Huu uzi hauna ukweli kiasi fulani,japo mgomo wa walimu upo lakini siyo wa siku tano wala kwa tarehe ambazo mleta mada ametutajia. Hili suala la mgomo wa walimu nimelifuatilia kwa kiasi kikubwa tu na ni kwamba CWT imetangaza mgogoro na serikali tangu tar-8/6 na kwa taratibu za sheria waalimu hawataweza kugoma mpaka kipindi cha siku 30 za mgogoro kipite na kama serikali(mwajiri) atakuwa bado hajatimiza madai ya wafanyakazi(walimu) ndipo mgomo unaweza kutangazwa. kipindi cha mgogoro kati ya serikali na walimu kitaisha tar- 7/7/2012, baada ya hapo ndo mgomo usiokuwa na kikomo na wala siyo wa siku tano na unaweza kuanza tar 8/7 kadiri utakavyo amuliwa mapema na baraza kuu la CWT. Tusipotoshe tafahdal!