KERO Ajira mpya Afya Halmashauri ya Rombo hatujalipwa fedha za kujikimu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sisi Watumishi wa Serikali ajira mpya ambao tulijiriwa mwezi wa Agosti, 2023 katika Sekta ya Afya, tunachangamoto ya kutolipwa pesa ya kujikimu tangu tulipo ajiriwa na kila tukifatilia tunapewa majibu yasiyoridhisha.

Sisi tupo Rombo Mkoani Kilimanjaro, tulipoajiriwa hatukulipwa fedha ya mshahara wala ya kujikimu kwa mwezi huo wa nane, mshahara tukaanzia kulipwa Septemba 2023.

Tangu wakati huo tulipokuwa tunaulizia tukawa tunajulishwa kuwa kuna changamoto ya mfumo, lakini tunakumbuka kwenzetu walioajiriwa Juni 2023 nao pia walipata chngamoto ya kutolipwa kama sisi, ni hadi waliporipoti kupitia Jamii Forums ndipo wakalipwa.

Tulipofuatilia Halmashauri nyingine mfano Wilaya ya Mwanga ambao waliingia katika ajira kama sisi wo wameshalipwa, pia kuna taarifa ambazo si rasmi kuwa fedha zimeshafika kutok TAMISEMI lakini ugumu upo kwenye Halmashauri.

Tunaomba msaada ujumbe huu ufike Serikali kuu kwa kuwa inaonekana wao wameshatoa ila tatizo ni huku kwenye Halmashauri yetu.

Tulipoulizia kwa wenzetu wa mikoa tofauti imeonekana wapo waliolipwa na wapo ambao hawajalipwa pia.


Pia soma - Walimu tulioajiriwa mwaka 2019 Ruangwa, Lindi, hatujalipwa pesa zetu za kujikimu hadi sasa
 
Tulia ndugu mutalipwa.
Huko local government pesa ya mwaka huu unaweza kulipwa hata miaka 7 mbele, huko guarantee ni mshahara tu.
 
Back
Top Bottom