Haya wale mabachela na wale wasiojua kupika wali mweupe

cold water

Senior Member
Oct 6, 2021
174
618
Mahitaji: mchele, maji, chumvi,mafuta bila kusahau moto wako wa gesi, mkaa,au kuni etc.hatua ya kwanza washa moto wako, kisha injika sufuria lako jikoni,unapoinjika tu akikisha mchele wako nao upo kwenye maji mambo ya kusema mnapika wali bila kuloweka mchele, ndo mana unatoka unatafunika, na wengine hawaoshi,usipoosha wali hautang'aa utakuwa wa brown hauwi mweupe.lakini sio lazima kuloweka kwenye maji unaweza tumia njia ya kuuosha na kuweka kwenye ungo bila kuweka kwenye maji.

Kama unapikia mkaa hadi sufuria ichemke mchele utakuwa ushaloana kwenye ungo,kama unapikia gesi basi loweka kwanza kabla ujaweka sufuria lako jikoni,after there kama Mchele umeloana, na sufuria lako linachemka basi hakikisha maji yanaendana na Michele sio unatia maji kibao mchele kidogo lazima utoke ubwabwa.Mimi sufuria likichemka huwa sianzi kutia mafuta.

Natia kwani Mchele na chumvi nakoroga naonja chumvi kama chumvi nyingi namwaga maji natia mengine ambayo hayana chumvi mpaka chumvi inirizishe ndipo naweka mafuta ,naangalia kipimo cha maji baada ya kukoroga nikishaweka mafuta.

Mchele niuone kwa mbali ndani ya maji sio umetia mchele kwenye maji uloinjika umekoroga ata kwa macho huuoni mchele uloutia, lazima utoke ubwabwa .na sitii mafuta kabisa kwasababu nikiona maji ni mengi napunguza, kuliko kutumia ile njia ya kutia maji na mafuta kwa wakati mmoja ukiona maji mengi ukipunguza mafuta unayaaribu maana utapunguza maji na mafuta uloweka,kingine zingatia mafuta unapopika wali acha kunyima mafuta kama unapika kande,wali hautang'aa na haunogi,na hauvutii!!!


Hakikisha wali wako ukishaiva haupati crachi yani kutafunika.anyways maneno yamekuwa mengi yasikuvuruge,baada ya kuangalia kipimo cha maji na mchele kwa macho basi funika sufuria lako bila kukoroga, koroga hadi maji yakakamie baada ya hapo kama unapikia mkaa palia moto juu na upunguze chini, chini weka kidogo sana ushawahi pika wali ukiipua sufuria chini hakuna ukoko kabisa ile inatokana na kutia mafuta ya kutosha na kuzingatia moto wa chini na juu usiweke moto mkali utasababisha ile layer ya juu kuwa ukoko.

Aisee inabidi siku nikipika nitume vidio kuandika kazi sana mtu kukuelewa fani za watu izi za uandishi wa habari.ha ha ha ha
 
Kuna kiumbe humu akijui kutoa wali kweli hawa watoto wa tusiime a st Mary's wa kazi sana
 
Formula ya kupika Wali kwa wasiojua kabisa

Pima kiasi cha mchele unataka kupika
Mfano, vikombe vitatu vya mchele, basi na maji pima vikombe vya maji vitatu kwenye sufuria la kupikia

Osha mchele wako vikombe vitatu wakati huo maji vikombe vitatu yakiwa jikoni ili yachemke


Yakichemka weka chumvi na mafuta kwa matakwa yako
Kisha weka mchele wako kwenye maji yaliochemka

Kama utakua umepima tatu kwa tatu basi mchele wote utazama na maji yatabakia kwa juu

Acha mchele uchemke hadi maji ya juu yakiisha na kubaki level moja na mchele
Hapo sasa punguza kabisa moto ubaki kiidogo
Kama ni mkaa ubakie kwa mbali kama ni gesi punguza hadi unakaribia kuisha

Funika sufuria vizuri kabisa kuhakikisha mvuke mwingi inabaki ndani
Baada ya dk 5 hadi 10 ubwabwa wako utakua tayari
Ugeuze na onja, kama unona bado kidogo unaendelea kuuacha kwa kuufunika

Mchele unaiva vizuri kwa mvuke na sio maji la sivyo utakua bokoboko

Focus kwenye kupunguza moto na kufunika vizuri (ndio maana rice cooker is the best)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom