Ikitokea umeshauri mtu avae Hijab nyekundu, huyo mtu akavaa, utajisikiaje? Kwa hili, Big Up Rais Samia na Serikali yako kwa kuwa wasikivu

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,504
113,618
Wanabodi
Jumapili ya leo, ni March 26, 2023, nimepata tena fursa ya kuja na makala nyingine ya kwa maslahi ya taifa.

Mabandiko mengi humu JF ni mabandiko kuhusu habari na matukio "news and events", kuzungumzia watu na matukio, lakini ni mabandiko machache sana humu ni ya mawazo tuu na vitu vya kufikirika.

Bandiko hili ni la swali la jambo la kufikirika tuu, kwa lugha ya wenzetu inaitwa hypothetical situation, yaani ni jambo la kufikirika tuu lakini lenye yumkini ya kuyumkinika au uwezekano wa kuwezekanika linalotokana na kitu kinachoitwa psychoanalysis ambalo kwa bahati mbaya sana mimi sijui Kiswahili chake. Hapa naomba msaada kwa mabingwa wa lugha yetu adhimu ya Kiswahili wanitafasirie neno hypothetical situation, psychoanalysis, psychoanalist, na psychoanalytic.

Swali lenyewe ambalo ni swali la hypothetical situation ni hili "Ikitokea kuna event fulani ambayo inakwenda kutokea kesho ambapo mgeni rasmi ni kiongozi fulani Mkuu wa nchi ambaye ni rais wa nchi, kwa vile huyu ni rais wa nchi, nyinyi wananchi wote mnamfahamu, ila yeye hawezi kuwafahamu nyinyi wananchi wote hivyo wewe mwananchi wa kawaida unaamua kumshauri avalie Hijab Nyekundu na gauni la Navy Blue, atatokelezea sana!. Japo kiongozi huyu ana washauri rasmi ambao hao anawasikiliza lakini pia sisi wananchi pia tunamshauri maoni yetu kupitia njia zetu, sasa unapoona ushauri wako umefanyiwa kazi, jee ungekuwa wewe ungejisikiaje?.
(up date- ushauri huu niliutoa Jumapili ya March 26, 2023.
Jumanne 28, Tanzania tulipata ugeni wa Makomo rais wa Marekani, Bi Kamala Harris.
Alhamisi Kamala akamtembelea Rais Samia Ikulu DSM, angalia Rais Samia amevaa nini Ikitokea umeshauri mtu avae Hijab nyekundu, huyo mtu akavaa, utajisikiaje? Kwa hili, Big Up Rais Samia na Serikali yako kwa kuwa wasikivu )

Jumapili Nilijisemea kuhusu Hijab Nyekundu,, Alhamisi Hijab Nyekundu ikavaliwa...!, unaweza kusema ni just a coincidence!, mimi nakuambia it's not!.

Angalia hapa nimeshauri nini, Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!

Leo asubuhi nimepokelewa na taarifa hii humu JF Serikali: Mchakato wa Katiba Mpya na maboresho ya Sheria ya vyama vya Siasa na Uchaguzi, sasa kuanza na hii
Ndumbaro Adai Katiba Mpya ni hitaji la Watanzania kwa sasa

Jambo umelipigia kelele sana mara linakwenda kutekelezwa Jee ungekuwa wewe ungejisikiaje?.

Kwa vile mimi ni mtu wa mastori mastori, kuna wengine wanapenda mastori mastori na wengine sio hawapendi bali hawana muda wa kusoma makitu marefu, wao wanataka kitu kifupi short and clear, hivyo kwa wale wa short and clear ishieni hapa na kujump to conclusion.

Wale wa mastori mastori, tuendeleeni...
Sisi kama binadamu tuna kitu kinachoitwa colours preferences ambapo mtu akivaa nguo za rangi fulani, wewe unamuona mtu aliyevaa nguo za rangi hizo amependeza sana na kuna rangi mtu akivaa unamuona kama amechukiza.

Mfano mimi tangu nikiwa mdogo niliipenda timu ya Simba kwasababu tuu za rangi ya jezi yake Nyekundu na nyeupe na kuichukia timu ya Yanga kwasababu tuu ya rangi ya jezi yake ya Kijani na Manjano.

Matokeo yake nikawa nachukia chochote cha kijani na manjano, wala sikuwahi kujidhania itafika siku mimi Pasco Mayalla naweza kuvaa nguo ya njano au kijani mpaka nilipojiunga CCM!.

Kufuatia kuipenda rangi Nyekundu mtu akivaa chochote chenye red naona kama unapendeza!.

Hivyo kila nikimuona rais wa nchi amevaa tie Nyekundu namuona rais unapendeza. Anza ku observes tie za marais wa dunia ile siku wanakula viapo wanavaa tie za rangi gani?. Ukimuondoa rais Nyerere na Rais Mwinyi kwenye the official potrait photo, Nyerere alivaa suti ya Choe on lie na Mwinyi alivaa Kaunda Suit lakini angalia rangi ya tie ya rais kwenye the official potrait photo ya Mkapa, Kikwete na Magufuli!.

Hivyo tulipompata rais Mwanamke, angalia Hijab yake kwenye the official potrait.

Kufuatia mimi kuipenda sana rangi Nyekundu, hivyo kila nilimuona rais Samia amevaa Hijab Nyekundu namuona kama anapendeza sana na anatokelezea!.

Sasa inapptokea kuna hypothetical event mimi nimealikwa, kwenye mwaliko nikaona Mgeni rasmi ni Rais Samia, sasa ili Samia aje amependezea na ametokelezea nakamua kuchukua kalamu na kuandika kwenye mitandao ya jamii na kumshauri Rais Samia "Vaa gauni la Navy Blue na ile Hijab yako Nyukundu".

Kesho yake kwenye ile event ukamuona Rais Samia ameingia ukumbini huku amevalia Hijab Nyukundu! na nguo ya Navy Blue, kama ulivyoshauri, jee ungekuwa wewe utajisikiaje?.

Huko kwa Samia kuvaa Hijab Nyekundu, usikute Samia hakuona huo ushauri wako, wala hakuna mshauri wake yoyote alie uona ule ushauri wako kusema labda aliona hivyo kumshauri rais avae Hijab Nyekundu bali ni Rais Samia tuu yeye mwenyewe, bila kushauriwa na yeyote, amejivalia tuu mwenyewe Hijab yake na ikatokea tuu ni amejivalia ile Hijab Nyekundu!, hivyo ni imetokea tuu as a coincidence kuwa amevaa gauni la Blue na Hijab Nyekundu kama wewe ulivyo shauri, ila in real facts ule ushauri wako kuwa Samia avae Hijab Nyekundu, has got nothing to do with Samia kuvaa Hijab Nyekundu siku hiyo, it was just a coincidence tuu wewe umeshauri na hilo likatokea, but an amazing coincidence!.

Tena usikute hiyo siku ya tukio hilo, hata yule valet wake amemuandalia gauni jeusi na Hijab ya Manjano, ila ni Rais Samia mwenyewe ndie alimua kuvaa gauni la Blue na Hijab Nyukundu, lakini bado wewe lazima utafurahi!.

Sasa kwa vile hili ulishauri na sasa linakwenda kutekelezwa na kutimizwa, kuna ubaya ukimpongeza?.

Sasa unaposhauri kitu halafu kikatokea vile vile kama ulivyo shauri, hata kama ni just by a coincidence, an amazing coincidence, lazima urejee na kuonyesha appreciation.

Kwa watu wa kawaida a coincidence ni jambo la kawaida na linatokea kila siku, lakini kwa sisi ma deep thinkers, hakuna coincidence!, everything happens for a reason and it's a premeditated move!.

Haya mambo ya mimi kusema kitu ama kushauri kitu halafu kikaja kutokea kweli sikuanza leo
Hata ile 2014 niliposema Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli nilijisemea tuu lakini ikaja kutokea kweli coincidentally tuu!.
Kwa wapenzi wa kitu kiitwacho kauli umba karibuni mitaa hii "Ombeni Mtapewa", "Tafuteni Mtapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa" Je, Wajua Kuna "Kauli" na "Kauli Umba" Ambazo Huumba? Shuhudia

Hili la ushauri kwa Rais Samia kuhusu Katiba, kiukweli kabisa kama ni kelele, sio nimezipiga sana bali nimezivurumisha
Hivyo mtu unapopiga kelele kama hizi halafu mwisho wa siku something is going tu be done, ukiwa ni mtu wa shukrani na appreciation, ni lazima utashukuru na kupongeza hata kama aliyesababisha sio wewe ila na kelele zako zitakuwa zimechangia.

Hongera sana Rais Samia na Serikali yako kwa kuwa ni rais msikivu na serikali sikivu, mimi Paskali Mayalla kwa niaba yangu mwenyewe, na kwa niaba ya wale wengine wote wenye mapenzi mema na taifa letu ambao tumekuwa tukipiga kelele zisizoisha za kilio cha haki na katiba mpya, nasema "Asante sana kwa hili la katiba!", utabarikiwa na Tanzania Itabarikiwa sana.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
 
Back
Top Bottom