Wakristo wanatoa sana kwa wachungaji kuzidi kwa wahitaji, Waislamu wanatoa sana kwa wahitaji kuzidi kwa mashehe

Sasa hao hao Answar wanaenda mahospitalini na kutoa misaada ya vyakula na nguo bure

Kwangu mimi sadaka hiyo ina sauti kubwa kuliko sadaka ya Kinafiki

Kama ningekuwa Muislam ningekuwa Answar
Una hoja mkuu, sadaka inayowagusa wenye uhitaji ni sadaka njema sana kuitoa hata nafsini mwako unapata amani.
 
Kuna watu makini sana JF, nakupa 5 ya nguvu. Ukristu ni upigaji, nilihama huko baada ya kuwa na mashaka na "ufufuko ". Mungu wa kweli anaweza kumtoa mwanae kafara kweli?
Inawezekana kabisa.

Hata wewe kumtoa mwanao kafara unaweza ukiamua.
 
ZAKAH YA MSHAHARA -02

Namna ya Kutoa Zakah ya Mshahara.

Kuna njia mbali mbali.

Ya kwanza; thamani ya dhahabu.

Zakah ya mshahara inahusu fedha unayopokea (Net amount). Utatoa deni unalodaiwa na gharama za kiwango cha chini cha matumizi yako ya msingi na familia yako. Je kuna kinachobaki?

Ikiwa kuna kinachobaki utazidisha mara 12. Ikiwa jawabu lake ni sawa au imevuka thamani ya 85 gram za dhahabu au Tzs 12,240,000 atatoa zaka kwa kiwango cha 2.5%. Hicho kiwango kitakachopaswa kutolewa zakah atakigawa mara 12 na kutoa kila mwezi.

Kwa mfano 1. Unalipwa msahara 1.3 million. Gharama zako kwa mwezi ni 700,000/=

Baki ni 600,000 x 12 = milion 7.2. Nisaab ni milion 12,240,000.

Hivyo mfanyakazi huyu hatolipa Zaka kwa kuwa baki yake ipo chini ya nisaab.

Mfano 2. Mfanyakazi mshahara wake 3 million (net amount). Gharama zake za msingi ni 1 million.

Baki yake kwa mwezi ni 2mil ×12 =24million. Kiwango hiki kimevuka Nisaab ya 12,240,000 milion. Hivyo zaka yake itakuwa 24 mil ×2.5% = 600,000/= kwa mwaka huo.

Namna ya utoaji; 600,000 ÷12 = 50,000 kila mwezi.

Hivyo katika mshahara wake kila mwezi atatoa elf 50.

Njia hii inatumika nchini Sudan.

Njia ya pili; Thamani ya Kilimo.

Mtu ambaye anapata mshahara ambao unamuwezesha kununuwa 5 awsaq au kilo 653 za ngano au kilo 524 za mchele wa bei ya kawaida atatoa 2.5% ya mshahara wake.

Kwa mfano, mfanyakazi anapokea mshahara wa milioni 3. Na bei ya wastani ya mchele kwa mfano ni 2600 x 524 = 1.3 million.

Hivyo mfanyakazi huyu atapaswa kutoa zaka kila mwezi ya Sh 75,000 (3mil ×2.5%).

Yule anayepàta mshahara chini ya 1.3 million, hatolipa Zakah.

Njia hii inafuatwa na Indonesia.

Mwisho.

Rejea.
1. Dr. Yusuf Qaradhawi, Fiqhul Zakah Vol. 1.

2. The National Board of Zakat - The republic of Indonesia. Circular 17 of Sept, 2017.
Kwa hiyo Zaka wanatoa wenye ukwasi tu?
 
Sasa hapo chuki Iko wapi,we mpumbavu nini!?..kamsikilize Nyerere akiongea na wazee wa dar anaposema mkiristu alikua yeye na Mara moja moja bomani wengine wote walikua waislam enzi za kusaka uhuru,kiswahili neno sharti liwe na irabu
We jamaa unapenda sana kubishana Kwa matusi. Kwani ukijenga hoja bila kumtukana mtu huwa unapungukiwa Nini?
 
KWENYE KILA TAASISI YA DINI NAAMINI ILIANZISHWA KWA NIA NJEMA ILA KATIKA KILA JEMA LAZIMA KUNA WAHUNI WATAINGIA.
MFANO KUNA SIKU TULIPELEKA MZIGO PALE KANISA KUU KATOLIKI MOSHI YANI KRISTO MFALME, WAKATI TUNASHUSHA MZIGO TUKAOMBA MAJI YA KUNYWA KWA PADRI, TUKAONESHWA BOMBA MBELE YETU TUKANYWE. ILE TUMEFIKA KWENYE BOMBA TU ALITOKEA KIJANA MMOJA WA HAPO MISSION AKATUZUIA NA KUTUULIZA NANI AMETURUHUSU KWENDA KUNYWA MAJI PALE? TUKAMJIBU NI PADRI FLANI, AKATUTUKANA KISHA AKATWAMBIA KAMWAMBIE NIMEWANYIMA.
TULIONDOKA PALE KWA HASIRA TUKIAMINI MAJI HAYANYIMWI MTU ILA HUYU MWEHU SIJUI KATOKEA WAPI KAAMUA KUTUKATILI NA KIU YOTE HII YA JUA KALI LA SAA 7 MCHANA TENA NI MISSION NDIO TUNAFANYIWA HIVI!!!!!!
YANI MPAKA LEO NAOGOPA SANA HIZI TAASISI ZA DINI MAANA BAADHI YAO ROHO ZAO HAZIENDANI NA SEHEMU WALIPO.
 
Naomba nitoe elimu kidogo: Kuna wakristo wasio wakristo, hawa hawaujui ukristo kwa maana ya kwamba hawana uhusiano binafsi na KRISTO. Wakristo wasio wakristo wanapotoa sadaka wanaamini wanampa/wanamfadhili mchungaji!! Wakristo walio WAKRISTO (waliookoka) wanapotoa sadaka wanajua wanamtolea Mungu na ndivyo ilivyo!! Wakristo wasio wakristo wamezaliwa na wazazi wakriso ambao pia wanaweza kuwa ni wakristo wasio wakristo pia!! Mkristo wa kweli ni yule aliyeokoka.
Mh! Nahisi kama sijakuelewa?
 
Back
Top Bottom