Walimu ajira mpya ngazi ya msingi hawajalipwa hela ya kujikimu tangu mwezi Julai

bumilo

JF-Expert Member
Mar 1, 2014
340
170
Hii ipo katika Halmashauri ya wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza. Sijui wamesahaulika au muda haujafika. Kumbuka hao ni binadamu na wana mahitaji yao binafsi na ya familia zao na wanalitumikia Taifa kihalali na kwa haki kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma. Sielewi tatizo lipo wapi.

Kumtumikisha mtu kufanya kazi na mafao yake hayapo hii si haki na si halali hata kidogo. Utu wa mtu uzingatiwe na sheria za utumishi wa umma zifuatwe na kutekelezwa ili walipwe fedha zao za kujikimu na pia walipwe mishahara yao kwani tangu Julai hadi Septemba hii wana haki ya kupata stahili/stahiki zao
 
Nchi hii inaviongoz wa ajabu kweli maswala ya msingi haya pewi kipaumbele.
 
Ngoja tumalize hiizi chaguzi tulikonunua viongozi kwanza
 
Hata kilombelo hawajapewa ya kujikimu na mshahara hakuna.NCHI YA KIS3NG3 HII
Why this my motherland? Mtumishi wa umma una dhambi gani mpaka umesahaulika kiasi hiki? Amka wewe uliyelala
 
Kuna teacher analia hapa anahitaji msaada...

Serikali mnawatengenezea saikolojia hasi walimu watandike wanafunzi viboko hadi kufa.
 
Kuna teacher analia hapa anahitaji msaada...

Serikali mnawatengenezea saikolojia hasi walimu watandike wanafunzi viboko hadi kufa.
I'm sorry to say this my dear JF member, sipo katika kada hiyo but si haki kumwona mtumishi anayeitumikia nchi kihalali akiishi maisha ya kuhangaika kiasi hiki. This is only in my motherland
 
Ma-PhD holder hawana muda huo. Tushamaliza Monduli na Ukonga tunatafuta uchaguzi mwingine hapo December au January. Tuvuliane tu.
 
I'm sorry to say this my dear JF member, sipo katika kada hiyo but si haki kumwona mtumishi anayeitumikia nchi kihalali akiishi maisha ya kuhangaika kiasi hiki. This is only in my motherland
Sorry pia nimeshindwa kuweka message yangu vizuri,kuna mwalimu alikuwa anaomba msaada wa kiasi cha mlo wa leo hali mbaya yuko mbali..

Sikumaanisha wewe...
 
Back
Top Bottom