Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,252
- 113,647
Mahojiano aliyoyafanya mkuu wa majeshi mstaafu yametufungulia kaupenyo kwenye dirisha la kilichokuwa kinaendelea kwenye siku za mwisho za uhai wa Rais Magufuli.
Kitendo cha mkuu wa majeshi na wenzake waliokuwepo wakati Rais Magufuli anavuta pumzi yake ya mwisho na ‘sintofahamu’ iliyojitokeza juu ya nini kifanywe baada ya kufa kwa marehemu wakati katiba iliyopo inaelezea vizuri tu utaratibu wa kurithi madaraka endapo Rais aliyekuwepo madarakani anakufa au anashindwa kufanya kazi yake ni hukumu mbaya dhidi ya CCM kuhusu utamaduni wa kuvunja katiba walioutengeneza wao wenyewe.
Katiba iko wazi kuhusu utaratibu wa kurithi uongozi wa nchi.
Lakini kumbe kulitaka kutokea ujanja ujanja wa kuvunja tena katiba mkiuke taratibu zilizopo.
Tutawalaumu vipi hao watu [sina hakika sana ni akina nani] wakati marais wa Tanzania ndo vinara wa kuvunja katiba?
Wenyeviti wa CCM ndo wavunja katiba wakuu. Kuanzia Nyerere mpaka Samia….wote wavunjaji wa katiba hawa.
Ndo maana haishangazi kuona au niseme kusikia kuwa kuna watu walitaka tena kuikiuka katiba na kufanya vile watakavyo wao baada ya Magufuli kufariki.
Ambaye angekuwa mhanga wa hilo naye alipoingia madarakani akaendeleza mambo yale yale ya uvunjaji wa katiba kana kwamba hakupata somo la kuiheshimu katiba walipotaka kumtenda.
Kaingia madarakani akaendeleza mambo yaleyale ya kupiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa [ambayo ni haki ya kikatiba] na akatoa kisingizio dhaifu sijapata kuona. Eti anatengeneza uchumi kwanza.
Hilo zuio haramu halipo tena. Ina maana uchumi ulishatengemaa?
Na ni wapi kwenye katiba panapomruhusu yeye kuzipiga marufuku haki za kikatiba kwa kisingizio cha kujenga uchumi?
Marais wote wa Tanzania ni wavunjaji wa katiba. Haishangazi kusikia kuna wengine nao walitaka pia kuivunja katiba kwenye kuurithi urais!
Uvunjaji wa katiba Tanzania ni zao la CCM na wala huwa hawakemeani. Sana sana huwa wanateteana.
Hivyo, waliotaka kuivunja katiba na kumtenda makamu wa Rais Samia, wala wasilaumiwe sana.
They are products of their environment.