Wanachuo wa St. Joseph (Boko) walalamikia kufelishwa wakidai Chuo kilichukua Wanafunzi wengi kuliko inavyotakiwa ili kujipatia fedha

Sina haja ya kukuaminisha, ila Siku ukikutana na mwanafunzi yeyote wa St. Joseph labda unaweza kuelewa. Wanafunzi wenyewe wanashangaa kwa nini chuo hakifutwi. Hapa nipo na Jamaa yangu ana diploma ya Ualimu kiswahili, ila kamaliza pale na Computer science.
Nabii daniel wewe ni mwanafunzi wa st joseph?tuanzie hapo kwanza
 
Vyuo vingine bhana
Fungua chako tukione
Ngoja nami nitie neno

Kwanza usiwaite "waliopitiswa" sema waliofaulu

Aya ya tatu inamashiko

Usiseme "wanefelishwa kilazima". Sema wamefeli kwani kama wote unaowaita"wamefelishwa" walikua na uwezo mdogo na kupekekea ku-perform below standard Sasa utasemaje umefelishwa ?

Kinacho mfanya mwanafunzi afeli sio idadi ya B Wala C Bali ni GPA kwaiyo hata Kama una B 4 na C mbili pia inabidi useme na masomo aliyofeli (kulingana na idadi ya course per semester) pia na minimum GPA ambayo inamwezesha mwanafunzi kuendelea na masomo ya semister inayofata

Pia kufaulu assignment kipindi Cha masomo huwa SIO GUARANTEE kwa wewe kufaulu mitihani ya mwisho was semister


Kuhusu form za kujaza kwa ajili ya appears ni utaratibu wa kawaida uliopo (nadhani kila chuo ) ambapo ujazwaji wa Hizo form huambatana na gharama ( ndo hiyo mmeambiwa 50000) gharama hutofautiana chuo na chuo

Lakini pia ukijaza form Hizo na kulipa gharama SIO GUARANTEE kwamba utafaulu mtihani ( kufaulu mtihani itategemea na ulijaza Nini)


Nadhani pia kwenye hicho chuo Kuna quality insurance ambayo ndo huwa ina-deal na Mambo ya ubora wa ufundishaji ambapo ilitakiwa kuwasilisha hayo malalamiko yenu lakini sio wakati huu hapa inabidi mjikite kwenye issue ya matokeo

Lakini pia msipeleke "hear says" muwe na ushahidi


Mwisho kabisa usi-blame others for your own failure

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upotoshwaji huu wa wanafunzi walioshindwa kufikisha GPA ya 1.8 kwa wanafunzi wa ufamasia unashangaza. Wakati program nyingine ziko na ufaulu wa GPA ya 2.0 bila malalamiko ninyi mnalalamika kutofikia GPA ya 1.8. muongozo mpya unawataka kufikisha gpa 2.0 na hivyo acheni kujisahau na mitandao ya jamii na mjikite kusoma hakuna muujiza katika kufaulu. Awamu hii mitihani hiyo mnayosema chuo kimewafelisha ilisimamiwa na wasimamizi wa nje waliotumwa na Wizara ya Afya na kuhakiki usimamizi, usahihishaji na utoaji wa matokeo kwahiyo tunaamini waliofaulu ndio wenye uwezo na kipimo sahihi cha kuendelea na muhula wa pili. Kisha mlalamikaji anapaswa ajulishwe kama hajarizika na matokeo kuna taratibu za kufuata anapaswa kuapeal kwa kufuata utaratibu uliowekwa. Na awe mkweli hakuna darasa lililokuwa na wanafunzi 200 ambalo wamefaulu 70 hizo data amepika na nimuongo aliyepanikishwa na kufeli (disco) anashauriwa afuate taratibu husika kupata haki badala ya kusema uongo katika mitandao ya kijamii na kuudanganya umma ambao umejikita katika kujikinga na janga la corona.
Pia aina hii ya wanafunzi katika fani ya huduma ya jamii imejionesha kuwa ilikosea njia inafaa kuangalia choice lingine sio kuhudumia jamii kwa kutoa taarifa za uongo katika jamii.
Mwanafunzi wa afya anapaswa kuwa mkweli, muwajibikaji, mwenye udhati wa kutatua changamoto sio mpiga porojo.
Uwezo wa darasa ni wanafunzi 240 ha hivyo kama walikuwa 200 bado walihitaji wanafunzi 40zaidi kwanini wawapunguze? Acha upotoshaji nenda katafute fani yako huko afya ilulikosea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wahindi ni tatizo hasa wasipofuatiliwa kwa umakini, Songea walikuwa na chuo kikuu chao cha sayansi kisicho na maabala, Siku ya ukaguzi wanaazima vifaa vya maabara kutoka sekondari, Serikali ikakifuta.

Mi nilikua nashangaa, mtu A level amesoma HGL, lakini pale anadahiriwa Bachelor ya Computer science, na anafaulu vizuri.
Acha ushamba kwani ukisoma HGL uhuwezi kusoma Computer Science,mimi nimesoma Masomo ya Arts ila kwa sasa nasoma Database
 
Wanafunzi wa Chuo cha St. Joseph Tawi la Boko linalotoa elimu ya Afya, wamedai kufelishwa na Uongozi wa Chuo hicho na kuambiwa hawawezi kurudi Chuoni hapo na kama wanataka kurudi basi warudie mwaka

Wanadai walifanya mtihani wa UE wakiwa takriban Wanafunzi 200 lakini Wanafunzi waliopitishwa ni 75 ikidhani ni kutokana na chuo hicho kuchukua idadi kubwa ya Wanafunzi kuliko kilivyotakiwa

Kwa kuwa kwa sasa hakuna kwenda Chuoni, Chuo hicho kilifungua makundi ya WhatsApp na kuwaweka wanafunzi, Wanafunzi hao walitakiwa kulipa ada na wasiolipa wanatolewa kwenye makundi hayo ambayo Chuo kilianzisha kikidai ni kwa ajili ya kufundishia

Wanafunzi hao wanadai kuwa Chuo kilichukuwa Wanafunzi wengi ili kupata fedha na sasa baada ya kuwa wamelipa fedha wengi wamefelishwa kilazima.

Wanadai kuna wanafunzi wana Ufaulu wa B nne na C mbili katika masomo ila ameandikiwa amefeli (Discontinuation). Wengi wanashangaa wakidai wana ufaulu mzuri wa 'Assigment 1 na 2' zinazochangia 50% mwenye mtihani wa UE ila wamefeli

Pia, amelalamika kuwa baada ya malalamilo hayo wametumiwa form za kujaza ili kukatia rufaa matokeo yao na kuomba kusahihishiwa upya. Rufaa hiyo ina gharama ya Tsh. 50,000 na mwanafunzi akilipa akifaulu anarudishiwa ila akifeli fedha hairudishwi. Wanafunzi wanadai hiyo ni njia yao ya kupata fedha kwani hakuna mwanafunzi anafaulu

Wanafunzi wanasema kile sio chuo, wanateseka sana, Walimu wanatembea na Wanafunzi na asilimia kuwa ya Wanafunzi waliopitishwa ni wale waliokuwa wakihisiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Walimu. Wameomba ikiwezekana chuo kifungwe na wao wahamishwe
Walimu wanatembea na wanafunzi wa jinsia gani au Ni zote?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ELIMU YA SAINT JOSEPH NI MBOVU MNO, SERIKALI IWE MAKINI
Shida ni moja, serikali haina shida na wataalamu wa course zote, walio mtahani wenyewe kuwaajili, wapo wengi hawewezi kuwamaliza.

Sasa waanze kuangaika na wew msomi mpya umalize salama ili iweje?
 
Baada ya walimu kuona uwezo wa wanafunzi kuwa mdogo kufuatia matokeo ya muhula wa kwanza ambayo wanalalamika kiliona ni vema kuwasaidia kwa kuanza kuwafundisha kwa mfumo wa masafa ili kuwapa fursa ya kuongeza uwezekano wao wa kufaulu lakini waliweka mapingamizi na malalamiko yasiyo na tija kwao na kupenda kukaa bila kuutumia muda huu kwa kuwa huru na shughuli za nje ya kimasomo na kujenga ujuzi wao. Kama chuo tumeshauri na tunasisitiza mudahuu wanafunzi walio na uwezo mdogo wanaweza utumia kuepusha matokeo mabovu na tunahitaji uungwaji mkono na jamii kwa tija ya wanafunzi na taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya walimu kuona uwezo wa wanafunzi kuwa mdogo kufuatia matokeo ya muhula wa kwanza ambayo wanalalamika kiliona ni vema kuwasaidia kwa kuanza kuwafundisha kwa mfumo wa masafa ili kuwapa fursa ya kuongeza uwezekano wao wa kufaulu lakini waliweka mapingamizi na malalamiko yasiyo na tija kwao na kupenda kukaa bila kuutumia muda huu kwa kuwa huru na shughuli za nje ya kimasomo na kujenga ujuzi wao. Kama chuo tumeshauri na tunasisitiza mudahuu wanafunzi walio na uwezo mdogo wanaweza utumia kuepusha matokeo mabovu na tunahitaji uungwaji mkono na jamii kwa tija ya wanafunzi na taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu analialia hapa, ajitokeze bila kutumia ID fake kama wewe ulivyofanya ili umsaidie
 
Shida ni moja, serikali haina shida na wataalamu wa course zote, walio mtahani wenyewe kuwaajili, wapo wengi hawewezi kuwamaliza.

Sasa waanze kuangaika na wew msomi mpya umalize salama ili iweje?
AKILI KUBWA MNO MKUU AGIZA BARAKOA NAKUJA KULIPA
 
Back
Top Bottom