Bado kuna ubishi kuwa hiki ni chuma? Je, chuma hiki ni chuma kingine ila ni kama kile au chuma hiki ni kile kile kimerejea kivingine?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,507
113,629
Wanabodi,

Kama kawa kila nipatapo fursa, huja na makala za Kwa Maslahi ya Taifa, leo ni swali tuu kuhusu hiki Chuma kipya.

Baada ya mtu kupelekewa moto na akaachia ngazi mwenyewe, bado kuna ubishi kuwa hili ingizo jipya ni chuma cha ukweli kama chuma cha Mjerumani?. Je chuma hiki ni chuma kipya kingine ila ni kinafana tuu kama kile chuma au chuma hiki ni chuma kile kile kimerejea kivingine?!

Hili ni bandiko la dhana tuu ya kufikirika, yaani an hypothetical situation ya just thinking aloud by imaginations, hiki chuma ni cha moto!. Kwa wale walionisoma hapa Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze... wakanielewa, wakilisoma bandiko hili watanielewa!, lakini kwa wasio elewa someni tuu na maisha yaendelee!

Naomba nianze na hadithi hii fupi.
Japo Mungu ni mmoja na ndie aliyeumba ulimwengu na kila kilichomo!,
Ila wakati anaamua kumuumba binadamu, kuna viumbe Mungu alisemezana navyo " Na tuumbe binadamu kwa mfano wetu" hii maana yake japo Muumba ni Mungu, lakini kuna viumbe alisemezana navyo viwe ni Mwana, yaani Neno, Roho Mtakatifu na malaika, hivyo God was not alone!.

Na baada ya binadamu kumuasi Mungu kwa kutenda ile dhambi ya kumega lile tunda la mti wa katikati, Mungu alikasirika akawafukuza Adam na Hawa kutoka bustanini, ila licha ya kuwatimua, aliwaaahidi hata waacha atawatumia Mkombozi.

Huko mbinguni, inasemekana Mungu aliwauliza hao aliokuwa nao, nimtume nani aende kuookoa ulimwengu?. Ndipo Neno akajibu, "unitumie mimi Bwana". Ndipo Mungu akamtoa mwanawe mpenzi na kumtuma duniani kuja kuukomboa ulimwengu, akazaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, kwake yeye Bikira Maria, akawa mwanadamu. Akasulubiwa na kuteswa kwa mamlaka ya Ponsio Pilato, akafa akazikwa, siku ya tatu, akafufuka, akapaa mbinguni, toka huko atakuja kuwahukumu wazima na wafu, na ufalme wake hautakuwa na mwisho!.
Ikumbukwe Masiha alikuja kwa ajili ya taifa la Mungu, ila alikataliwa na wale aliokuja kuwakomboa na wakamsulubisha!, ila ni kwa kuteswa kwake na kwa kupigwa kwake, sisi tumeponywa!

Hivyo ndivyo Taifa letu la Tanzania lilivyo, ni taifa la Mungu. Mungu akatuletea mkombozi Nyerere, akamtwaa kabla ya kutufikisha nchi ya ahadi.

Taifa likayumbayumba, hapa katikati kwa kufanywa kichwa cha Mwendawazimu huku kiuchumi tukifanywa ni shamba la bibi!, tukamlilia Mungu atuletee mkombozi mwingine, Baba Mungu akakisikia kilio chetu akatuletea Magufuli. Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania ilihitaji Dikiteta, tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Chuma hiki kiliinyoisha nchi!, na nchi ikaanza kunyooka, vyuma vilikaza watu wakaanza kupiga mayowe, na kama ilivyo kwa manabii wengine Ama kweli nabii hakubaliki nyumbani. Je, Magufuli ni nabii? Tanzania wanambeza, Afrika wanamlilia! Tanzania yapigiwa mfano Magufuli awe Rais wa Afrika, kelele zilipozidi, mwishowe Mungu akamtwaa na kumchukua kwake mbinguni, kabla ya kutufikisha nchi ya ahadi Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani.

Baada ya kumtwaa Magufuli, Mungu akatuletea Samia. Magufuli alikuwa chuma na alitawala taifa hili kwa mkono wa chuma, hivyo JPM alikuwa ni chuma!, ila Samia.

Tuambizaze ukweli, Rais Samia sio chuma kivile kwa uchuma wa Magufuli type, ila yeye naye ana uchuma wake kupitia jicho!. Rais Samia ana jicho hilo!, linaona kila mahali na kila pahala!. Sasa ili mambo yaende, hili taifa linahitaji chuma cha kulikimbiza mchaka mchaka!. Jicho la Mama Samia lika kispoti chuma fulani kikiwa kipo tuu!, Samia akakisajili chuma hiki na kukiita kumsaidia kule kwenye chama!, na kusema ukweli kilikuja moto, kwa mwendo wa mchamchaka, alianza kuwakimbiza kwa kuanza na kinara wao kwa kupewa ultimatum!, kisha mawaziri na watendaji wakaanza kuperekeshwa!

Mara yakaibuka mayowe kila kona!

Ndani ya CCM pia kuna baadhi ya makapi yalikuwa yamedanda, na kujishikiza kwa kujibananisha kama luba!, baada ya chuma kuingia baadhi ya makapi haya, yakapelekewa moto! yakaanza kuishiwa nguvu, yakaanza kushindwa na kulegea!, baadhi yao ndio hawa sasa wameanza kuachia ngazi mwenyewe kwa kutafuta visingizio!

Ni baada ya makapi haya kuanza kuachia ngazi, ndio sasa macho yangu yameanza kufunuka na kuona kwa hakika hakuna ubishi kuwa hiki ni chuma!. Swali ni, je chuma hiki ni chuma kingine ila ni kinafanana kama kile chuma, au chuma hiki ni chuma kilekile kimerejea kivingine?, ili kuja kuikamilisha kazi ya ukombozi mpya wa taifa letu!

Ili kujua kama hiki ni chuma kile kile au ni chuma kipya karibu mitaa hii Nikimwangalia Makonda, mambo anayoyafanya namuona kama Magufuli

CCM inazidi kuimarika, kupendwa na kukubalika, hadi makapi ya ndani ya chama, yameanza kujichuja yenyewe!!, si mnaona!

Na hapa ndio mwanzo tuu wa hizi amsha amsha!, kama ni mvua, hii ni rasha rasha tuu!, mvua halisi ni 2025!.

Ila pia kijana ni msikivu sana, alianza kwa moto sana, tukampooza Pongezi Paul Makonda kuifufua CCM kwa amsha amsha. Twende mdogomdogo ngoma ikivuma sana inakaribia kupasuka! sasa anakwenda vizuri!.

Na kwa vile humu umezuka mtindo ukimkubali mtu ukamsifia na kumpongeza, huchelewi kuitwa chawa!,
angalia huyu dogo sisi kaka zake, tumeanza nae wapi.

Mimi nilianza nae hapa Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
Nikaja hapa Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe walilolikataa Waashi litafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni.

Alipopitia misukosuko tukasimama nae kwanza kwa kutoa wito Ndugu, Jamaa na Marafiki, Njooni Tumtetee Makonda Dhidi ya Mapapa Wauza Unga Wanaomzushia... kisha tukamshauri Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho Dhidi ya Mafanikio Yake!. Makonda Wapuuze! .

Kuna watu wenye roho za kwanini tukawaambia Wale mnaosubiri kwa hamu Makonda atumbuliwe, mtasubiri sana!. Ukiwa ni mpakwa mafuta, ni mpakwa mafuta!

Na mwisho nikapendekeza Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM! Apunguze.

Hivyo wandugu, kama hiki chuma ni kile kile, then kaeni mkao wa mguu sawa!, 2025 mambo ni yale yale na vile vile!. Msije kusubiria mpaka 2025 mambo yakatokea kivile, watu ndio mkaanza kupiga kelele baada ya mambo kutokea, msije kusema hamkujua, tumewaambia mapema kabisa mkae mkijua chuma bado kipo!

Kiukweli kabisa kuna watu wana macho lakini hawaoni na wana masikio lakini hawasikii!

Nawatakia Ijumaa Kareem

Paskali.
 
Mkuu Pascal Mayalla

Jinsi unaona mambo ni kwa namna ya kipekee sana. Sina mashaka kabisa kuwa maoni haya ni kwa mujibu wa "classified data".

Walau sasa neno litatimia kwamba ...vipofu wanaona na viziwi wanasikia...

Shukrani sana kwa kutufumbua macho
Anaandaliwa hapo mbeleni ashike!!Lakini najiuliza 2025-2030 nani anasimama!!?

Tusubiri,labda majaliwa kwa muhula mmoja coz inaonekana ulinzinwake uliimarishwa!!

Sasa FDR vip!!?ataingiaje!!?

Haya!!!?
 
Wanabodi,

Kama kawa kila nipatapo fursa, leo ni swali tuu Baada ya ... Bado Kuna Ubishi Kuwa Hiki ni Chuma? Je Chuma hiki ni Chuma Kingine ila ni kama kile au Chuma Hiki ni Chu Kile Kile Kimerejea Kivingine?!



Paskali.
Kama Samia ana jicho kali kwann hakuviona hivyo vyuma mapema na badala yake akawaweka hao unaowaita makapi? Mwambie sasa hivi kwa kutaja majina ya makapi wengine waliobaki, au unasubiri kusifia baada ya kuona mabadiliko.?
 
Back
Top Bottom