Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundu mh jenister mhagama amewataka walimu wote wanaosubiri kuajiriwa naserikali kuwa wazalendo na nchi yao kwa kukubali kupangiwa sehemu yeyote. Akifunga rasmi mafunzo ya kijeshi yaliyochukua takribani miezi mi3 na nusu waziri huyo amesema walimu wengi hawataki kufanya kazi sehemu za vijijini hivyo kusababisha shule za vijijini kukosa walimu wa kutosha. Waziri huyo alienda mbali zaidi na kusema walimu tarajali wanatakiwa kuwa na uzalendo kwa kukubali kufanya kazi popote watakapopangiwa na serikali..
CHANZO radio kiss fm
CHANZO radio kiss fm