Hafidhibrahim
Senior Member
- Nov 4, 2014
- 142
- 32
Angalizo pia kwa wamiliki,hili nimekuwa nikilisema sana pia:-
Pindi unapoomba dua au maombi wakati unaenda kazini au unapoamka,basi ombea pia drivers wako au waajiriwa wako ili mungu awalinde na awape wepesi kwenye biashara yao,ikiwemo kupata wateja wengi na wenye kheir na huduma hizo.Maana Driver akipata na wewe ndio umepata.
Na kwa sie Waislam ni kwamba Mtu ukimuombea dua njema mwenzio basi mungu anakuongezea wewe zaidi,na pia hutenga malaika wa kukuombea na wewe zaidi.Ila wengi wetu kidogo hili ni tatizo.Maana hata hawa Drivers tunaowaajiri na wao pia hutuombea sie mabosi wao ila tunakuwa hatujui,maana anaomba kwamba usifilisike,na ufanikiwe zaidi,ili leo na kesho na yeye umkumbuke pindi neema zinapozidi.
Mie Drivers wangu karibia wote ni wakristo,ila katika kila sikukuu zao kwa wale nilionza nao muda wa mwaka,basi huwa natoa pesa ya sikukuu zoote kwa imani yake.Na hesabu ya siku moja au mbili za sikukuu naiacha ili na yeye aweze kuhudhuria ibada kanisani,na pia apate muda wa ku enjoy na watoto nyumbani na kuwapeleka sehem za michezo ya watoto nk.
Unapokuwa na furaha nyumbani wewe na watoto basi jua na mwenzio umkumbuke kwa imani yake.
Ila wengi wetu aisee,akiisha nunua huwa hana lugha njema,yaani ni ku force kwenda mbele,kuna jamaa mmoja yeye ni mtu wa Ulabu,basi anaweza kumstukiza Driver hata kati ya wiki ampelekee pesa bar.Asipopeleka kazi kweli.
Sasa hata hawa Drivers wanachangamoto zao nyingi sana kutoka kwa Matajiri,na ndio maana Drivers wengi hupenda kudeal na chombo anachomiliki Mwanamke.
mungu akubarik sana kk endelea na moyo uo uo gud