Wakristo wanatoa sana kwa wachungaji kuzidi kwa wahitaji, Waislamu wanatoa sana kwa wahitaji kuzidi kwa mashehe

Makanisani wakristo wengi wakishatoa sadaka kanisani ndio shughuli imeishia hapo. Ni rahisi sana kuwakuta wachungaji mabilionea wanaotajirika kwa sadaka za waumini lakini kuna waumini wana changamoto zinazoweza kutatulika kwa milioni 10 ila wanaombewa badala ya kusaidiwa

Licha ya kwamba waislamu wengi ni maskini ukilinganisha na wakristo, Nimegundua waislamu hawatoi sana sadaka misikitini lakini huwa wanasaidia sana huku nje.

Nimewahi kupata shida ya maji na niliweza kuchota maji bure kabisa msikitini wiki nzima.

Niliwahi kufikia sehemu sina pa kulala nilienda kanisani nikiwa muumini wa kanisa tangu mtoto lakini nilikataliwa kabisa, sehemu iliyonitunza ni msikiti, kanisa waweza kukuta lina mabomba ya kutosha ila ni kwajili ya matumizi ya kikanisa tu.

Mwezi wa Ramadhani ule mwezi mzima ni kawaida sana kuwakuta waislam wanasaidia vyakula watu wenye shida.

Waumini wana magonjwa ambayo yanatibika kwa milioni 10 lakini wachungaji wenye account zinazosoma Bilioni wapo kujifanya wanawaombea, Kweli? Haya kama sio maombi ya kinafki tuyaitaje?

Pamoja na mazuri haya kilichonitatiza kuhamia uislam ni dini ambayo ina baadhi ya sheria zenye mirengo mikali sana, hakuna free will uhuru wa kiimani kwamba unaweza kuchagua dini nyingine, kukariri koran na kuomba kwa lugha usiyoijua, mistari yenye kuchochoea chuki dhidi ya wasio waislam, n.k.
Wakristo ni wapuuzi ...ndiyo maana wanasababisha majambazi na wahuni kuanzisha makanisa na makanisa ya kihuni kuongezeka nashauri waache kupeleka sadaka makanisani na wakipeleka isizidi buku tu vinginevyo ukristo utazidi kuchafuka
 
Makanisani wakristo wengi wakishatoa sadaka kanisani ndio shughuli imeishia hapo. Ni rahisi sana kuwakuta wachungaji mabilionea wanaotajirika kwa sadaka za waumini lakini kuna waumini wana changamoto zinazoweza kutatulika kwa milioni 10 ila wanaombewa badala ya kusaidiwa

Licha ya kwamba waislamu wengi ni maskini ukilinganisha na wakristo, Nimegundua waislamu hawatoi sana sadaka misikitini lakini huwa wanasaidia sana huku nje.

Nimewahi kupata shida ya maji na niliweza kuchota maji bure kabisa msikitini wiki nzima.

Niliwahi kufikia sehemu sina pa kulala nilienda kanisani nikiwa muumini wa kanisa tangu mtoto lakini nilikataliwa kabisa, sehemu iliyonitunza ni msikiti, kanisa waweza kukuta lina mabomba ya kutosha ila ni kwajili ya matumizi ya kikanisa tu.

Mwezi wa Ramadhani ule mwezi mzima ni kawaida sana kuwakuta waislam wanasaidia vyakula watu wenye shida.

Waumini wana magonjwa ambayo yanatibika kwa milioni 10 lakini wachungaji wenye account zinazosoma Bilioni wapo kujifanya wanawaombea, Kweli? Haya kama sio maombi ya kinafki tuyaitaje?

Pamoja na mazuri haya kilichonitatiza kuhamia uislam ni dini ambayo ina baadhi ya sheria zenye mirengo mikali sana, hakuna free will uhuru wa kiimani kwamba unaweza kuchagua dini nyingine, kukariri koran na kuomba kwa lugha usiyoijua, mistari yenye kuchochoea chuki dhidi ya wasio waislam, n.k.
Naunga mkono Waislamu
 
Wakristo utoaji unaonekana wazi Tena mkubwa kaangalie shule zilijengwa na wakristo kuanzia chekechea ,msingi Hadi sekondari na Hadi vyuo vikuu ili.kuondolea waumini ujinga na kuwapa elimu ya uhakika shule

Pili kaangalie mahospitali yanayohudumia watu wote bila ubaguzi makubwa Hadi ya rufaa yaliyojengwa na Wakristo.Waoslamu kazo kugawa tende mwezi wa Ramadhani na kufuturisha watu au kugawa kakiroba la kilo kumi.kamoja mwezi wa Ramadhani.Maskinini anaishia tu kufuturu Ramadhani baada ya hapo anarudi kwenye Umaskini wake anasubiri Ramadhani ijayo
Hizo shule mnasoma bure, hospital mnatibiwa bure? Hiyo ni miradi ya kanisa sio msaada
 
Wakristo utoaji unaonekana wazi Tena mkubwa kaangalie shule zilijengwa na wakristo kuanzia chekechea ,msingi Hadi sekondari na Hadi vyuo vikuu ili.kuondolea waumini ujinga na kuwapa elimu ya uhakika shule

Pili kaangalie mahospitali yanayohudumia watu wote bila ubaguzi makubwa Hadi ya rufaa yaliyojengwa na Wakristo.Waoslamu kazo kugawa tende mwezi wa Ramadhani na kufuturisha watu au kugawa kakiroba la kilo kumi.kamoja mwezi wa Ramadhani.Maskinini anaishia tu kufuturu Ramadhani baada ya hapo anarudi kwenye Umaskini wake anasubiri Ramadhani ijayo
Maji ni muhimu kuliko kitu chochote.Bila maji mwanafunzi hawezi kwenda shule,kuoga,kufua,kwenda choo,kupika,vyote vinahitaji maji.Hata ukiumwa,kabla kwenda hospital,kunahitajika maji ya kuoga,kufua,kwenda choo,upikiwe uji,usafi wa deki,kunahitaji maji.Maji muhimu kuliko kingine chochote.
 
nikajua waislamu hawana kabisa utaratibu wa kutoa sadaka za fedha

The Icebreaker vipi huko kwenu
ZAKAH YA MSHAHARA -02

Namna ya Kutoa Zakah ya Mshahara.

Kuna njia mbali mbali.

Ya kwanza; thamani ya dhahabu.

Zakah ya mshahara inahusu fedha unayopokea (Net amount). Utatoa deni unalodaiwa na gharama za kiwango cha chini cha matumizi yako ya msingi na familia yako. Je kuna kinachobaki?

Ikiwa kuna kinachobaki utazidisha mara 12. Ikiwa jawabu lake ni sawa au imevuka thamani ya 85 gram za dhahabu au Tzs 12,240,000 atatoa zaka kwa kiwango cha 2.5%. Hicho kiwango kitakachopaswa kutolewa zakah atakigawa mara 12 na kutoa kila mwezi.

Kwa mfano 1. Unalipwa msahara 1.3 million. Gharama zako kwa mwezi ni 700,000/=

Baki ni 600,000 x 12 = milion 7.2. Nisaab ni milion 12,240,000.

Hivyo mfanyakazi huyu hatolipa Zaka kwa kuwa baki yake ipo chini ya nisaab.

Mfano 2. Mfanyakazi mshahara wake 3 million (net amount). Gharama zake za msingi ni 1 million.

Baki yake kwa mwezi ni 2mil ×12 =24million. Kiwango hiki kimevuka Nisaab ya 12,240,000 milion. Hivyo zaka yake itakuwa 24 mil ×2.5% = 600,000/= kwa mwaka huo.

Namna ya utoaji; 600,000 ÷12 = 50,000 kila mwezi.

Hivyo katika mshahara wake kila mwezi atatoa elf 50.

Njia hii inatumika nchini Sudan.

Njia ya pili; Thamani ya Kilimo.

Mtu ambaye anapata mshahara ambao unamuwezesha kununuwa 5 awsaq au kilo 653 za ngano au kilo 524 za mchele wa bei ya kawaida atatoa 2.5% ya mshahara wake.

Kwa mfano, mfanyakazi anapokea mshahara wa milioni 3. Na bei ya wastani ya mchele kwa mfano ni 2600 x 524 = 1.3 million.

Hivyo mfanyakazi huyu atapaswa kutoa zaka kila mwezi ya Sh 75,000 (3mil ×2.5%).

Yule anayepàta mshahara chini ya 1.3 million, hatolipa Zakah.

Njia hii inafuatwa na Indonesia.

Mwisho.

Rejea.
1. Dr. Yusuf Qaradhawi, Fiqhul Zakah Vol. 1.

2. The National Board of Zakat - The republic of Indonesia. Circular 17 of Sept, 2017.
 
Wakristo wengi wana matatizo, wengi hawajui wanachoamini. Ni kama vile wanaamini viongozi wao wa kanisa ndio Mungu wao, ndio maana unaweza kuona mkristo anaenda kanisani kuchangia milioni 10 wakati kwenye familia yake kuna mtoto kakosa ada.

Wakristo wengi wa kizazi hiki wamemuacha MUNGU na wanawatukuza viongozi wao wa kanisa. Kibaya zaidi ni kwamba, hao viongozi wa ibada ndio wamewatengeneza kuwa hivyo kwa maslahi yao binafsi.
 
Sio kweli, tunatoa kanisani na tunatoa nje japo hatujioneshi. Kaa ukilitambua hilo. Tunamuongozo wa namna ya kutoa kwa wahitaji mkuu.
Hakuna watu wanaotoa sadaka kwa sifa kuwazidi wakristo ndio maana kuna nyimbo kabisa za sadaka...sasa je tujiulize wakati wa manabii sadaka ikitolewaje?
 
Hakuna watu wanaotoa sadaka kwa sifa kuwazidi wakristo ndio maana kuna nyimbo kabisa za sadaka...sasa je tujiulize wakati wa manabii sadaka ikitolewaje?
Naona unaleta mashindano ya kidini. Hakuna anayetoa sadaka kwa sifa, wanatoa sadaka kwa kile Mungu alichowabariki na toka mwanzo watu walikuwa wanatoa sadaka tena kwa nyimbo za furaha na kumshukuru Mungu. Abeli alitoa Sadaka, Nuhu alitoa sadaka, Ubrahimu alitoa sadaka tena Fungu la Kumi kwa Melkizedeki. Musa alitoa sadaka kule Mlimani na hata wakati wa ujenzi wa Hema la kukutania walitoa sadaka kwa mioyo ya kupenda, shukrani na kuimba.

Wakati wa Daudi akiandaa ujenzi wa Hekalu walitoa sadaka kwa moyo wa Shukrani. Wakati wa Suleiman, walitoa sadaka. Wakati wa Yehoshafeti Mfalme walitoa sadaka. Wakati wa Zerubabeli hata wakati wa Yesu akiwa kwa jinsi ya Mwili alitoa sadaka na mwishowe akajitoa sadaka mwenyewe kwa dhambi zetu. Wakati wa Paulo na mitume walitoa sadaka za zaka,Mimbuko, Changizo na shukrani. Hata sasa tunatoa sadaka Makanisani, kwenye makusanyiko na kwa wahitaji.

Kimsingi, kuna sadaka aina 4 katika Ukristo.
1. Fungu la kumi/zaka. Hili hutolewa pale unapoabudia kwa ajili ya watendakazi wa Bwana.
2. Malimbuko. Haya ni mazao ya kwanza ya shambani/mifugo yako. Haya tunayapeleka kwa makuhani.
3. Shukrani- hii ni kwa kumshukuru Mungu kwa yale aliyotutendea. Hii unaweza Peleka kwa wahitaji.
4. Changizo hizi ni kwa ajili ya kuendeleza kazi ya Bwana. Hii walitoa wana wa Israel toka enzi za Musa wakati wa ujenzi wa Hema hadi wakati wa Paulo.
 
kitu ambacho siwezi kuruhusu familia yangu itumie ni hizi nyama za kugawiwa BURE kutoka misikitini.

Nyama za Kafara
We unawaza kafara tu!?..kafara kwenye uislam ni Haram,hutakiwi kula chakula Cha kafara ni Haram Kama nguruwe na pombe,Idd waislam hutakiwa kutoa chakula mashuhuri kwa masikini,hutoa m hele,nyama na mafuta bila kujali Imani ya masikini husika . uislam unasisitiza kusaidia wasiojiweza,ndiyo kazi ya zakka na sadaka, mtaani wakiristo wanazitwanga kinoma hizo nyama na huzingoja kwa hamu
 
Ni wakristo sio wakiristo
 
Back
Top Bottom