Wali Special Thread: Jifunze jinsi ya kupika mapishi mbalimbali ya wali

MAPISHI YA MWAMBAO VYAKULA VIKUU

bshhh.jpg

WALI WA ASUMINI

Mchele kilo 1

Kuku mkubwa 1

Vitunguu maji kilo 2

Mayai 8

Samli kilo 1

Thomu gram 200

Tangawizi mbichi gram 50

Mdalasini gram 50

Hiliki gram 50

Bizari nzima kiasi

Siki kiasi

Mtindi painti 1

Tungule kilo 1

Zabibu nyeusi kiasi

1 Mkate kuku umwoshe umchemshe kwa maji na chumvi mpaka awive, kisha muepue.

2 Menya vitunguu uvioshe uvikate na uvigawe sehemu mbili. Sehemu moja uiweke, sehemu ya pili vikaange mpaka viwe vyekundu kama vya biriani. Kisha vichuje uitoe samli yote, vitie katika sinia uvitandaze ili vipoe kwa kupata upepo.

3 Chukua mdalasini, hiliki na bizari utwange pamoja, kisha uchunge unga laini. Saga thomu na tangawizi mbichi. Saga tungule.

4 Teleka sufuria tia samli ile ile iliyokaangiwa vitunguu halafu utie vile vitunguu vilivyobakia uvikaange. Vikianza kuiva tia viungo ulivyovitwanga na kuvisaga. (Bakisha vitunguu na viungo kidogo). Tia vipande vya kuku, mtindi siki na supu ya kuku iliyobakia katika sufuria. Acha ichemke nyama pamoja na vitu vyote mpaka libaki rojorojo.

5 Teleka maji, yakichemka tia chele. Ukiiva utoe uchuje yatoke maji yote.

6 Teleka tena sufuria utie samli kidogo utie na vile vitunguu ulivyovibakisha uvikaange. Tia mdalasini nzima, kaanga pamoja, tia na ule wali ukoroge koroge ili uchanganyike na viungo. Kisha ufunike upalie moto.

7 Chemsha mayai yote uyamenye.

8 Wali ukishakauka utaupakua, lakini lazima itabidi utumie kombe au sahani kubwa itakayoweza kuingia wali pamoja na vitu vyote. Kuupakua kwake kwanza utatia nusu ya wali katika hiyo sahani, baadae utatia masalo na nyama yote, na mayai, kisha utayafunika masalo kwa wali uliobakia. Mwisho utachukua vile vitunguu ulivyovikaanga na ukavitandaza ili vipo, utavimwaga juu ya wali.Kwani ni kwa sababu ya hivi vitunguu ndio maana ukaitwa wali wa asumini. Ukipenda utapamba chembe za zabibu juu yake. ZABIBU HIZO Ziroweke kwanza ili zivimbe.
 
mimi nimeanza kujipikia mwenyewe hapa, ila nikipika wali sijui nakosea kipimo cha maji au vip ila wali unakua rojo sana, na unakua sio mzuri
pia napenda kujuzwa ni namna gani unapika wali halafu unachanganya na nyanya, karoti n.k huko huko kisha baadae unaandaa mboga nyingine
thanks
 
Kupika wali ni rahisi sana.

Na ni vyema, kama unajifunza kuupika basi usitumie rice cooker.

Kwa jinsi ya maelezo yako, inavyoelekea unaweka maji mengi mno.

Ukitaka upike utokee usio rojorojo [mkavu kwa kiasi flani na usioshikamana] basi ni vyema kwanza ukatumia mchele ulio bora.

Mimi napenda kutumia Mahatma Jasmine rice kama huu kwenye picha:
jasmine.jpg

Namna ya kupika kwa kutumia sufuria dogo na jiko la umeme [samahani, sijawahi kutumia jiko la mkaa wala mafuta kwa hiyo nitakupa maelezo ya kupikia kupitia jiko la umeme.], ni kama ifuatavyo:

- Pima mchele kwenye kikombe kimoja cha chai.

- Kwa kutumia saizi ya hichohicho kikombe, weka vikombe viwili vya maji kwenye sufuria lako.

- Chemsha hayo maji mpaka yachemke kabisa. Yakishachemka weka mafuta au siagi.

- Ukishaweka mafuta au siagi, weka sasa huo mchele kwenye hilo sufuria.

- Koroga kidogo halafu punguza kiasi cha moto [katikati ya low na medium]; ukishapunguza moto funika sufuria yako.

- Baada ya dakika 10 hivi funua mfuniko halafu koroga tena [na mwiko] mchele wako; punguza tena moto mpaka kwenye
'low' halafu rudisha mfuniko kwenye sufuria.

- Baada ya dakika tano, sita, au nane hivi funua tena mfuniko uuangalie wali wako uko kwenye hali gani. Kama maji yashakauka basi zima moto halafu rudishia tena mfuniko.

- Funika kwa kama dakika tano au saba hivi na baada ya hapo wali wako utakuwa uko tayari kuliwa.

NB: Haya maelezo ni yale ya msingi tu katika kupika wali mzuri usio rojorojo. Ni wajibu wako pia kutazama kwa macho yako hicho unachokipika na ikiwezekana kuongeza au kupunguza vitu kadha wa kadha , basi fanya hivyo.
 
Kumbe trainer unajua kupika ehh?
step zako zote nazifuata ila sikorogi ama kugeuza mpaka maji yakauke. Mtoa mada ningemshauri atafute sufuria yenye mfuniko wake mzuri inayotunza mvuke pia.

Angalizo, huwezi kuweka nyanya kwenye wali. Kuongeza ladha unaweza kuweka viungo/spices, carrot ama sausage zilizokatwa ndogo ndogo.

Trick nyingine inayosaidia wali usidode ni kukaanga mchele. Osha mchele (wowote ule kuosha inaondoa kiasi cha wanga na vumbi, sijui ni obsession tu ya usafi pia?). Hiyo siagi ama mafuta weka kwa sufuria, ikishapata moto kabisa weka mchele na kaanga kidogo kama dk 3. Weka maji na umalizie kwa steps alizoelezea Nyani Ngabu
 
Mimi tena?

I am so versatile you wouldn't believe it.

Nadhani kinachonifanya niwe hivyo ni kupenda challenges. I like to challenge myself and actually do enjoy it.

Leo yenyewe tu hapa tumepika wali nyama, maharage ya nazi, na kabichi!

Halafu sasa, nilivyo mthubutu wakati mwingine [kama leo] huwa naweka bbq sauce kwenye nyama ili kuipa hint ya utamu [sweetness]. Huwa naweka kidogo tu lakini.

Hii ndo niliyoitumia leo
NF1241652L.jpg
 
Shkamoo yako boss hahaha.
Mie napenda sana spicing. Bbq sauce nawekaga tu. Nilipata life lessons ya ku-stick to the type siku niliweka pork spices kwenye kuku haikufaa kula.

Nilitaka kutaja nazi kwa mtoa mada nikaogopa kumvuruga. Jana nilialikwa lunch nikajifunza upishi mpya wa maini nikafurahi sana.

Appreciated
 
Huwa natumia ratio ya 2:3 yaani mchele vikombe 2 na maji vikombe 3.

Huwa nakaanga mchele kwenye sufuria, wakati huo huo nachemsha maji pembeni kwenye kettle.

Mchele naukaanga ukianza kuwa Brown napunguza Moto Na kumimina vikombe vi 3 vya maji.

Mi hutumia gas kwa hiyo napunguza Moto hadi kipimo cha mwisho.

Unafunika kwa DK 10 wali unakuwa umeiva.
 
nina uzoefu wa kupika wali ,na uzuri nimekulia sehemu ambayo wali ni chakula kikuu,pia napenda kupika.
Kwa kuongezea tu njia nyingine ya kufanya wali usiwe rojo ni kwamba maji yaliyochemka ukiweka mchele ,maji yauzidi mchele kama kwa nchi moja na nusu, ni bora ukatenga maji ya moto pembeni ili kama utakuwa mkavu zaidi baadae utaongeza maji kidogo,epuka kuongeza maji ya baridi.kuhusu moto kwa kila hatua hapo juu wameelezea vyema
 
Shkamoo yako boss hahaha.
Mie napenda sana spicing. Bbq sauce nawekaga tu. Nilipata life lessons ya ku-stick to the type siku niliweka pork spices kwenye kuku haikufaa kula.

Nilitaka kutaja nazi kwa mtoa mada nikaogopa kumvuruga. Jana nilialikwa lunch nikajifunza upishi mpya wa maini nikafurahi sana.
King'ast nipe huo upishi mpya wa maini.
 
Kupika wali ni rahisi sana.

Na ni vyema, kama unajifunza kuupika basi usitumie rice cooker.

Kwa jinsi ya maelezo yako, inavyoelekea unaweka maji mengi mno.

Ukitaka upike utokee usio rojorojo [mkavu kwa kiasi flani na usioshikamana] basi ni vyema kwanza ukatumia mchele ulio bora.

Mimi napenda kutumia Mahatma Jasmine rice kama huu kwenye picha:
jasmine.jpg

Namna ya kupika kwa kutumia sufuria dogo na jiko la umeme [samahani, sijawahi kutumia jiko la mkaa wala mafuta kwa hiyo nitakupa maelezo ya kupikia kupitia jiko la umeme.], ni kama ifuatavyo:

- Pima mchele kwenye kikombe kimoja cha chai.

- Kwa kutumia saizi ya hichohicho kikombe, weka vikombe viwili vya maji kwenye sufuria lako.

- Chemsha hayo maji mpaka yachemke kabisa. Yakishachemka weka mafuta au siagi.

- Ukishaweka mafuta au siagi, weka sasa huo mchele kwenye hilo sufuria.

- Koroga kidogo halafu punguza kiasi cha moto [katikati ya low na medium]; ukishapunguza moto funika sufuria yako.

- Baada ya dakika 10 hivi funua mfuniko halafu koroga tena [na mwiko] mchele wako; punguza tena moto mpaka kwenye
'low' halafu rudisha mfuniko kwenye sufuria.

- Baada ya dakika tano, sita, au nane hivi funua tena mfuniko uuangalie wali wako uko kwenye hali gani. Kama maji yashakauka basi zima moto halafu rudishia tena mfuniko.

- Funika kwa kama dakika tano au saba hivi na baada ya hapo wali wako utakuwa uko tayari kuliwa.

NB: Haya maelezo ni yale ya msingi tu katika kupika wali mzuri usio rojorojo. Ni wajibu wako pia kutazama kwa macho yako hicho unachokipika na ikiwezekana kuongeza au kupunguza vitu kadha wa kadha , basi fanya hivyo.
Ahsante sana, ila Umesahau chumvi :p
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom