R-K-O
JF-Expert Member
- Jun 27, 2023
- 482
- 2,138
Tajiri unakuta ana mabilioni lakini suala la elimu ya mtoto kwake analifanya liwe la kuiga watanzania wanaosifia elimu nzuri ni mtoto akisoma shule hizi za Necta huko boarding awe anaamka saa 11 asubuhi, apate division 1 au 2 aende kusoma UDSM.
Kwa elimu ipi hapa bongo uendelee kumsomesha mtoto wako kama pesa unazo ?
Kuna shule zipo zina mitaala ya cambridge mtoto anaunga moja kwa moja vyuo vizuri, hadi mtoto anamaliza degree yake ni kama milioni 500 hadi 900 hivi.
FAIDA ZA KUSOMESHA WATOTO SHULE ZA CAMBRIDGE
Huku mtoto hata awe na uwezo wa kawaida darasani lugha zitamkaa sawia barabara, ataongea kiingereza na kifaransa kama maji, sio hivi viingereza vya english medium vina lafudhi ya kibantu, huyo mwalimu anaefundisha ukimletea mzungu anaomba arudie rudie anachosema kila mara, mtoto ukimwekea mziki wa chris brown aandike mashairi uki google hayo mashairi ukianza kufananisha unaona bado mwepesi.
Mtoto akihitimu huku hata kama ataajiriwa basi ni ajira nzito nzito, wakihitimu vyuo wanapata wepesi wa kuaminiwa na mashirika ya Kimaifa kama UN, UNHCR, UNICEF, connection huwa zinawasaidia sana lakini pia hizi shule mtu anaweza awe na uwezo wa kawaida darasani lakini anazungumza lugha tatu tofauti na zote ni kimataifa, chuo kasoma huko oxford, field kafanya mashirika makubwa huko ulaya na marekani, hapa kupenya inakuwa fasta. na sidhani kama kuna hasara endapo mtoto akisoma shule hizi na akaja kupata ulaji hapa hapa Tanzania sehem kama benki kuu, bandarani, ikulu, tanapa, n.k.
Kibiashara anapata exposure kubwa sana kusafiri nje ya nchi, kukuana na wenzie wa mabara tofauti, kujua mifumo ya kidunia, n.k. kama baba anamiliki mashamba mengi ya mihogo anawauzia wahindi elf 10 kwa debe wao wanaenda kuuza laki 2 huko uingereza, hapa mtoto anaweza kutumia maarifa na connections ajifunze kufikisha mwenyewe huo mzigo pesa yote inabaki kwenye biashara ya familia.
Sasa Tajiri ana Mabilioni ni vipi elimu ya mwanae anajibana bana ?