Waliochangia Ujenzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,922
30,271
MWINYIMBEGU ( MWINYI) DIBIBI si jina geni masikioni mwa watu wa Tanganyika ya kale na hususan wenyeji wa Upwa wa Pwani ya Tanganyika.

Huyu ni Babu yangu ambaye wanamwita kama ni uzao Mkuu ambaye alifanikisha kwa kushinda mapambano ya Uhuru wa Tanganyika katika ardhi ya asili yetu.

Miongoni mwa mambo makubwa ambayo yatabaki katika shajara ya kumbukumbu za Wazalendo wa Tanganyika kwa wakati huo ni mchango wake katika Taifa hili ambalo baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar sasa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Babu yangu, Mzalendo wa Kiafrika, MWINYIMBEGU DIBIBI ni miongoni mwa watu waliotoa mchango wa hali na mali katika kuanzisha hii leo kinaitwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (rejea tovuti ya chuo kikuu hapo chini)

Si wengi wenye shauku ya kufahamu waliotoa michango kusimamisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, lakini kwa wale wadadisi na wenye kukumbuka wema na hisani, lazima watataka kufahamu Wazalendo kama Babu yangu aliyetoa kiasi cha pesa taslimu na hii ilikuwa Mnamo mwaka 1958 wakati huo vuguvugu la Waafrika kutaka kuondoa Ukoloni na kujitawala wenyewe tutakavyo lilipamba moto.

Ari ya Waafrika wa Tanganyika kutaka kujitawala ilikuwa imemjaa kila mtu, kike, kiume, wa Mjini na Mashamba ilmuradi watu walichoka kutawaliwa na wageni.

Hakuwa babu yangu tu aliyechangia kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, bali kulikuwa na Wazalendo wengine 110 waliotoa mchango wa pesa taslimu.

Mwanafalsafa mmoja, Frederick Douglass aliwahi kusema kwamba " Elimu ni Ukombozi” kwa hakika, Wanamajumui hawa wa Kiafrika kutoka Tanganyika walifahamu ubora wa elimu na umuhimu wake katika kujenga jamii iliyoelimika ambayo wataitumia kama silaha na nyenzo katika kupambana na maisha yanayobadilika kila uchao huku wakikabili changamoto zinazohitokeza.

Kwa kutumia nyenzo ya elimu kama silaha ya kupambana na vikwazo vilivyowekwa na Wakoloni, Waafrika wakielimika katika elimu bora ingewasaidia kufikia malengo na ahadi zao katika kuondoa vizuizi vilivyowekwa na mfumo wa Ukoloni.

Babu yangu ni mmoja wa watu walionithamini sana kiasi cha kunishawishi na kunipa ari ya kipawa changu kutafuta elimu na taaluma ya ujuzi na kuweza kuwasaidia na wengine ambao wanahitaji maarifa na weledi wetu.

Jina lake limeorodheshwa katika tovuti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akipewa nambari 96.

Kwa hakika kila aliyetenda wema katika mgongo wa dunia anahitaji jazaa njema, nami nachukua fursa hii kuweka kumbukumbu hii ya Babu yangu iwe rejea kwa wale wataopenda kufanya utafiti juu ya historia ya kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mwisho.
 
Mavi ya kale hayanuki. Unataka ujiko wa babu yako. Je wewe umechangia nini kwa taifa? Najua umesoma na kutoa mchango mkubwa kiakili. Hivyo, ningeshauri uachane na mchango wa babu yako.

Badala yake durusu mchango wako. Alichofanya babu yako ni kitu chema na namuombea thwawabu lukuki apate ahera. Sina ugomvi nawe kujivunia mchango wa babu yako. Ila tabia hii imewadhoofisha wengi kiakili na kimaendeleo.

Najua watoto wengi wa Kipata na mitaa mingine waliorithi majumba walioshindwa hata kusoma kwa vile baba zao walikuwa wenye nyumba. Mwisho wa siku waliuza nyumba zile ima kwa magabacholi au wale waliokuwa wapangaji wao.

Ukiwaona watoto wa wenye nyumba wa zama zile kama vile akina Matimbwa, Litera na wengine, wako hoi wakati wale ambao hawakuwa na hata mkokoteni lakini shida zikafanya wawasomeshe watoto wao. watoto wao sasa wanawatumikisha wale walioleewa sifa za wazazi wao.
 
Mavi ya kale hayanuki. Unataka ujiko wa babu yako. Je wewe umechangia nini kwa taifa? Najua umesoma na kutoa mchango mkubwa kiakili...
Father...
Mzee Mwinyimbegu ni babu yake Ahmed Dibibi na nduguze wengi.

Wakipenda watakujibu.

Kilichofanya mimi kuweka makala hayo hapa ni ule umuhimu wa historia hii katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nimepitia majina ya wachangiaji wa Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam yaliyoko katika kitabu cha Abdul Sykes na katika Maktaba kujua historia zao katika TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika:

Mchangiaji No. 3 ni Julius Nyerere.
Historia ya Mwalimu Nyerere haihitaji kuelezwa hapa ni maarufu sana.

Mchangiaji No. 15 ni Abbas Sykes.
Historia ya Balozi Abbas Sykes halikadhalika ni maarufu pia haihitaji kuelezwa.

Nyerere na Abbas Sykes wamejuana 1952 Mwalimu alipofika kwao kuonana na kaka yake Abdul Sykes aliyekuwa wakati ule Secretary na Act. President wa TAA.

Mchangiaji No. 16 ni Makata Mwinyi Mtwana.

Huyu hafahamiki lakini alitoa mchango mkubwa katika TANU.

1685593410005.jpeg


Makata Mwinyi Mtwana ni huyo kushoto tajiri mkubwa Tanga miaka hiyo ya 1950s.

Kulia ni Rashid Makoko mwanachama shupavu wa TANU na ubavuni kwake ni mwanae Rashid Mamboleo Makoko.

Wanaoangalia kamera kulia ni Sadik Patwa alikuwa Muhindi tajiri mwenye kiwanda cha kutengeneza soda na kulia kwake ni Julius Nyerere.
 
Back
Top Bottom