TAKUKURU ichunguze malalamiko ya Wanafunzi wa Vyuo kutorudishiwa Fedha za 'Refund', kuna kitu hakiko sawa

Aug 31, 2022
54
99
Kwa takriban miezi miwili sasa kumekuwa na Malalamiko mfululizo kutoka Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu kutoka maeneo mbalimbali nchini ambao wanadai Fedha zao za Refund walizolipa wakati wa kujisajili kisha kuahidiwa kurejeshewa wakati wa kuingizwa fedha za Mikopo lakini hadi sasa wengi hawalipwa, vyuo vingine vimelipa baadhi ya wanafunzi na vingine vimelipa fedha chache.

Vyuo ambavyo hadi sasa vimelalamikiwa kutolipa Fedha za Refund ni Mzumbe, Chuo cha Mwalimu Nyerere, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma, DIT, UDOM, IFM, MZUMBE, Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) na vingine ambavyo sijavitaja hapa. Hivi vyote vinalalamikiwa kutolipa Fedha za Refund kwa Wanafunzi na havisemi sababu nini.

Nashauri Serikali ifanye uchunguzi wa suala hili ikibidi TAKUKURU wafuatilie nini kinakwamisha malipo hayo huku baadhi ya wanafunzi wakiambiwa watalipwa fedha hizo kwenye mwaka wao wa mwisho wa masomo, kitu ambacho sio haki.
 
Aisee hawarudishi. Mi hawakurudisha. Utasugua miguu mpaka ukome.
 
Hivi kuna mtu anajua hawa TAKUKURU wanacho fanya? Inaonesha hawafatilii chochote. Kuna mianya mingi sana ya rushwa na ubadhirifu wa mali za serikali au wananchi lakini wao wapo wanapiga mishahara na labda kushiriki katika kugawana hayo mafungu.
 
Mwaka huku serikali iliongeza Fedha za ada kuwa wanafunzi wengi wa elimu ya juu Tz , kipindi nyongeza inatoka wanafunzi wengi walikuwa washalipa ada hivyo kisheria inatakiwa uongozi wa chuo iwarudishie wanafunzi ada zao.

Wanafunzi wakafuata utaratibu wa kuandika barua za kudai Fedha zao kama jinsi ambavyo uongozi wa chuo ulivyoelekeza ila kinachosikitisha tokea mwezi wa 2 mwishoni mwaka huu mpaka sasa kasi ya urudishaji ndogo sana waliopata sijui kama idadi yao inavuka 20% wakati bodi ya mkopo ishatoa Fedha vyuoni.
 
Nimepewa taarifa za malalamiko kuhusu refund na wanafunzi vyuo kama UDSM ,NIT na SUA .Wengi wameonyeshwa kukata tamaa na kutokuwa na imani na vyuo vyao kuhusu huo mchakato halafu ikizingatiwa hawatoi taarifa kuwa shida iko wapi na watarajie lini.
 
Miongoni mwa nyuzi za malalamiko zlizowahi kuletwa humu kuhusu hiyo kadhia..
IMG_20231026_191724.jpg
 
Hivi kuna mtu anajua hawa TAKUKURU wanacho fanya? Inaonesha hawafatilii chochote. Kuna mianya mingi sana ya rushwa na ubadhirifu wa mali za serikali au wananchi lakini wao wapo wanapiga mishahara na labda kushiriki katika kugawana hayo mafungu.
Nilitaka kuuliza hili swali ..TAKUKURU ipi inazingumziwa hasa ikafuatilie? Najua umenielewa.
 
Back
Top Bottom