Wazoefu wa biashara ya bodaboda naomba msaada wa mawazo

demand

JF-Expert Member
Jul 21, 2023
272
572
Natumaini hamjambo, na wengne mnajitahidi allah atufanyie wepesi katika afya na maeneo yetu ya ridhiki.

Kimsingi nataka kujarbu kufanya biashara ya bodaboda, nimejarbu kufanya tafiti ndogo nimegundua changamoto kubwa ni derava kutoleta hesabu kama inavyotakikana, wizi wa vyombo, ajali (hii inaweza kutozuilika) nk.

Naomba ushauri kwenye mambo yafuatayo:

1. Boda iwe mpya au used.
2. Hesabu au mkataba (japo binafsi napendelea hesabu) huku used ni 6000 mpya ni 7000/8000 mkataba 10000
3. Usimamizi upi utakaofaa angalau kupunguza changamoto

Nawasilisha, kwa unyenyekevu mkubwa

Ninyi ni watu wema.
 
Kama upo Dar es salaa mwambie boda kuwa awapo barabarani yeye ndo research ya uboreshaji wa huduma barabarani , Hana haki sawa na wenye magari... Mana hawa watu Wana vibri mwisho hutia hasara Sana mabosi zao na nyumbani kwao kuwa vilema na vifo
 
Unaikatia bima
 
Back
Top Bottom