Wanachuo wa St. Joseph (Boko) walalamikia kufelishwa wakidai Chuo kilichukua Wanafunzi wengi kuliko inavyotakiwa ili kujipatia fedha

w0rM

Member
May 3, 2011
68
164
Wanafunzi wa Chuo cha St. Joseph Tawi la Boko linalotoa elimu ya Afya, wamedai kufelishwa na Uongozi wa Chuo hicho na kuambiwa hawawezi kurudi Chuoni hapo na kama wanataka kurudi basi warudie mwaka

Wanadai walifanya mtihani wa UE wakiwa takriban Wanafunzi 200 lakini Wanafunzi waliopitishwa ni 75 ikidhani ni kutokana na chuo hicho kuchukua idadi kubwa ya Wanafunzi kuliko kilivyotakiwa

Kwa kuwa kwa sasa hakuna kwenda Chuoni, Chuo hicho kilifungua makundi ya WhatsApp na kuwaweka wanafunzi, Wanafunzi hao walitakiwa kulipa ada na wasiolipa wanatolewa kwenye makundi hayo ambayo Chuo kilianzisha kikidai ni kwa ajili ya kufundishia

Wanafunzi hao wanadai kuwa Chuo kilichukuwa Wanafunzi wengi ili kupata fedha na sasa baada ya kuwa wamelipa fedha wengi wamefelishwa kilazima.

Wanadai kuna wanafunzi wana Ufaulu wa B nne na C mbili katika masomo ila ameandikiwa amefeli (Discontinuation). Wengi wanashangaa wakidai wana ufaulu mzuri wa 'Assigment 1 na 2' zinazochangia 50% mwenye mtihani wa UE ila wamefeli

Pia, amelalamika kuwa baada ya malalamilo hayo wametumiwa form za kujaza ili kukatia rufaa matokeo yao na kuomba kusahihishiwa upya. Rufaa hiyo ina gharama ya Tsh. 50,000 na mwanafunzi akilipa akifaulu anarudishiwa ila akifeli fedha hairudishwi. Wanafunzi wanadai hiyo ni njia yao ya kupata fedha kwani hakuna mwanafunzi anafaulu

Wanafunzi wanasema kile sio chuo, wanateseka sana, Walimu wanatembea na Wanafunzi na asilimia kuwa ya Wanafunzi waliopitishwa ni wale waliokuwa wakihisiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Walimu. Wameomba ikiwezekana chuo kifungwe na wao wahamishwe
 
Kwa serikali yetu hii duu..
Nadhani hili swala litaishia kuwa la mwanachuo na mzazi wake.

Ni kuomba neema tu huwenda wakapata solution ya malalamiko yao
 
Wahindi ni tatizo hasa wasipofuatiliwa kwa umakini, Songea walikuwa na chuo kikuu chao cha sayansi kisicho na maabala, Siku ya ukaguzi wanaazima vifaa vya maabara kutoka sekondari, Serikali ikakifuta.

Mi nilikua nashangaa, mtu A level amesoma HGL, lakini pale anadahiriwa Bachelor ya Computer science, na anafaulu vizuri.
 
Tatizo la wanafunzi wasiopenda kusoma. Wanafunzi wa St Joseph ni wa Udaktari, inakuwaje wawe zaidi ya 100? Haya ni majungu
 
Wahindi ni tatizo hasa wasipofuatiliwa kwa umakini, Songea walikuwa na chuo kikuu chao cha sayansi kisicho na maabala, Siku ya ukaguzi wanaazima vifaa vya maabara kutoka sekondari, Serikali ikakifuta.

Mi nilikua nashangaa, mtu A level amesoma HGL, lakini pale anadahiriwa Bachelor ya Computer science, na anafaulu vizuri.
Una uhakika na unachokisema? Kwanza mwanafunzi yeyote akidahiliwa lazima ahakikiwe na TCU. Acheni majungu yenu
 
Sina haja ya kukuaminisha, ila Siku ukikutana na mwanafunzi yeyote wa St. Joseph labda unaweza kuelewa. Wanafunzi wenyewe wanashangaa kwa nini chuo hakifutwi. Hapa nipo na Jamaa yangu ana diploma ya Ualimu kiswahili, ila kamaliza pale na Computer science.
 
Mimi nina mtoto yupo pale anasoma udaktari mwaka wa tano acha kudanganya wewe. Kwanini chuo kifungwe? Kama unaona huhitaji kusoma hapo nenda chuo kingine.
 
Sina haja ya kukuaminisha, ila Siku ukikutana na mwanafunzi yeyote wa St. Joseph labda unaweza kuelewa. Wanafunzi wenyewe wanashangaa kwa nini chuo hakifutwi. Hapa nipo na Jamaa yangu ana diploma ya Ualimu kiswahili, ila kamaliza pale na Computer science.
Wewe ni mwanafunzi wa hapo ama unapata taarifa kutoka kwa mwanafunzi wa pale?
 
Unaona jinsi wanavyojikanyaga hawa vijana, umbea tu. UE ni TCU tu. Hawa ndiyo wanaoi water down JF
Mkuu siyo umbea, tatizo ni ujuwaji kuwadharau wenzao hasa wanaosoma vyuo vya kawaida. Wakati huo wote waki graduate wanakutana sehemu moja kwenye interviews za kugombania ajira!

kama hujaelewa soma comments.
 
Wahindi ni tatizo hasa wasipofuatiliwa kwa umakini, Songea walikuwa na chuo kikuu chao cha sayansi kisicho na maabala, Siku ya ukaguzi wanaazima vifaa vya maabara kutoka sekondari, Serikali ikakifuta.

Mi nilikua nashangaa, mtu A level amesoma HGL, lakini pale anadahiriwa Bachelor ya Computer science, na anafaulu vizuri.
1470679339024.jpg
 
Hayo ni majungu matupu.

Wanafunzi wa kizazi hiki wana changamoto nyingi sana za uelewa.

Hapo juu tu ninaona wanasema assignment zinachangia 50%?Ni kozi gani ya afya yenye kuwa na vigezo hivyo?

Mtihani tu ya majaribio na assignment zote kwa pamoja zinachangia 40% na sivyo walivyosema hapo juu.

Hata hivyo pia kama ni kweli katika watu 200 ni 70 tu waliofaulu,kuna tatizo sehemu katika usimamizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wakisha 'disco' ndiyo wanaleta malalamiko mbuzi, wangelalamika kabla kuwa wapo wengi kuliko uwezo wa chou tunge waelewa vizuri sasa wameisha disco ndiyo wana 'table' malalamiko yao??
 
Ngoja nami nitie neno

Kwanza usiwaite "waliopitiswa" sema waliofaulu

Aya ya tatu inamashiko

Usiseme "wanefelishwa kilazima". Sema wamefeli kwani kama wote unaowaita"wamefelishwa" walikua na uwezo mdogo na kupekekea ku-perform below standard Sasa utasemaje umefelishwa ?

Kinacho mfanya mwanafunzi afeli sio idadi ya B Wala C Bali ni GPA kwaiyo hata Kama una B 4 na C mbili pia inabidi useme na masomo aliyofeli (kulingana na idadi ya course per semester) pia na minimum GPA ambayo inamwezesha mwanafunzi kuendelea na masomo ya semister inayofata

Pia kufaulu assignment kipindi Cha masomo huwa SIO GUARANTEE kwa wewe kufaulu mitihani ya mwisho was semister

Kuhusu form za kujaza kwa ajili ya appears ni utaratibu wa kawaida uliopo (nadhani kila chuo ) ambapo ujazwaji wa Hizo form huambatana na gharama ( ndo hiyo mmeambiwa 50000) gharama hutofautiana chuo na chuo

Lakini pia ukijaza form Hizo na kulipa gharama SIO GUARANTEE kwamba utafaulu mtihani ( kufaulu mtihani itategemea na ulijaza Nini)

Nadhani pia kwenye hicho chuo Kuna quality insurance ambayo ndo huwa ina-deal na Mambo ya ubora wa ufundishaji ambapo ilitakiwa kuwasilisha hayo malalamiko yenu lakini sio wakati huu hapa inabidi mjikite kwenye issue ya matokeo

Lakini pia msipeleke "hear says" muwe na ushahidi

Mwisho kabisa usi-blame others for your own failure

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanafunzi wa Chuo cha St. Joseph Tawi la Boko linalotoa elimu ya Afya, wamedai kufelishwa na Uongozi wa Chuo hicho na kuambiwa hawawezi kurudi Chuoni hapo na kama wanataka kurudi basi warudie mwaka

Wanadai walifanya mtihani wa UE wakiwa takriban Wanafunzi 200 lakini Wanafunzi waliopitishwa ni 75 ikidhani ni kutokana na chuo hicho kuchukua idadi kubwa ya Wanafunzi kuliko kilivyotakiwa

Kwa kuwa kwa sasa hakuna kwenda Chuoni, Chuo hicho kilifungua makundi ya WhatsApp na kuwaweka wanafunzi, Wanafunzi hao walitakiwa kulipa ada na wasiolipa wanatolewa kwenye makundi hayo ambayo Chuo kilianzisha kikidai ni kwa ajili ya kufundishia

Wanafunzi hao wanadai kuwa Chuo kilichukuwa Wanafunzi wengi ili kupata fedha na sasa baada ya kuwa wamelipa fedha wengi wamefelishwa kilazima.

Wanadai kuna wanafunzi wana Ufaulu wa B nne na C mbili katika masomo ila ameandikiwa amefeli (Discontinuation). Wengi wanashangaa wakidai wana ufaulu mzuri wa 'Assigment 1 na 2' zinazochangia 50% mwenye mtihani wa UE ila wamefeli

Pia, amelalamika kuwa baada ya malalamilo hayo wametumiwa form za kujaza ili kukatia rufaa matokeo yao na kuomba kusahihishiwa upya. Rufaa hiyo ina gharama ya Tsh. 50,000 na mwanafunzi akilipa akifaulu anarudishiwa ila akifeli fedha hairudishwi. Wanafunzi wanadai hiyo ni njia yao ya kupata fedha kwani hakuna mwanafunzi anafaulu

Wanafunzi wanasema kile sio chuo, wanateseka sana, Walimu wanatembea na Wanafunzi na asilimia kuwa ya Wanafunzi waliopitishwa ni wale waliokuwa wakihisiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Walimu. Wameomba ikiwezekana chuo kifungwe na wao wahamishwe
ELIMU YA SAINT JOSEPH NI MBOVU MNO, SERIKALI IWE MAKINI
Una uhakika?una ushahidi au ni porojo tu? Ifike mahala muelewe hakuna mteremko .. kwanza hakuna chuo kinachopenda kufelisha wanafunzi wake kwasababu kufelisha ni kupunguza mapato...sasa kama unasema basis ya st joseph ni kupata hela akiwafelisha hela zinatoka wapi? jukumu la chuo ni kuhakikisha inakupa elimu bora na hyo ni joint effort katibya mwanafuzni na mwalimu . Mwalimu akimaliza wajibu wake ka we mwanafunzi hutatimiza wako utegemee miujiza lazima ufeli.. someni acheni porojo
 
Back
Top Bottom