Wakuu naumia sana, naombeni msaada wa ushauri

Dem ashajua huchomoi kwake ndo maana kasema poa maana anajua utarudi tu.
Dem akijua unaumia kwa ajili yake dadeki hamna rangi utaacha ona.

Pole mkuu bila shaka utateseka sana hapo kazini, na hivi unaumia ukimuona anaenjoy na vijeba wengine dadeki utasaga meno we jamaa kama nakuona unavolilia vyoo vya ofisi 😂😂.
 
Sheria yangu no.1

Sitoruhusu mahusiano ya aina yoyote mahali nafanyia kazi, hata huyo bint awe na uzuri wa aina gani

Pole ila ukifanikiwa kuachana nae itakua jambo jema sana,mapenzi kazini kiasi kikubwa huaribu kazi
 
Habari za sikukuu ya pasaka natumai wote ni wazima wangwana niende Moja Kwa moja kwenye mada ni kwamba hapa kazini Kuna dada mmoja tulitokea kupendana sana Sasa juzi tukapishana kauli nikatikisa kiberiti mwenzang kamwaga njiti kabisa nilikuw nampima tu kwamba tuachane akakubali Sasa nimeweka ngumu lakini naona kabisa nashindwa kibaya Kila saa namuona anavyo chat na majamaa wengine Wanacheka nn Kwa kweli nje navumilia lkn nachomeka mwenye mbinu yeyote anipe jaman ya kumpotezea unaye mpenda alaf mpo karibu ushauri pia kukosolewa naruhusu karibuni sana
Pole mkuu hii kitu namm kidogo nijichanganye kwa workmate, Mungu mkubwa niliepukana nayo,
 
Ni simple sana, badili mtindo wa kunyoa, badili marashi unayotumia, badili uvaaji wako. Alafu endelea na maisha mengine usihangaike na huyo dada tena.

wanawake wanagundua vitu vidogo vidogo haraka sana.

Kama ukitaka kuwa mtu wa propaganda kama muenezi, tafuta mdada ambae ni rafiki wa huyo dada muulize ukiwa serious akuambie pete nzuri ya uchumba au kagauni ka engagement. Alafu umwambie asimwambie huyo demu. Ila na wewe usimwambie unataka kumvalisha nani.

Komoaneni tu Mkuu, mpaka aokote hizo njiti alizomwaga 😂😂
 
Back
Top Bottom