Wana-jf nimefiwa na mke wangu!!

Duuu!!! Pole sana mkuu! Mungu akutie wewe pamoja na watoto ktk kipindi hivi kigumu. Poleni sana.
 
Pole sana mkuu,Mungu mfariji akupe faraja wewe na watoto
 
Sajenti, ni Mungu pekee awezaye kukupa faraja ya hakika na ya kweli, mtazame yeye tu, atakufariji kwa faraja na pendo lake kuu la kweli na la ajabu.
 
Pole sana afande wangu, jipe moyo mkuu, sote twaelekea huko. Mungu akujaalie uvumilivu ktk kipindi hiki.
 
Pole sana mkuu .
Mwenyeenzi Mungu akuuongeze faraja zaidi
Wewe na wanawe . Na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi ..
 
Inna Li Llahi wa Inna iLlahi Rajiun.

Mwenyeezi Mungu akupe subira. Ni mtihani mzito sana, inapaswa ukumbuke kuwa hiyo ndio njia yetu sote, mwenzetu katutanglia na sisi sote tupo nyuma yake.
 
Pole sana maana yeye alisema:
KAMA ULIVYO NAYE ALIKUWA!!!!!!
NA KAMA ALIVYO WEWE PIA UTAKUWA!!!!!!!
 
Nasikitika kuwafahamisha kuwa nimepata msiba leo alfajiri mke wangu kipenzi amenitoka. Kimsingi mazishi yamefanyika leo saa 10 kwenye makaburi ya changanyikeni...wife ameniachia watoto wawili wa kike 11 & 8.

Pole sana kwa msiba mkubwa namna hii; nakuombea faraja wakati huu wa majonzi makubwa. Mungu akuinue na kukupigania na aipumzishe roho ya marehemu pema peponi Amina.
 
Nasikitika kuwafahamisha kuwa nimepata msiba leo alfajiri mke wangu kipenzi amenitoka. Kimsingi mazishi yamefanyika leo saa 10 kwenye makaburi ya changanyikeni...wife ameniachia watoto wawili wa kike 11 & 8.

Pole sana! ni wakati mgumu kwako ila ukimwamini Mungu, utapata faraja ya kweli. May she rest in peace! AMEN
 
Pole sana Sajenti, Mungu akupe faraja,nguvu na matumaini zaidi. Amepumzika palipo na amani,shukuru kwa yote!
 
Nasikitika kuwafahamisha kuwa nimepata msiba leo alfajiri mke wangu kipenzi amenitoka. Kimsingi mazishi yamefanyika leo saa 10 kwenye makaburi ya changanyikeni...wife ameniachia watoto wawili wa kike 11 & 8.

Inna Lillah Waina Illahi Rajoon

“Sisi ni wa Allaah nasi Kwake tutarejea, Ee Mwenyezi Mungu Walipe wafiwa kwa msiba huu na uwape badili yake bora kuliko huo”

“Ewe Mwenyezi Mungu msamehe marehemu na ipandishe daraja yake katika walioongoka, na weka badili yake kwa aliyowacha nyuma na utusamehe sisi na yeye ewe Mola wa viumbe vyote na umkunjulie yeye katika kaburi lake na umtilie mwangaza ndani yake”

Pole sana mkuu wangu, kuwa na subra katika kipindi iki kigumu na Mwenyezi Mungu atakupa faraja
Insha'Allah.
 
Back
Top Bottom