilishwa na Wakili Rose Rutta.

Katika kesi hiyo, wanafunzi hao kupitia wakili wao Muga wanadai kuwa TCU iliruhusu Chuo Kikuu cha St. Joseph kudahili wanafunzi wa Digrii ya miaka mitano wa ualimu wa Sayansi. Miaka miwili kwa ajili ya kuwaweka wanafunzi hao vizuri kwa sababu ni wa kidato cha nne lakini baaday e Mei 2016, TCU ikasema hawana sifa warudi nyumbani wakati baadhi yao walikwisha kaa chuoni hapo kwa kipindi cha mwaka mmoja, miwili na wengine mitatu na wamekwisha kilipa gharama nyingi.

Wanafunzi 316 waliokuwa wakisoma katika Chuo Kikuu cha St Joseph waliorudishwa nyumbani kwa kukosa sifa,wamefungua kesi ya madai ya Sh6 bilioni kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam dhidi ya chuo hicho na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU).

Katika kesi hiyo iliyopangwa kuanza kusikilizwa Septemba 13 na Jaji Winfrida Koroso, wanafunzi wanne Ramadhan Kipenya, Innocent Peter, Faith Kyando na Mohammed Mtunguja waliruhusiwa kuwawakilisha wenzao mahakamani hapo.Wanafunzi hao ambao wanatetewa na Wakili,Emmanuel Muga wanaiomba mahakama iamuru walipwe zaidi ya Sh1 bilioni kama gharama ikiwamo za ada walizokilipa chuo hicho.

Pia, wanaomba kulipwa Sh5 bilioni kama fidia ya jumla ya gharama za hasara walizozipata. Wakili Muga ambaye anawawakilisha wanafunzi hao aliiomba Mahakama kuendesha kesi hiyo kwa haraka, kwa sababu wanafunzi hao wapo mtaani na hawajui hatima yao huku fedha zao zikiwa zimeliwa. Chuo Kikuu cha St. Joseph katika kesi hiyo kinawakilishwa na Wakili Jerome Msemwa, huku TCU ikiwakilishwa na Wakili Rose Rutta.

Chanzo: Mwananchi
 
Huenda kutoka na kesi hii tukapata majibu ambayo Tulikuwa tukiyahitaji,mathalani kwenye utaratibu wa kudahili watu wasio na vigezo.
 
Wanafunzi 316 waliokuwa wakisoma katika Chuo Kikuu cha St Joseph waliorudishwa nyumbani kwa kukosa sifa,wamefungua kesi ya madai ya Sh6 bilioni kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam dhidi ya chuo hicho na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU).

Katika kesi hiyo iliyopangwa kuanza kusikilizwa Septemba 13 na Jaji Winfrida Koroso, wanafunzi wanne Ramadhan Kipenya, Innocent Peter, Faith Kyando na Mohammed Mtunguja waliruhusiwa kuwawakilisha wenzao mahakamani hapo.Wanafunzi hao ambao wanatetewa na Wakili,Emmanuel Muga wanaiomba mahakama iamuru walipwe zaidi ya Sh1 bilioni kama gharama ikiwamo za ada walizokilipa chuo hicho.

Pia, wanaomba kulipwa Sh5 bilioni kama fidia ya jumla ya gharama za hasara walizozipata. Wakili Muga ambaye anawawakilisha wanafunzi hao aliiomba Mahakama kuendesha kesi hiyo kwa haraka, kwa sababu wanafunzi hao wapo mtaani na hawajui hatima yao huku fedha zao zikiwa zimeliwa. Chuo Kikuu cha St. Joseph katika kesi hiyo kinawakilishwa na Wakili Jerome Msemwa, huku TCU ikiwakilishwa na Wakili Rose Rutta.

Chanzo: Mwananchi
 
Hawa nao wamekosea, wangefanya usajili wa kibatala na Tundulissu. Hakika kesi wangekuwa na 90% ya kushinda.
 
Wanafunzi 316 waliokuwa wakisoma katika Chuo Kikuu cha St. Joseph ambao walirudishwa nyumbani kwa kuwa hawana sifa, wamefungua kesi ya madai ya Sh 6 bilioni katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam dhidi ya Chuo hicho na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
Katika kesi hiyo iliyopangwa kuanza kusikilizwa Septemba 13,2016 mbele ya Jaji Winfrida Koroso, wanafunzi wanne Ramadhan Kipenya, Inocent Peter , Faith Kyando na Mohammed Mtunguja waliruhusiwa kuwawakilisha wenzao mahakamani hapo.
Wanafunzi hao ambao wanatetewa na Wakili, Emmanuel Muga wanaiomba mahakama hiyo iamuru walipwe zaidi ya Sh 1 bilioni kama gharama ikiwamo za ada walizokilipa chuo hicho.
Pia wanaomba kulipwa Sh 5 bilioni kama fidia ya jumla ya gharama za hasara walizozipata.
Kwa upande wa Wakili Muga ambaye anawawakilisha wanafunzi hao aliiomba mahakama kuendesha kesi hiyo kwa haraka kwa sababu wanafunzi hao wapo mtaani na hawajui hatma yao na fedha zao zimeliwa.
Chuo Kikuu cha St. Joseph katika kesi hiyo kinawakilishwa na Wakili Jerome Msemwa huku Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ikiwakilishwa na Wakili Rose Rutta.
Katika kesi hiyo, wanafunzi hao kupitia wakili wao Muga wanadai kuwa TCU iliruhusu Chuo Kikuu cha St. Joseph kudahili wanafunzi wa Digrii ya miaka mitano wa ualimu wa Sayansi.
Miaka miwili kwa ajili ya kuwaweka wanafunzi hao vizuri kwa sababu ni wa kidato cha nne lakini baaday e Mei 2016, TCU ikasema hawana sifa warudi nyumbani wakati baadhi yao walikwisha kaa chuoni hapo kwa kipindi cha mwaka mmoja, miwili na wengine mitatu na wamekwisha kilipa gharama nyingi.
mwisho
Share
Rose Rutta, Judge
 
Hapa utendaji wa serikali (wizara, TCU) na chuo husika (St. Joseph) utakuwa chini ya darubini ya mahakama. Kama program ilikuwa authorised na vijana walidahiliwa baada ya kukidhi vigezo vilivyo kubaliwa na serikali basi serikali itabidi iwajibike. Ni wanafunzi ambao walichaguliwa kinyume na vigezo vilivyowekwa ambao serikali inahaki ya kukataa kuwajibishwa lakini vyuo na wale walio wapa idahili watatakiwa kubeba mzigo wao. Kama kulikuwa na hongo wahusika nao wawajibishwe.
 
Serikali nayo hakuna kitu bora ihukumiwe kikamilifu,,,ila hio idadi ya waliorudishwa nyumbani haiko sahihi
 
Back
Top Bottom