Wamiliki wa shule binafsi kwanini matangazo yenu katika shule zenu kipaombele ni kujua Kiingeleza na kufaulisha watoto?

mr pipa

JF-Expert Member
Jul 26, 2021
2,330
4,854
Ningependa mnishawishi kupitia hilo mkitoa haya mnayotutangazia, kuna kipi cha ziada ambacho mtoto wangu anaweza kunufaika nacho kwa hapo baadae, hasa kwenye hizi shule zenu.

Maana ufaulu sio kigezo kwa sasa na hata lugha sio kipaombele kwa sasa kutokana na teknolojia ilivyokuwa hauhitaji kujua lugha kama mnavyotuaminisha ingekuwa hivyo kila raia wengebaki kwenye mataifa yao.

Mfano kuna mikutano ya kimataifa inayojumuisha pengine viongozi wa nchi mbali mbali hivi mnataka kuniambia wale wote wanajua lugha moja inayoongelewa sehemu husika mfano raisi wetu huyu wa sasa ni kweli anajua kuongea kichina, kifaransa, au kireno, Kama sio Ni kipi kinachowafanya wote wakaelewana pindi wanapoongea?

Jibu ni teknolojia sasa kwanini mkazanie kiingeleza, na kufaulisha ndio kiwe kipaombele chenu hebu mnishawishi ili nijipange kumleta mwanangu kwenye shule zenu
 
Back
Top Bottom