Wamiliki wa Bodaboda za biashara tukutane hapa

Zanz spices nimependa idea yako.
Kwa upande wangu namiliki BAJAJI ya abiria, sina uzoefu sana lkn ningependa kujua suala la siku 6 za kazi na 1 ya dereva imekaaje mana dereva wangu ananiambia siku 5 kazi, siku ya sita service ya saba inakuwa cku ya dereva.
Duuuh! Hii haijakaa poa sana. Hivi service ya bajaji inachukua siku nzima?? Mimi madereva wangu wanaleta hesabu kila siku ila sikukuu huwa nawapa ofa wafanye kazi na hesabu inakuwa yao ila sharti warudishe mapema bajaji. Nafanya nao kazi vizuri, hakuna cha leo siku ya dereva wala nini, ila tumepeana hesabu ya kawaida sio ya kumuumiza sana dereva. Pia nawavumilia na kuwasikiliza shida zao bila kuziendekeza. Nawapenda madereva wangu, nawaheshimu pia.
 
15,000x7x30=3,150,000
Iko powa hiyo.
Ukimpata wa hivyo mpe tu. faida yake ni 50% kwa muda wa miezi sita. Hiyo ni super profit.
Nilifanya uchunguzi kwa madogo hatimaye nikampata dogo mmoja ambaye hatumii kilevi cha aina yoyote na pia anaishi kwao(kwa baba na mama) tunasali nae jumuiya
 
Mkuu hii hapa chini ni katika utaratibu wangu wa kuuza kila baada ya miezi sita ili kubadilisha nyingine na kumpa tena Driver.
Angalia hapo ikiwa na only six months na wiki tatu tangu kutumia.Sasa utuzwaji huo unatokana na hamasa kwa Driver kwamba pindi nikiiuza nampa percentage fulani ya bei kama motisha kwa matunzo.
Badi wanashindana kwa umaridadi.

Na Boxers zote nilizifunga GPS Tracking System,maana kipindi cha nyuma hali ilikuwa inatisha sana kwenye Boxers,hizi nyingine maana hazipo kwenye Target sana ya kuibiwa sijaweka,ili ni cost karibia laki nne kwa kila moja kuifunga.Ila nikiiuza huwa naitoa.Maana huwa nalipia huduma hiyo kwa Mwaka.

Hii hapa mkuu,ambayo nilii replace mwezi wa tano mwaka huu.Na hii ndio latest picha wakati namtumia mnunuaji,basi haikufika siku ya pili akanitafuta mbio,nikamuelekeza mdogo wangu wanakutana Bank na Lawyer wangu kesi ikaisha.Alilipa depost then muda wa Two weeks akamalizia akaja kuichukua
View attachment 295889
Mkuu pikipiki iliyotumika miezi sita huwa unaiuza bei gani? Pia bodaboda huwa zinahitaji service kwa muda gani na inagharimu shiling ngap?
 
Mkuu pikipiki iliyotumika miezi sita huwa unaiuza bei gani? Pia bodaboda huwa zinahitaji service kwa muda gani na inagharimu shiling ngap?
Nimependa huo ulinzi tu ntakutafuta mkuu
Duuuh! Hii haijakaa poa sana. Hivi service ya bajaji inachukua siku nzima?? Mimi madereva wangu wanaleta hesabu kila siku ila sikukuu huwa nawapa ofa wafanye kazi na hesabu inakuwa yao ila sharti warudishe mapema bajaji. Nafanya nao kazi vizuri, hakuna cha leo siku ya dereva wala nini, ila tumepeana hesabu ya kawaida sio ya kumuumiza sana dereva. Pia nawavumilia na kuwasikiliza shida zao bila kuziendekeza. Nawapenda madereva wangu, nawaheshimu pia.
 
Mkuu hii hapa chini ni katika utaratibu wangu wa kuuza kila baada ya miezi sita ili kubadilisha nyingine na kumpa tena Driver.
Angalia hapo ikiwa na only six months na wiki tatu tangu kutumia.Sasa utuzwaji huo unatokana na hamasa kwa Driver kwamba pindi nikiiuza nampa percentage fulani ya bei kama motisha kwa matunzo.
Badi wanashindana kwa umaridadi.

Na Boxers zote nilizifunga GPS Tracking System,maana kipindi cha nyuma hali ilikuwa inatisha sana kwenye Boxers,hizi nyingine maana hazipo kwenye Target sana ya kuibiwa sijaweka,ili ni cost karibia laki nne kwa kila moja kuifunga.Ila nikiiuza huwa naitoa.Maana huwa nalipia huduma hiyo kwa Mwaka.

Hii hapa mkuu,ambayo nilii replace mwezi wa tano mwaka huu.Na hii ndio latest picha wakati namtumia mnunuaji,basi haikufika siku ya pili akanitafuta mbio,nikamuelekeza mdogo wangu wanakutana Bank na Lawyer wangu kesi ikaisha.Alilipa depost then muda wa Two weeks akamalizia akaja kuichukua
View attachment 295889
Ulinzi wa GPS umenivutia je ni effective maeneo yote mkuu au kwa mjini tuu
 
Bora Uzi huu umeanzishwa. , binafsi natafuta pikipiki nianze biashara ..nawaza kununu Pikipiki kwa mtu mwenye anayeuza Ukiwa katika hali nzuri, I mean kwa hawa wanaosema wanabadilisha kila baada ya miezi kadhaa.
Nipo Dsm.

Atakayekua nayo Basi naomba aniPM.
 
Asante mkuu nitakupa maelezo kwa ninavyoelewa,ila wengine watajazia,maana mie binaadam na sio mkamilifu wa kujua kila kitu,nitakapokosea watu watarekebisha.

Kwanza lazima uwe unaipenda hii biashara,sio kuona kwamba fulani anaifanya,au wengine hupenda kuitwa maboss.
Maana siku hizi ukiwa na bodabodam moja tu,basi kama Driver wako anapaki kituo fulani basi yeye anakuita boss,sasa na wenzie woote ukipita pale unasikia boss wake fulani yuleee,sasa kuna wengine wagonjwa kweli kuitwa boss wanaona rahaaa,hovyo kabisa
Sasa lazima iwe kwenye dam,na ukubali changamoto zake,ni biashara ngum sana ila nyepesi kama unajitambua.
Maduka mengi unapoenda kununua wanakusajilia pale pale kila kitu kama ukienda Mapema.Mie huwa naenda pale makao makuu ya Boxer duka lao kubwa.Na ukifika mapema wanakusajilia kila kitu an pia wanaku advise bima.So unatoka pale umekamilika,kinachofuata ni siku ya pili mwenyewe kwenda TRA ambapo ni procces fupi saana.
Unaweza haya yote ukayamaliza ndani ya siku mbili tu ukaanza kazi.
GPS system hii inategema na system ipi unatakiwa uwekewe ina specifications nyingi mno.Na kila moja ina gharama zake.zipo hadi zinaangalia mafuta yamo lita ngapi,zipo ambazo unazowez kuzima mwenyewe hata kama upo ulaya
Sasa kwa bodaboda,unaweka ila ya kawaida tu ya kuwezesha kujua chombo kipo wapi,na access ya Start and off.Halafu unapewa short training pale na consultation ya kuweza kutambua kama chombo chako kimeibiwa kutokana na speed na pia muelekeo wa chombo chako.Maana unaweza kuona kitu kinaeleke dodoma,hapo lazima utastuka,so unaweza kuwasiliana na kituo cha polisi na wakaikamata na unaweza pia kuizima ukiwa popote pale.
Ila wengi wakiibiwa na kama mwizi hajui,basi mtu huizimi,ila unawasiliana na kampuni iliyokufungia,then wao wana link a poloce wa kwenye doria kisha wanaikamata hata kama ipo Kyela huko.

KWa ufupi hakuna usumbufu wowote,unaponunua bodaboda ndio unasajiliwa kila kitu,inabakia wewe tu kwenda TRA kupata kadi maalum kama chombo cha biashara.GPS kuna mtu naweza kukupa number yake ila siku hizi kampuni nyingi saana wanafunga hizi stystem so unaweza ku google na ukazipata

Zanzibar Spices naomba namba za watu wa gps niwatafute mkuu
 
Komaa kaka,we hata ukiibiwa Bodaboda moja kaza ongeza nyingine huku kesi ikiendelea.
Yaani hii biashara aisee inalipa asikudanganye mtu,ila kama mtoto wa mama unakimbia changamoto basi kaa mbali kabisa na biashara hii,utakuwa unanunia watu kila siku kwa kesi za Drivers,hahahaha

Maana wapo wamiliki hawataki kusikia Driver anaumwa wala anapata msiba wala anauguza,ebbbbo.
Na ndio maana wengi huwa hawabarikiwi kwenye game hii,maana wao wanajiangalia wao tu na pesa.

Mfanye Driver wako kama familia yako.Mie wapo Drivers wangu waliofiwa na wazee wao,basi huwa ndugu zangu waliopo Dar wanaenda msibani,na pia mie pia husafiri na kuja msibani au kama ninakazi basi Wife anapanda boat anakuja Dar kama siku nne then anageuza.Lakini lazima kati ya mie au wife aje Dar.Na the same akipata ajali lazima ndugu zangu wa Dar wahusike na the same time mie au wife anakuja Dar kumpa pole na kutoa mkono wa Pole.

Na kama ni ajali basi matibabu yoote tunasimamia sie,hata kama uzembe ni wa Driver basi mie huwa siangalii uzembe wake,kwanza ni kumshughulikia tiba yake then akiwa mzima ndio mengine yanafuata.Na sijawahi kumlaumu Driver kwa Uzembe wala kumlipish,maana hakuna anaependa ajali,muhim ni ushauri tu.Kisha natengeneza chombo changu siku zinaenda,na mungu mkubwa kwamba ajali nyingi sio kubwa saana.

Nikitengeneza naenda kugombana na watu wa bima,maana hawa jamaa wabishi kulipa kama wao hakuna.Wanaona Bodaboda kama vile ndio chanzo cha ajali zoote kumbe wazembe njiani ni wengi tu.
Hongera sana mkuu kwa kujali
Drive wako hakika lazma
Mungu akubark kwa wema huu
 
Uzi mzuri sana huu na mimi ni mmoja wapo wa wamiliki wa boxer tatu na bajaji moja,,
Na Kwa week kwa makubaliano yetu ni 60,000Tsh ambayo kwa siku 6 ni 10,000 afu siku moja ya dereva ila mi sina mkataba na pikipiki napiga tu ya kawaida na bajaji ni 105,000Tsh kwa week na kwa siku ni 15,000 ila kuna changamoto zake ambazo ni ;

1.matengenezo ya hapa na pale kama vifaa kuharibika sanasana ni spoketi na kubadilisha tairi ,,

2.Mvua kunyesha ambapo zikinyesha huharibu sana mahesabu yetu ya week inabidi madereva waniombe niongeze tena siku moja au mbili mbele ya kupokea hesabu,,

3.kukamatwa na polisi kwa makosa ya wrong parking na bima ambapo utatakiwa kutoa 30,000Tsh kuikomboa pikipiki yako kituoni na hii huku kwetu luguruni na mbezi mwisho hutokea ila sio mara kwa mara.

4.Na hii ni upepo wa abiria kuwa wachache pindi chuo kikifungwa ambapo sisi huku hutegemea sana wanafunzi wa chuo kwa ajili ya usafiri kwa hiyo inabidi dereva aunganishe week mbili ili akujumlishie hesabu yako yote ya week mbili.

5.Matatizo binafsi ya dereva anaweza akakwambia yeye au ndugu ama mzazi anaumwa kwamba ela katumia kwa matibabu au kalipia chumba chake cha kupanga inabidi tu uvumilie week mbili ili akuunganishie ela yako yote.

Angalizo kwa hizi changamoto usipokuwa mvumilivu kwa dereva wako mnaweza shindwana kwa kweli inahitaji uvumilivu wa hali ya juu maana matatizo yapo kwetu sote na inabidi wote tusikilizane...!!!!!!!
 
Angalizo pia kwa wamiliki,hili nimekuwa nikilisema sana pia:-
Pindi unapoomba dua au maombi wakati unaenda kazini au unapoamka,basi ombea pia drivers wako au waajiriwa wako ili mungu awalinde na awape wepesi kwenye biashara yao,ikiwemo kupata wateja wengi na wenye kheir na huduma hizo.Maana Driver akipata na wewe ndio umepata.

Na kwa sie Waislam ni kwamba Mtu ukimuombea dua njema mwenzio basi mungu anakuongezea wewe zaidi,na pia hutenga malaika wa kukuombea na wewe zaidi.Ila wengi wetu kidogo hili ni tatizo.Maana hata hawa Drivers tunaowaajiri na wao pia hutuombea sie mabosi wao ila tunakuwa hatujui,maana anaomba kwamba usifilisike,na ufanikiwe zaidi,ili leo na kesho na yeye umkumbuke pindi neema zinapozidi.

Mie Drivers wangu karibia wote ni wakristo,ila katika kila sikukuu zao kwa wale nilionza nao muda wa mwaka,basi huwa natoa pesa ya sikukuu zoote kwa imani yake.Na hesabu ya siku moja au mbili za sikukuu naiacha ili na yeye aweze kuhudhuria ibada kanisani,na pia apate muda wa ku enjoy na watoto nyumbani na kuwapeleka sehem za michezo ya watoto nk.
Unapokuwa na furaha nyumbani wewe na watoto basi jua na mwenzio umkumbuke kwa imani yake.

Ila wengi wetu aisee,akiisha nunua huwa hana lugha njema,yaani ni ku force kwenda mbele,kuna jamaa mmoja yeye ni mtu wa Ulabu,basi anaweza kumstukiza Driver hata kati ya wiki ampelekee pesa bar.Asipopeleka kazi kweli.
Sasa hata hawa Drivers wanachangamoto zao nyingi sana kutoka kwa Matajiri,na ndio maana Drivers wengi hupenda kudeal na chombo anachomiliki Mwanamke.
Mkuu ubarikiww kwa darasa napata vingi
 
Katika biashara ya kivivu ambayo haina faida ni boda boda....

Na ninawashangaa saana wanaofanya iyo biashara km sehemu ya kutengenezea pesa....

Mwelewa katika mambo ya pesa hawez fanya iyo boda trade...

Unanunua pikipiki 2m alafu unapata buku 7 per day... it means mpaka miezi kumi baadae ndio uanze kupata buku 7 per day km faida...

Na izo hesabu hapo haujakutana na majanga ivyo........

Then bado trafic n.k

Sasa je.... kama iyo 2m ungeiweka kwenye biashara ingine... ina maana kwa miezi kumi ungepata zaid ya iyo buku 7 ya boda....

Tatizo nyie wana boda boda munaangalia saaana kinachoingia kuliko kilichotoka...

Income-Starting package=profit
 
Fact
 
Zanzibar Spices
Hongera kwa ushauri mzuri, sasa kwa wiki 50k baada ya miezi sita hela inakuwa imerudi? Ukiuza kama boxer unaiuza kiasi gani muda huo?
 
Katika biashara ya kivivu ambayo haina faida ni boda boda....

Na ninawashangaa saana wanaofanya iyo biashara km sehemu ya kutengenezea pesa....

Mwelewa katika mambo ya pesa hawez fanya iyo boda trade...

Unanunua pikipiki 2m alafu unapata buku 7 per day... it means mpaka miezi kumi baadae ndio uanze kupata buku 7 per day km faida...

Na izo hesabu hapo haujakutana na majanga ivyo........

Then bado trafic n.k

Sasa je.... kama iyo 2m ungeiweka kwenye biashara ingine... ina maana kwa miezi kumi ungepata zaid ya iyo buku 7 ya boda....

Tatizo nyie wana boda boda munaangalia saaana kinachoingia kuliko kilichotoka...

Income-Starting package=profit
Una dharau pesa??
Aisee nimekushangaa sana we jamaa. Si bora wao wanaoingiza elfu saba kwa siku, na wanaouza voch wanaIngiza sh ngapi kwa siku??
Hakuna biashsra isiyo na risk wala challengs, weakness. Hakuna.
Everything have an imperfection. Hakuna kilicho kamili, kwa maana hata penseli ikawekewa erraser.

So usidharau wala kukatisha tamaa juhudi za mtu.
 
Haujasoma na kuelewa nilichokiandika... rudia teena ucomment vizuri.

Inshu ni kwamba unawekeza million 2 afu haupati faida yoyote mpaka miezi kumi ipite... wakati iyo million mbili ungewekeza kwingine... ungepata faida mapema saana.... hapo nadharau pesa vipi sasa...

Usicomment tu... uwe unasoma na kuelewa kilichoandikwa...

Mimi nishafanya iyo biashara.. inazngua na ni maalumu kwa wavivu na waoga wa kurisk... eti million mbili afy faida baada ya miez 10..

What the https://jamii.app/JFUserGuide... hata ningeamua kulima maaragwe isingefika miezi kumi kuona faida....
 
Back
Top Bottom