Waislamu kumbukeni kujenga nyumba nzuri ya imamu karibu na msikiti. Pia maimamu na mashehe wawe na mishahara kama wakristo kwa wachungaji

MKATA KIU

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,883
6,314
Habari wadau.

Binafsi naishi karibu na imamu wa msikiti mmoja mkubwa tu Temeke. hali yake ya maisha inasikitisha .

Nyumba anayoishi na hali yake kiuchumi haiendani na huduma yake anayoitoa msikitini.

Waislamu msiwasahau viongozi wenu wa dini.

Wakristo wanapojenga kanisa huwa wanajenga na nyumba ya kuishi padri au mchungaji jirani na hilo kanisa

Mfano hili ni kanisa la katoliki Tabata Kisukulu. pembeni yake kuna nyumba ya nzuri ya ghorofa yenye appartments imejengwa kwa ajili ya padri na wahudumu wengine wa kanisa hilo

kisukulu nyumba.jpg

kisukulu1.jpg

WAISLAMU MNAPASWA KUIGA UTAMADUNI WA KUWAJALI WATOA HUDUMA KWENYE MISIKITI PIA. ILI NA WAO WAISHI MAISHA MAZURI
 
je Hali nzuri yake imekuja kwa kulipwa na Waislamu, ama hali nzuri yake imekuja kwa shughuli zake binafsi nje ya msikiti ?
Unapo zungumzia kulipwa na waislam me naona haijakaa sawa, sidhani hata kama upande wa pili nako kuko hivyo.

Misikiti karibia yote ina usimamizi, hao wasimamizi ndio wana jukumu la kulipa ma imamu wao kiufupi ni hivyo hapa ni public siwezi kuelezea kwa kina
 
Hata wale wanaojitoleaga kuwafundisha watoto madrasa pia wengi wao hali sio nzuri.

Wazazi ni wagumu kishenzi kuwalipa wale walimu, yaani mtu analipa milioni kadhaa huko shule mtoto apate elimu dunia ila buku 5 sijui 10 kwa mwezi kwa mwanae ili apate ilim akhera inamtoa roho.

Madrasa zinasaidia mno kushape watoto wa kiislam, mtoto mpaka aje kujiingiza kwenye upuuzi basi tayari ilim ya dini ipo kichwani na ipo siku akili ikimkaa sawa atamkumbuka Mola wake.

Tatizo ni wazazi wa kipindi hiki wagumu kutoa.
 
Kwanza unatakiwa ujuwe imamu ni nani tafsir yake ,pili imamu anaweza kuwa mtu yoyote ilikuongoza swala baada ya hapo anakuwa na shughuli zake za utafutaji kama kawaida ,siyo kuwa imamu anatakuwa kushinda msikitin haiko hivyo
Ndo anashaur wajengewe nyumba
 
Habari wadau.

Binafsi naishi karibu na imamu wa msikiti mmoja mkubwa tu Temeke. hali yake ya maisha inasikitisha .

Nyumba anayoishi na hali yake kiuchumi haiendani na huduma yake anayoitoa msikitini.

Waislamu msiwasahau viongozi wenu wa dini.

Wakristo wanapojenga kanisa huwa wanajenga na nyumba ya kuishi padri au mchungaji jirani na hilo kanisa

Mfano hili ni kanisa la katoliki Tabata Kisukulu. pembeni yake kuna nyumba ya nzuri ya ghorofa yenye appartments imejengwa kwa ajili ya padri na wahudumu wengine wa kanisa hilo

View attachment 2896396

View attachment 2896398

WAISLAMU MNAPASWA KUIGA UTAMADUNI WA KUWAJALI WATOA HUDUMA KWENYE MISIKITI PIA. ILI NA WAO WAISHI MAISHA MAZURI
Padre au Mchungaji ni full time job. Nadhani haiko hivyo kwa Waislamu. Ana kazi zake za kutafuta maisha nje ya Uimam.
 
Wachungaji wanasema hawalipwi mshahara ila wanalipwa pesa ya kujikimu 😂 mana kazi ya Mungu haina malipo
 
Back
Top Bottom