Kaunga
JF-Expert Member
- Nov 28, 2010
- 12,530
- 13,469
Moja ya tofauti kubwa kati ya traditional media na social media ni quality ya content. Kwenye traditional media ni rahisi kuhakiki quality kabla ya ku-publish kwa sababu information ina-flow vertically. Information inapitiswa kwanza kwenye chujuo kuchuja pumba zote kwanza kabla ya kuwa released. Lakini kwenye social media information ina-flow horizontally. Matokeo yake ni kuwa na content ambayo ni high quality, low quality na wakati mwingine abusive content.
Social media ina user generated content. How users generate the content depend on their lives, personal experience, likes, dislikes, how they feel about certain things at a particular time. Pia kadri muda unavyokwenda watu wengi zaidi hasa katika nchi zinazoendelea wana-spend muda mwingi zaidi kwenye social media. Kwa hiyo, kutakuwa na mix ya watu tofauti na ilivyokuwa zamani. Tatizo ni kuwa wengi wao bado hawajui nini waandike au wasiandike kwenye internet na implications za kufanya au kutokufanya hivyo.
Social media ina faida zake nyingi tuu. Lakini pia ina limitations zake hasa kuhusiana na uaminifu wa habari zinazowekwa na maana hasa ya interactions ya watu kwenye social media. Lakini pia social media inaleta demokrasia kwenye internet. Wapo wanaopenda hiyo demokrasia lakini pia wapo ambao wangependa ku-dictate nini kiwe kinaandikwa. Kwenye kitabu kiitwacho "The Cult of the Amateur", Andrew Keen ameikandia social media huku akidai it only helps the loudest and most opinionated people to survive. Whether it is true or not I don't know.
Lakini siyo kila kinachoandikwa kwenye social media kinaweza kuleta positive outcomes kama kufundisha, kuelimisha, n.k. Inasemekana kuwa social media inaweza kutumika kama bullying method, ku-maximise sexual satisfaction, sexual propaganda, n.k. Pia tusisahau kuwa JF ni type ya honeycomb framework ya social media ambapo members wanaweza kuamua, pamoja na mambo mengine, kama wanataka kuwa anonymous au ku-reveal their actual identity.
Nadhani, in future itabidi tuwa-treat watu online kama tunavyowa-treat watu mitaani. Kama mtu ni mlevi na hupendi ulevi wake, sidhani kama unaweza kumwambia barmaid au mwenye bar asimwuzie tena bia au ahakikishe anamwuzia soda tuu. Sana sana utamshauri jamaa aache ulevi akikataa it is up to him/her. The same to social media. Kama mtu anaandika utumbo na anaambiwa anachoandika ni utumbo lakini anaendelea kuandika utumbo there is nothing you can do kumzuia kufanya hivyo. Sana sana either utakubali kutokubaliana nae or utamwi-ignore.
In fact, tatizo hili halipo MMU tuu. Lipo pia kwenye majukwaa mengine kama Jukwaa la Siasa. Probably, inabidi tufike mahali tukubali kuwa the way people behave on the internet na hasa hapa JF has changed considerably. Kwa hiyo, it is up to the users wenyewe kuamua kuwa serious kwenye hizo threads, kujihusisha katika threads za majitaka, au ku-igonore kabisa hizo threads. Kuhusiana na utoto ulioingia MMU na kwingineko, inawezekana kweli kuna watoto hapa na hivyo watakachoandika hakitakuwa relevant kwa wakubwa and vice versa.
kwenye red ndicho nilichoazimia kuanzia mwaka huu, na nafikiri si rahisi kumbadilisha mtu na huenda si sahihi sana kwani sina authority na maisha au jinsi mtu anavyopaswa kuishi maisha yake na mwisho nani kasema mtazamo wangu ndio sahihi?
Nimejifunza kuignore nyuzi nyingi sana bila kutia neno (ingawa Eiyer katika uzi wake alisema ni ushetani huo) nikiombwa ushauri nitatoa lakini sioni usahihi wa kuimpose morals zangu kwa watu wengine.
Last edited by a moderator: