Wanafunzi kugoma kuingia madarasan kisa kupinga kupewa adhabu ni sahihi?

CPA

JF-Expert Member
Mar 1, 2011
809
354
Wanafunzi wa nane nane secondary school morogoro wamegoma kuingia darasan, kisa kupinga kupewa adhabu, kama viboko na nyinginezo. Je hii sahihi, wanataka waishi kama wafalme huku wakiendelea kupata zero. Naona wanafunzi wa kipindi hiki wanakosa nidhamu, wenyewe na simu mkononi na face book.
Source. ITV
 
kwahiyo fimbo ndo mwisho wa zero???fikiria kabla ya kuandika. Fimbo ni utumwa!! Wahindi wanazidi kuchanja mbuga tu,lakini fimbo hawawahi hata kuziona,toka kindegate hadi chuo!! Mi sekondari fimbo ilikuwa mwiko!!hamna kabisa, ukipata kosa basi we ni kulima au kwenda msituni kukata kuni...na nimetoka na div 1 single digit
 
wewe ndio uwe unafikiria kabla ya kuandika, kwani kulima au huko kukata kuni sio adhabu. Ninawasiwasi na hiyo div one yako, itakuwa ni div 4 ya mwisho
 
wewe ndio uwe unafikiria kabla ya kuandika, kwani kulima au huko kukata kuni sio adhabu. Ninawasiwasi na hiyo div one yako, itakuwa ni div 4 ya mwisho

Mkuu kiujumla adhabu za mashuleni mi sikubaliani nazo!! coz si njia mbadala wa kumfanya mtoto awe na akili.
 
Adhabu zipo kila pahali, hata mbinguni! Everyone has take the responsibily for his/her actions.
 
Kwa jinsi nilivyowasikiliza watoto hawa walikuwa na madai mengi ambayo ni pamoja na kutokufundishwa halafu wanaadhibiwa kwa kufail mitihani. Ki msingi walikuwa wanaona shuleni kwao kuna matatizo ambayo yalihitaji utatuzi wake kuhusisha pande mbalimbali ikiwa ni pamoja na wao wenyewe wanafunzi,waalimu wao,wazazi na hata serikali yenyewe lakini waalimu wao walichukua njia rahisi ya kuwaadhibu wakitegemea ndio kikombe cha hayo matatizo.
 
Wana haki ya kufanya demo! Walikuwa na madai ya msingi mfano uwepo wa school baraza n.k
 
kwahiyo fimbo ndo mwisho wa zero???fikiria kabla ya kuandika. Fimbo ni utumwa!! Wahindi wanazidi kuchanja mbuga tu,lakini fimbo hawawahi hata kuziona,toka kindegate hadi chuo!! Mi sekondari fimbo ilikuwa mwiko!!hamna kabisa, ukipata kosa basi we ni kulima au kwenda msituni kukata kuni...na nimetoka na div 1 single digit

.... na mimi enzi zangu nasoma nilikua nakua wa kwanza tu.. nikishika nafasi ya pili sili mwezi mzima....
 
Mchelea mwana kulia,....mie nimesoma primary tulikuwa tunagongwa sijaona,tena kama tunasema watoto wa leo wanachapwa,siyo kweli,ina maana mmesahau kushika kucha,mmesahau kupigwa mzunguko na staff nzima?mmesahau au hamjawahi hata kusimuliwa?sasa sema umeona wapi leo watoto wanashika kucha?

Navyojua mie ni kwamba walimu wanasoma psycology humo wanasoma module ya punishment,nadhani wanazielewa zaidi yetu,tusiondoe punishment kwa kisingizio cha kuwepo kwa minor indiscplnary cases,hzi cases zishughurikiwe lakini adhabu ziendelee kuwepo,kasome behavioural psycologists (Puvlov,Bruner,Ausbel n.k)

nachokiona hapa wanasheria wanaingilia fani kwa kumanipulate,hvi nyinyi wanasheria mnaelewa nini kuhusu child dvlopment?behaviours?mnaelewa nini juu ya Montessori in education pedagogy?mnaelewa ama tuwasaidie kuwajuza?be free
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom