Wale mnaosubiri kwa hamu Makonda atumbuliwe, mtasubiri sana!. Ukiwa ni mpakwa mafuta, ni mpakwa mafuta!

Navyomuelewa Rais Magufuli amekuwa ni Rais wa kuchukua hatua mara anapoona kunajambo asiloridhishwa nalo hasa katika utumishi wa wateule wake. Aliwahi kumwondoa RC wa Tabora Mama Malechela kisa tu kusema uongo kuwa hakuwa na watumishi hewa. Japo huyu mama alisema kutokana na taarifa aliyokuwa amepewa. Bado Rais akamtumbua alie kuwa rafiki yake wa Karibu Mhe. Kitwanga kwa kuingia bungeni kalewa. Na wengi wengineo aliwatumbuwa papo kwa hapo mfano Marehemu Kabwe.
Sasa Huyu RC Makonda anakashifa mbaya ya kukwepa kodi. Kwanza alikana makotena si yake. Baadae huyo huyo akajitokeza na kudai makotena ni kwa ajili ya shule za Dar. Huyo huyo akasema ole wao wanayo yazuia atawashitaki kwa Rais. Wakati huu wote Rais alikuwa kimya hakusema chochote. Msimamo wa Waziri wa Fedha nampongeza ndiyo umesaidia pamoja na Commissioner wa forodha. Baada ya mnada wa kwanza RC Makonda akajitokeza tena kanisani akidai kuwapa laana wale wote watakao nunua hiyo thamani kwa kulaani wao na vizazi vyao. Kwa maana hiyo hata akiwa ni nduguye kanunua laana itamfika yeye na uzao wake. Hapa nilijiuliza kama Mungu anaejua kutenda haki iweje huyu mtu anaekwepa kodi na kudanganya Taifa kuwa thamni ni za shule anajiapiza na kulaani wale watu watakao jitokeza kukomboa kodi hiyo kwa kununua thamani hizo.
Rais Magufuli alijitokeza baada ya waziri wa fedha kuwa ameonesha msimamo. Rais kwa sauti ya kubembeleza aliongea kuwa RC Makonda alipe kodi. Hivi mheshimiwa Rais, wewe mwenyewe umekiri thamani hizo ni ulaghai unatumika si za mashule bali kuna mkono wa wafanya biashara. Hapa Makonda kadanganya ili akwepe kodi. Je kwanini usimchukulie hatua mteule wako kama wengine?
Mhe. Rais Makonda kesha onesha hana mpango wa kulipa kodi na katoa laana kwa atakaye yanunua, hivyo katishia umma kwa imani yake, na kutaka kuzuia serikali isijipatiae mapato yake kwa hiyo kauli, je Mhe. Rais bado huoni ili ni kosa kuzuia mnada au kutaka kuuvuruga? Mbona DR. Luis Shika alikamatwa kwa kuvuruga mnada japo yeye alishiriki mnada?
Mhe. Rais wetu! Makonda ni nani katika nchi hii hata wewe unamuogopa? Mhe. Rais ulithubutu kumwambia Waziri mkuu kwenye swala la Korosho kuwa nae ungemtimua na kupiga hata mashangazi zake. Mbona kwa makonda ambapo ni swala la kodi unambembeleza? Ujatishia kupiga hata wajomba zake huko usukumani?
Mhe. Rais mimi napenda juhudi zako unazofanya, na hatua kadhaa kujenga uchumi wa nchi. Kwanini unakuwa na kiongozi anae onesha picha mbaya kwa jamii tena kwa majivuno bado unamshikilia. Hata ulivyomkemea! Mhe. rais haikuwa katika sauti yako niliyoizoea unapokemea maovu. Uliongea kwa unyonge na kwa kumbembeleza alipe kodi. Si mbaya ila Mhe. Rais napenda kujua Makonda ni nani? Kwa Dc Hapi ulisema ulitamani hata utengeue uteuzi kisa Wilaya yake kushuka katika mapato. Mbona kwa Makonda ujasema ungetamani kufanya nini? Mhe. Rais wetu, watu wanakupenda ila kiukweli hili la Makonda linaleta ukakasi! Si kwamba namchukia Makonda hapana. Bado unaweza mpa uteuzi mwingine utaoona unafaa; kama unaona hatakoswa kuendesha maisha yake bado ni kijana mpeleke Monduli TMA apate mafunzo hata anaweza kwenda kulinda amani huko DRC Congo.
Mwl. Nyerere alikuwa akiondoa au kutumbua kiongozi anapozalilisha familia binafsi, alipenda kiongozi kuwa na maadili katika jamii. Sasa Mhe. Rais wewe upangiwi au kushauriwa ulichukua fomu mwenyewe japo ukumbuke wananchi ndo walikupa ridhaa hiyo ukujipa mwenyewe, hivyo una wajibu wa kuwatumikia na kuwasikiliza. Usiwe na maamuzi ya kutaka kuwa komoa wapinzani wako kisa hutaki ionekane umefanya wanayotaka. Hekima na Busara zitumike zaidi kuliko kuoneshana nguvu na ubabe. Kuna mtumishi mmoja alisema Rais kama utaendelea kumkumbatia RC Makonda ipo siku atakuaibisha atafanya mambo ya ajabu. Naanza kuona dalili hizo! Nawe Mhe. Rais wangu endelea kumkumbatia ipo siku utajutia nafsi ya huyu mwana wa pekee! Mhe. Rais najua hutonijibu humu ila natarajia kuona majibu yako kwa matendo nini kitafuata baada ya mtumishi wa umma na mteule wa Rais kukwepa kodi makusudi kwa kutumia ulaghai. Je Mamlaka ya uteuzi itafanya nini?
 
Mtoa mada una kichwa cha panzi na unatakiwa kukumbushwa kubakiza akiba ya maneno, uchafu unaorusha kwa Makonda wewe mwenyewe utakuja kuusafisha. Kumbuka ya Lowasa.

Siku Makonda akihamia chadema atapata mapokezi makubwa
na kusafishwa kwa kila aina ya Omo na kubatizwa mleta mabadiliko wa Ufipa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi,

Wengi wetu humu jf, ni watu wa matukio, yaani wanajikita zaidi katika tukio, kilichotokea, lakini wale wasoma trends humu ni wachache, mimi ni mmoja wao. Trends ni the motive behind, the causative agents na the underlying facts. Likitokea tukio, hatujiulizi kuhusu ni nini kilichotokea kwenye tukio fulani, bali tunakwenda mbali zaidi kwa kujiuliza kilichosababisha tukio hilo kutokea, the underlying facts na causative agents, na kumalizia na the motive behind.

Hivyo jana baada ya Rais Magufuli, kuyasema aliyoyasema kumhusu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, na ukwepaji kodi wa Makontena, kuna wengi ambao ni watu wa matukio, sasa wanasubiri kwa hamu na shauku kubwa kusikia Makonda ametumbuliwa!, Makonda hatatumbuliwa kwa sababu...

Wale wote wenye kusibiri hilo litokee, kiukweli kabisa, watasubiri sana!.
Sababu pekee halisi itakayofanya Makonda asitumbuliwe sitaitaja hapa, ila nakuwekea tuu uthibitisho kuwa Makonda ni mpakwa mafuta. Ukiwa ni mpakwa mafuta, then wewe ni mpakwa mafuta tuu, no matter what, hivyo haya yote yanayoendelea sasa kuhusu sakata la makontena ya Makonda, ni mapito tuu, hiyo kodi italipwa na maisha yataendelea.

Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe Walilolikataa Waashi Litafanywa Kuwa Jiwe Kuu la Pembeni - JamiiForums

P.
Kodi ndio jambo la msingi na muhimu katika sakata hili. Kodi ikilipwa hili jambo litatoweka vinywani mwa watu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom